WCB watoa nyumba tano kama mchango wa waathirika wa mafuriko Iringa

WCB watoa nyumba tano kama mchango wa waathirika wa mafuriko Iringa

Lebo ya WCB imeahidi kutoa nyumba tano kwa ajili ya wahanga wa mafuriko mkoani Iringa kati ya 85 zilizoharibika.

x15534947_234819120279557_3664305946206666752_n.jpg.pagespeed.ic.xLIsM8Arae.webp


Diamond Platnumz ambaye ni bosi wa lebo hiyo amemuahidi Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliyetembelea kwenye ofisi za WCB kuwa watachangia nyumba hizo na kuzikabidhi siku ya sikukuu ya Christmas watakapokuwa wakitumbuiza mkoani humo.

Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameandika:

Tunakushkuru sana Mkuu wa wilaya Iringa Mh: Richard Kasesela kwa Kututembelea Vijana wako na pia kutukaribisha rasmi Iringa kuja kula Sikukuu ya X-mass tareh 25/12 /2016 kwenye [HASHTAG]#VodacomWasafiFestival[/HASHTAG] …lakini pia nitumie fursa hii kuwapa pole ndugu zetu wa IRINGA kwa kubomokewa ama kupoteza makazi zaidi ya 86 kutokana na Mafuriko yaliyotokea….kwakuamini kuwa sisi sote ni binaadam na kuwa la kwako ni sawa na la kwangu, tukiwa kama @Wcb_Wasafi tumeahidi kutoa Nyumba Tano kwajili ya wahanga hao na Panapo Majaaliwa tutazikabidhi Nyumba hizo siku tutayofika Iringa
1f64f.svg
….. ndugu zetu wapendwa kwa alie na chochote pia anaweza kuwachangia ndugu zetu wa Iringa, waweze fanikisha makazi ama Nyumba hizo 85….

Hongera RAIS DIAMOND
 
unaweza ukamsaidia mtu kutokana na kuguswa bwana prof ndumilakuwili , sio eti kwa sababu wao wamepanga ndio iwe kikwazo, kwan ww katika maisha yako hujawah kumsaidia mshkaji wako hata 2000? sasa kama ulimsaidia mshkaji wako 2000 ina maana haukuwa na ndugu yako mwenye shida ya 1000 mpaka ukampe mshkajo 2000? tuwe wazalendo jaman tuache longomba zisizo na maana
 
Vituko wanatoa nyumba tano msaada wakati wasanii na wafanyakazi wa WCB bado wamepanga!
Hiyo inaitwa Corporate social responsibility, nikurudisha sehemu ya faida kwa najamii na sio kwa wafanyakazi. Wafanyakazi wana vyao mabavyo ni posho, bonus na mishahara.
 
Wabongo mmezidi sasa yaani mpaka habari za misaada kama hizi MNAPOVUKA?
 
Hizo nyumba ziko wapi!? ...maana nasoma kuwa watazikabidhi watakayofika/kwenda Iringa hivyo nikadhani labda kuna mtu anazihifadhi kabla ya kuzipeleka kuzikabidhi.
Kumbe wakuu wa wilaya/mkoa Kagera walikosea kutokuja kuwaona WCB na kupiga nao picha labda nao wangeambulia walau nyumba moja.
Tulia we tomaso
 
Huyu blaza namkubali ila akepunguza media ..... angekuwa anafanya vitu kimya kimya Mungu angembariki sana .....
 
Huyu blaza namkubali ila akepunguza media ..... angekuwa anafanya vitu kimya kimya Mungu angembariki sana .....
Yeye kama msanii kioo cha jamii inabid afanye vitu vionekane ili kuhamasisha watu wengine watoe msaada.
Mungu huwez kumuongelea jinsi anavyobariki waja wake
 
Kwahyo hizo nyumba tano ni kwaajili ya nani maana wahanga ni wengi.
 
Back
Top Bottom