WE ARE SIMBA: Tukutane uwanja wa Taifa Jumapili 25 Agosti 2019

Simba usaliji yule kiungo na yule wakenya pale mko vizuri sema mkude atafutiwe mtu
 
Uko sahihi mkuu, ila hujajua tu maoni yako yashaanza kufanyiwa kazi, ukiangalia usajili ulivyo utagundua hilo.kilichobaki ni kocha kufanyia kazi, lakini kocha pia anapanga timu kulingana na alichokiona ktk mazoezi, huenda wakati wake bado, lakini soon mabadiliko utakayo yatakuja
 
believe me or not kwa ninavomjua uchebe kuna wachezaj wake piga ua lazima awapange.. labda kama wanaumwa..just kwa mfano ile gem ya ud songo boccp hakuwa fit kabisa alionyesha poor perfomance lakin alimaliza mechi..na wawa the same....hapo ndo huwa namkumbuka kocha mmoja alikuwa anaitwa loga yeye kukuingiza na kukutoa hapohapo haikuwa shida kwake
 
Uko sawa kwa Sergi WAWA kupumzika... lakini hata pale kati ukabaji wa middle zetu sio mzuri sana.
Hii inafanya mabeki kuwa na eneo kubwa la kuzuia mashambulizi viungo wakipoteana.
 
Ndio mkuu yeye Ndio ana haribu na Boko mara nyingi mkude pass anatoa kwa wapizani hayupo accuracy
Hao wote wapumzishwe mwalimu awape program ya mazoezi. Nafasi ya Bocco anayo Mbrazil majeruhi. Nafasi ya Mkude aaminiwe Mzmiru na Fraga Viera
 
Upo sahihi mpira unachezwa hadharani kila mtu anaona. Mungu anisamehe ila kuna kipindi Boko na Wawa wakipata majeraha ya kuwa nje huwa naona afadhali
 
Juzi mechi ya azam uwanjani pale palikuwa pomoni,ilikuwa hata sehemu ya kuweka mguu ha kun a,kweli simba kiboko
 
Nikianza na mechi iliyopita kule Msumbiji ni kuwa kwanza UD Songo walikosa umakini katika umaliziaji na hata bahati hawakuwa nayo kwani mechi ingekuwa imeishia kule Msumbiji na Simba tungekuwa tumeshatoka kwani walikosa clear goli zaidi ya tano ndani ya box la Simba. Na uchebe naye alimng'ang'ania Boko wakati ilikuwa wazi hata kwa mtu asiye na taaluma ya ukocha kuona kuwa Boko mpira ulimkataa. Wachezaji duniani kote inatokea kuna siku mpira unamkataa sio kitu cha ajabu lakini Uchebe aliendelea kumng'ang'ania Boko na sijui hata makocha wasaidizi kazi yao ni nini hasa kama wanashindwa hata kumshauri kocha mkuu afanye mabadiliko.

Sasa hivi watu ndio wanaanza kuyaona mapungufu ya Wawa, Nyoni na Mkude. Lakini haya yote tuliyapigia kelele sana hapa jamvini na viongozi wakaziba masikio wakati wa usajili. Tuliandika hapa wasiache kumsajili Kotei bila kupata mtu sahihi wa kuziba nafasi yake kwani ndiye aliyekuwa anafuta makosa yote ya akina Mkude, Nyoni na Wawa. Na hata Simba ikifanikiwa kuingia kwenye makundi matokeo ya mwaka huu hayatokuwa na tofauti na ya mwaka jana kwa sababu ya upungufu wa kiungo mkabaji mwenye uwezo kama Kotei. Watu wengi na hata viongozi wanasema Shiboub ndiye mbadala wa Kotei. Jibu ni hapana, Shiboub ni kiungo mshambuliaji japo ana uwezo mkubwa wa kukaba. Ndio maana mara nyingi sana hata kwenye mchezo wa juzi alikuwa anaonekana katika box la Azam. Sasa kwa timu zinazopiga counter attack zenye washambuliaji wenye kasi watakuwa wanawakuta Mkude, Wawa na Nyoni bila ya msaada wa mtu wa nne ukizingatia wote hao hawana kasi na hawawezi kumvaa mtu kama alivyokuwa anafanya iron man Kotei basi hapo ni majanga tu.

Viongozi niwapongeze kwa kukubali ushauri wa wadau wengi waliotaka Kapombe aongezewe mtu wa kumsaidia na wakakubali kwa kumsajili Shamte.

Ushauri wangu kwa viongozi timu ikifanikiwa kupita makundi tafuteni beki wa kati mmoja aliye tayari kwa mashindano sio wa kusikilizia kama hao wabrazili kwani mpaka sasa hawajulikani kama wapo vizuri au ni majanga.

Najaribu kujenga picha kuwa Kotei yupo na Mkude kiungo cha chini (hapa Wawa na Nyoni wangekuwa salama) halafu Shiboub yupo kiungo cha juu halafu Chama na Dilunga wanatokea pembeni kwa kweli hata Al Haly angekufa pale Misri.

Ni mtazamo tu.
 
[emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji83][emoji83][emoji83][emoji83]
 
Hivi simba hawana graphic designer?? Mbona matangazo yao mabaya sana kulingana na ubora wa Club
 
upo sawa mkuu wote ni washabik wa simba tusijifarij saana kwamba tuna timu nzur bado ukuta wetu ni janga kubwa. pale nyuma tungekuwa na combineshen kama ya yokub na agrey wa azam na tungepata mtu kama bwalya angalau tungesema tuna uhakika hata wa kufikia record ya mwaka jana. Kwa simba hii na uchebe jins alivyokariri wachezaj tutafika makund kwa vile droo imetubeba kiaina. Replacrment ya wawa na bocco ni inevitable. Afu na sisi tunapenda sana vya bure huwez tegemea kupata jembe la maana kwa kusubir wachezaj waliomaliza mikataba ndo uwasajil. Watu wanavunja bank, Kwa simba level yetu kubwa itakuwa kwenye makundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…