SoC03 "We! Mmmmhh ni wewe, hapana sio wewe ni wewe" alisikika rafiki wa maisha akimuita Naisha

SoC03 "We! Mmmmhh ni wewe, hapana sio wewe ni wewe" alisikika rafiki wa maisha akimuita Naisha

Stories of Change - 2023 Competition

KABOYATU

New Member
Joined
May 8, 2023
Posts
3
Reaction score
2
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Hahaa!! Acha nicheke nifurahi, nikakumbuka hadithi ya "Nani amfunge paka kengele" niliyofundishwa na Mwl Ludao ๐Ÿ˜€ Mmhh, nyie! Acha kabsaa, ukiachilia mbali ile hadithi ya Mwl Kukome "Sizitaki mbichi hizi".

Ukiachilia mbali maswali yangu niliyouliza kutojibiwa zaidi ya kuambiwa kua uyaone ๐Ÿ˜‚, nilishitushwa na sauti ya rafiki yake Maisha akimwita Maisha, licha ya sauti kubwa aliyokuwa akitumia. Cha ajabu, utamshangaa Maisha, yeye haitiki wala kumfata rafiki yake! Sijui tatizo lilikuwa nini?

Ila pengine rafiki yake Maisha aliona nikikaa na rafiki yangu, nimepata vyote. Cha kushangaza, wapambe wa Maisha ndiyo waliokuwa wakiitika, sio Maisha!! Eee ndiyo ๐Ÿ™„ unashangaa nini sasa, kwani hujui Maisha ana wapambe? Tena wengi.

Acha nikutajie wachache: Uongozi, imani, magonjwa, uchumi, na pesa. Hao ni baadhi tu, mmmmhhh! Ulifikiri wameisha? Wapo kwanza, hembu subiri!!! Aaah ๐Ÿ˜Ž nimekumbuka, hata kama chakula ni kitamu sana na kimepikwa kwa ustadi na usafi wa hali ya juu, ukila sana utavimbiwa tumbo. ๐Ÿ˜€

Kwani rafiki yake Maisha ambaye alikuwa akimwita Maisha ni nani? We!! Uko serious unataka kumjua!!! Aaaah! Achana naye, tuzungumzie wapambe wa Maisha:

Tuanze na huyu mpambe kiherehere "Uongozi".

Ni mfumo wa utawala ambao hutengeneza mifumo na sera mbalimbali za kushikilia Maisha ya rafiki yake Maisha. We! Mimi sijatumia kamusi, nimeongea tu kutokana na mnuno Maisha alipoitwa na rafiki yake.

Anyway, uongozi una viongozi, je, kiongozi ni nani? Mimi mzee wa mifano bwana; kwani nini, usinionee tu kwani ukinisoma utapungukiwa mini. Kwanza hapo ulipo una stress za madeni ๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ๐Ÿ˜๐Ÿ˜Ž. Dereva akiwa anaendesha gari ni kiongozi! Unaonaje akilala wakati anaendesha!! ๐Ÿคฉ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜‚ Usipige yowe!::

Kiongozi ni mtu anayeijua njia ambayo watu wanatakiwa kupita. Vipi!!!?

Huku kwetu kuna mmoja kawa kipofu, sisi tukaona kabla yake. Tukamwambia Mh: umekosea njia, akabisha. Sio tukaona sio tabu, tukae chini kaenda peke yake porini. Maendeleo yetu yakadumaa.

Sasa wakati tulipokaa chini, tukaupoteza muda. Tukaanza kujiuliza kilichotufanya tusiendelee kwenda na njia sahihi tulioiona ni nini? Na kwanini tumeshababisha hasara ya muda kiasi kile? Tukajua uzembe, ubishi, kutojali maisha yetu na wanaotutegemea, kumetufanya kuwa wabinafsi, hivyo kusababisha watoto wetu kukosa maisha bora.

Bado tu unataka kumjua rafiki yake Maisha aliyekuwa akimuita Maisha? Nisubiri, nakuja โ˜บ๐Ÿ˜.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom