We si unaona kingereza dili..ebu msome jose chamelion

We si unaona kingereza dili..ebu msome jose chamelion

Heri umasikini wa mali kuliko wa akili....Lugha ni kitu muhimu sana ukiweza kujua lugha hata kumi ni vizuri kwako..ila wanaodharau Lugha ya kwao ni wajinga kupindukia.
 
Tatizo la mjadala wa lugha hapa Tanzania ni ile polarization ambayo inalenga au kukikuza Kiswahili na kupuuzia mengine, au kukikuza Kiingeraza na kupuuzia Kiswahili. Watu wanaotoa mifano ya nchi za Ulaya, kwa mfano, watakuambia kwamba kule wanatumia lugha yao ya Kidachi. Lakini masharti ya shule ni lazima usome lugha nyingine mbili kikiwemo Kiingereza. Zingatia hapo: Lugha yao kwanza, na lugha nyingine ni lazima.
Isitoshe, wanafunza hizo lugha nyingine kikweli si kubabaishaji. Mjadala wa lugha hapa TZ mara nyingi unasahau kwamba kwa miongo mingi sana, lugha zote mbili Kiingereza na Kiswahili zimefundishwa vibaya mno au hazikufundishwa kabisa pengine. Kuna wakati tulikuwa tunajaza vyuo vya ualimu vijana waliofeli masomo yote, kikiwemo Kiswahili. Watu hao ndiyo walioenda kufundisha baadae katika shule za msingi. Uzoefu wangu ni kwamba hata sekondari walimu wengi hawana ujuzi wa kutosha kufundisha Kiswahili. Achia Kiingereza, Kiswahili tu kwanza hakifundishwi vema.
Nimebahatika kuona mfumo wa elimu huko Marekani pia. Katika vyuo vikuu huko, wanafunzi kwanza lazima wasome madarasa kadha ya Kiingereza (lugha yao), wanajizatiti katika stadi mbalimbali: reading, college writing, etc Sasa turudi kwetu TZ, Kiswahili kilishatupwa baada ya Form IV kwa kiwango ambacho hawajakisoma vizuri. Na Kiingereza, je? Tumewaachia mangwini chuoni maana hawana jingine la kufanya. Halafu tukienda nje Kiingereza kikatugonga, tunasingizia Kiswahili ndiyo kimeleta taabu hiyo.
Nahitimisha, lugha ya kwanza kutiliwa mkazo ni Kiswahili. Wanafunzi wakijifunza Kiswahili vizuri wataweza kuhamishia stadi zao kwenye Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kireno, nk. Kwa hakika tunahitaji lugha kama tatu na si mbili tu. Nitoe mfano tu mdogo. Kuna watu wanamaliza vidato na hawajui sentensi ni kitu gani, hawajui jinsi ya kusoma haraka haraka upate pointi, hawajui jinsi ya kuandika muhutasari, nk. Fikiri mwenyewe kama mtu amepata stadi hizo ktk Kiswahili, ni rahisi sana kuhamishia kwenye lugha nyingine.
Mjadala usifinywe kwenye Kiswahili au Kiingereza, bali namna gani tunaweza kupangilia mafunzo yenye kuleta ufanisi na ustadi katika lugha tatu na zaidi.
 
Ni kweli kiswahili kidumishwe ila english pia muhimu ... nilikuwa nchi flan nikaenda hospital na hakuwepo hata dr kwa wakati huo anaeongea eng.. ilibidi nirudi na kupangiwa appointment siku nyingine kusomea majibu yangu akiwepo dr anaeongea eng. Kama ningekuwa sijui japo kidogo siijui ingekuwaje.

NI KWELI KWAMBA KIINGEREZA NI LUGHA INAYOFAHAMIKA NA KUTUMIKA NA WATU WENGI WENYE UTAIFA WA AINA TOFAUTI (NI LUGHA INAYOONGOZA KWA KUA NA MATAIFA MENGI YANAYOITHAMINI NA KUJIFUNZA NA PIA WENYE LUGHA WANAJITAHIDI KUIENEZA DUNIANI KOTE KAMA UTAMADUNI WAO NA KUPATA KIPATO KIKUBWA) ILA KISWAHILI NI LUGHA YETU YA TAIFA (TANZANIA) HATUNA HIARI KUJIFUNZA NA KUIFAHAMU KWA UFASAHA KAMA WENZETU WANAVYOKIENDELEZA KIINGEREZA.(Ni hatua kubwa sana kwa sisi watanzania kuanzisha lugha yetu binafsi, maana makoloni au nchi nyingi za Africa zilishindwa kuanzisha lugha zao binafsi na kuziendeleza baada ya Uhuru na mpaka sasa wanatumia lugha za wakoloni wao pamoja na za makabila yao na hakuna lugha ya pamoja wanayoifahamu kwa ufasaha(lugha ya kuwaunganisha na kujivunia kama kiswahili hapa TZ))

KWA SASA IDADI YA WATANZANIA INAONGEZEKA KWA KASI NA MATAIFA JIRANI WAMESHAPATWA NA WASI WASI KUHUSU KUFANYA BIASHARA NA WATANZANIA,NA WANAJITAHIDI SANA KUIJUA LUGHA YA KISWAHILI KWA KUJIFUNZA SHULENI AU KWA NAMNA YOYOTE ILE ILI WARAHISISHE SHUGHULI ZAO WAKIWA PANDE YOYOTE YA TZ.

KWA UCHUMI WA TANZANIA NI VIZURI TUKAJIFUNZA LUGHA YA KIINGERZA KWA UFASAHA MAANA ITATUSAIDIA KURAHISISHA SHUGHULI ZETU ZA KIUCHUMI HAPA TANZANIA NA NJE YA NCHI (HUKO WANAKOJIFUNZA KIINGEREZA KWA BIDII),HATA HUKO CHINA AMBAKO HAWAJUI KIINGEREZA,KWA MGENI UKIJUA KIINGEREZA CHA KUBABAISHIA NA CHA KWAO CHA KUBABAISHIA BIASHARA INAENDA:ILA KAMA HUJUI KICHINA NA KIINGEREZA NCHINI CHINA UTAPATA SHIDA SANA NA WAWEZA USIFANIKIWE KWA 100% KUFANYA SHUGHULI UNAYOTAKA KUFANYA.

UKWELI USIOFICHIKA NI KWAMBA KIINGEREZA KIMETAPAKAA KILA NCHI JAPOKUA KUNA BAADHI YA NCHI KUNA IDADI YA WATU WACHACHE WANAOKIFAHAMU KIINGEREZA (WATU HAO WACHACHE NI RAHISI KUWAPATA UKIWA NJE YA NCHI),UKIKIFAHAMU UTAPATA MSAADA WA MAWASILIANO NA UTATATUA SHIDA YAKO HUKO UGHAIBUNI NA TZ PIA:THAMANI YA KIINGEREZA HAIFANANI NA HIZO LUGHA NYINGINE TUNAZOZIITA LUGHA KUBWA.

KUJIFUNZA KIINGEREZA NI KITU MUHIMU KWA MTANZANIA,NA UNAPOJIFUNZA KIINGEREZA JARIBU KUUFIKIA UBORA UNAOTAKIWA NA SIO UBABAISHAJI.
ILA KISWAHILI NDO BABA LAO NDANI YA TZ.
 
wachina wanatumia hicho kingereza chako??
Ji**ga kweli wewe
Acha kuleta matusi bure bure hapa. Mnapenda kutumia videtails vidoogo kujustify mnachotaka kusema. Sucess behind wachina kuna factor nyingi sana zaidi ya lugha. Waliosoma chinese economy hili wanalijua. Lakini pia sasa hivi chinese wanajifunza english kama hawana akili nzuri. Kwa taarifa yako kuanzia elementary class in china kwa sasa hivi english subject ni lazima. Jiulize ni kwanini? Wameshaona hawawezi kwenda ulimwenguni bila kujua english. Sasa nyie ng'ang'anieni hicho kiswahili chenu halafu msijifunze english tuwaone.
 
kwa mtazamo mdogo nilionao, nahisi katika hili swala wadau wanachanganya kati ya lugha ya mazungumzo( hii huwepo kwa asili ya mtu katika eneo analokulia) na isimu ( sayansi ya lugha husika, ambapo hii ni lazima ujifunze kupitia katika taaluma ya isimu) ambapo hivi ni vitu viwili tofauti kabisa, kwahiyo jaribuni kuchanganua kabla ya kutoa hoja yako.
 
katika suala la lugha kwa sasa duniani tunaaswa kujua lugha za asili au lugha za mama huku tukijifunza na lugha angalau moja ya kimataifa ili kuweza kuwasiliana na watu wengi zaidi kadri tuwezavyo.
Na sio ajabu Jose Chameleone anaelezea mafanikio yake kutokana na Kiswahili huku akitumia lugha ya Kiingereza ambayo inatumika na watu wengi duniani, unadhani ni kwa nini hatumii Kiswahili hicho hicho kueleza hayo!?
 
Watu wangapi wanaojua kiswahili fasaha wamekuwa mamilionea kama Chameleone?
 
Back
Top Bottom