Kwa ujumla majibu ya mawaziri Bungeni yanachefua. Ni kweli wana majibu ya hovyo hovyo. Kuna Mbunge mwingine leo aliuliza kwa nini, OC za vyuo vidogo (akatolea mfano chuo cha maji) ni nyingi kuliko za chuo kikubwa kama Udom. Akaomba serikali ifikirie kugawa fedha za OC kwenye vyuo kulingana na ukubwa wa shughuli za cghuo. Waziri Maghembe katika majibu yake ya hovyo hovyo wala hata hakugusia iwapo hilo litafikiriwa, alisema tu kuwa hali ni mbaya sana kwenye vyuo hivyo vidogo wakati inajulikana kuwa hakuna chuo chenye hali nzuri kifedha.
Kuna Mbunge mwingine alilalamikia fedha kidogo zinazotengwa kwa UDSM and Mzumbe. Pia akasema hata hizo chache zinazotengwa, hazipelekwi zote. katika majibu yake ya hivyo hovyo, maghembe anasema serikali itajitahidi kuhakikisha vyuo vyote vinapatiwa fedha za kutosha, Alisema hivyo baada ya kulieleza Bunge kuwa hali ya kifedha serikali ni mbaya sana na ndio maana fedha zinatengwa kidogo.
yaani ni vigumu sana kulewa wanachojibu mawaziri kwenye maswali ya wangune.
lakini wanaoshangaza zaidi ni wabunge ambao wanakubaliana na majibu hayo.
Lakini hata Sitta si aliwahi kuahidi kuwu hatovulimia majibu ya hovyo hovyo kutoka kwa mawaziri?