Website mpya Air Tanzania BIGUP!!!!!

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Napenda niwapongeze AirTanzania kwa website mpya walau inayo kidhi mahitaji ya wateja na hata mwonekano mmepatia.

Kitengo cha ICT kinaonekana kimepata mtu makini kwa kuwa wasikivu.

Mkiwekeza kwenye ICT mtakua mna nia njema ya kulifanya shirika liwe na uahindani..

Wadau tunafurahi tunapo ona mambo mazuri kama haya yanafanyika.

Big up DG na timu yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mtu wa martketing amezingua..

Utawekaje nauli ya kukata ticket siku hiyo hiyo kama ndio benchmark?

Kwa namna hii kila mtu anaona air tanzania mpo ghali sana.

Hamjifunzi fastjet walivyo kua wanafanya.. matangazo yao ya gharama za ticket waliweka based kwa mtu anaye kata ticket mwezi mmoja kabla..

Mfano

Nikikata ticket leo na kusafiri leo toka mwanza hadi dar nalipa karibia 350,000 kwa safari moja..

Wakati nikikata kiketi mwezi mmoja kabla nalipa karibia 160,000 ..

Kwanini kwenye matangazo msiseme mtu anaweza safiri kwenda mwanza kuanzia 160,000 kuliko kutangaza nauli ya kukata siku hiyohiyo ambayo ni zaidi ya 350,000.

Msije tafuta mchawi, precision air kila siku wanatutangazia kuanzia 90,000 tunaweza kuafiri.

Mnatakiwa kuhimiza abiria kukata ticket mapema kwa kuonyesha punguzo la bei .. na hilo ndilo litakalo wapa uhakika wa biashara.


Nadhani kitengo cha marketing kina matatizo makubwa.

I love air tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli wamefanya vema sana timu ya IT.... Tatizo ndo hivyo kama ulivyosema kwenye market nao waige mfano.
 
Sahihi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…