Weekend unafanya nini? Ratiba yako ikoje?

Weekend unafanya nini? Ratiba yako ikoje?

kuangalia shows ninazopenda

kuandika code

kugombana na watu wangu wa karibu kisa siendi kanisani
 
Watu wengi haswa wenye shughuli rasmi kama biashara au ajira huwa wana mapumziko mwisho wa wiki.

swali langu ni je unautumiaje muda wako wa weekend ambapo hauna jukumu la kufanya kazi? Hebu toa ratiba ili watu wapate kujifunza.

Makala mbalimbali zinashauri vitu vya kufanya wikiendi:

1. Kujifunza mambo mbalimbali kama kozi pamoja na kusoma vitabu.

2. Kutembelea marafiki na kufanya mtoko wa kujivinjari.

3. Kufanya usafi na kazi za nyumbani kama bustani, ujenzi n.k.

4. Kufanya mazoezi.

5. Kujitolea/volunteer.

6. Kuanzisha project unayoipenda.

7. Kufanya maandalizi ya wiki inayofuata.

Hizi ni nadharia je uhalisia wako wa wikiendi ukoje?
Weekend ni Kanisani kwa ibada, Kupumzika , na kutembelea maeneo, ndugu, Jamaa na Marafiki
 
Hii kule 254 wanaita Aluta, jitahidi upunguze kwa ajili ya ubora wa uchumi na afya pia.
Bila uchumi na afya huwezi himili ile kitu mjomba, afya ninayo na buku mbili mbili kila weekend sikosi.
 
Hongera mkuu, kijijini kwneu watu hawana namna ya kujua yanayoendelea kupitia media na mitandao?
Wengi hawaelewi chochote ,mtu yeyote akinunua simu lazima ailete Mimi nimuungie Facebook ndiyo mtandao wanaoujua ila hawanunui simu mpaka nimewatajia simu nzuri .

Kijiji karibia kizima Wana aina ya simu yangu maana nilisema iko vizuri
 
Back
Top Bottom