ASHA NGEDELE
JF-Expert Member
- Jul 5, 2011
- 784
- 327
Habari wandugu,
Nasumbuliwa sana na unene na nimejaribu sana kufanya mazoezi lakini huishia kupungua kilo 3 hadi 5 alafu pindi niachapo basi hurudi kuongeza hadi kilo kumi. Kilo zangu zinacheza 95 mpaka 100 na urefu wangu hauzidi futi tano naa..
Nimejaribu pia kubadili life style karibu mwaka sasa, nimepunguza red meat, soda, heavy food intake at night na nimeacha kabisa sukari natumia asali kwenye kila kitu. Familia yangu ina asili ya miili mikubwa lakini siamini kuwa hakuna uwezekano wa kupunguza hizi kilo mpaka 75.
Nataka nijaribu kutumia supplements za kupunguza uzito kama hizi ambazo zinatangazwa sana na makampuni kama Forever Living na mengineyo ambazo wanasema ni natural.
Ushauri wa kidaktari au kifamasia naohitaji kwenu ni kwa kiasi gani dawa hizi zinaathiri mwili baada ya muda mrefu au mfupi. Nyingi ya dawa hizi wanadai ziko effective kwa muda mfupi sasa na unapunguza kilo nyingi sana sasa kuna uwezekano mkubwa dawa hizi zinaambatana na side effects ambazo zimejificha.
Naomba ushauri wenu kwani huu uamuzi wangu utabadilika kufuatana na ushauri wenu.
Asante.