Weinstein alitaka kulala na Lupita Nyong'o

Weinstein alitaka kulala na Lupita Nyong'o

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwigizaji huyo mashuhuri kutoka Kenya anaeleza jinsi ambavyo Harvey Weinstein, meneja ya kampuni ya utengenezaji filamu, alimnyanyasa kijinsia. Weinstein anasakatwa na sakata la unyanyasaji wa wanawake kadhaa.



Lupita ameliambia gazeti la New York Times kuwa alikutana na Harvey Weinstein kwa mara ya kwanza Berlin, Ujerumani, katika sherehe ya tuzo za filamu mwaka 2011. Kipindi hicho Lupita akiwa bado mwanafunzi katika chuo cha uigizaji nchini Marekani. Alikuwa na ndoto ya kuwa muigizaji mashuhuri duniani hivyo alipotambuliswa kwa Weinstein alifurahi.

Lakini mwanamke mmoja ambaye naye alikuwa mtaalamu wa filamu alimuonya Lupita kwamba Weinstein ni mtu mzuri lakini wakati mwingine anaweza kuwa mwenye mabavu. Lupita alimpa Weinstein mawasiliano yake, akitumaini kwamba atashirikishwa kwenye kazi za mtayarishaji huyo.

Muda mfupi baada ya kukutana Berlin Weinstein alimualika Lupita nyumbani kwake Connecticut, Marekani, kuangalia filamu. Dereva aliyeagizwa kumchukua Lupita kutoka nyumbani kwake alimtaarifu kuwa wanaelekea katika mgahawa ambapo Weinstein alikuwa akimsubiri kwa chakula cha mchana kabla hawajaelekea nyumbani kwake. Wakiwa hapo Lupita aliagiza kinywaji kisicho na kilevi, jambo ambalo halikumfurahisha Weinstein.

Baada ya mzozano Weinstein alimwambia mhudumu amletee Lupita kinywaji chenye kilevi kwani yeye ndiye anayelipia. Lupita hakupendezwa na hilo hivyo akaamua kunywa maji yaliyokuwa mezani. Walipofika nyumbani kwake Lupita na watoto wa Weinstein walikaa na kuanza kuangalia filamu.

Baada ya dakika kumi na tano Weinstein alimuita Lupita akisema angependa kumuonyesha kitu. Lupita alikataa kwani alitaka kufanya kile alichoalikwa kufanya lakini alipoona Weinstein anamshinikiza sana alikubali ili kutobishana mbele ya watoto wa Weinstein.

Wanawake wasema walibakwa na Weinstein


Weinstein ni mtengeneza filamu mwenye mafanikio na ushawishi mkubwa

Weinstein alimpeleka chumbani kwake na kumwambia kuwa anataka kumkandakanda. Lupita alidhani Weinstein anatania lakini baada ya kuona kuwa Weinstein anamaanisha anachosema ilimbidi kuwaza kwa haraka jinsi ambavyo ataweza kujitoa katika sehemu hiyo tata. Akikumbuka alivyojifunza shuleni jinsi ya kumkanda mtu, Lupita alimshawishi Weinstein amruhusu amkande.

Baada Lupitaya kumkanda mgongo, Weinstein alisema kwamba anataka kuvua suruali yake. Lupita alipatwa na hofu na kumwambia Weinstein kwamba hatafurahishwa na jambo hilo lakini Weinstein aliinuka na kuanza kuvua suruali yake. Hapo ndipo Lupita alipopata mwanya wa kutoroka na kusimama mlangoni.

Lupita alimwambia Weinstein kama hawaendelei kuangalia filamu ile ni bora arudi zake shule. Pamoja na hayo, Lupita anasema upo wakati mwingine ambapo Weinstein alimwambia anataka kulala naye. Alipokataa, Weinstein alimtishia kwamba jambo hilo litakuwa na athari kwa kazi yake kama mwigizaji.

Lupita si mwanamke wa kwanza kudai kwamba Weinstein alimnyanyasa kijinsia. Katika wiki zilizopita, wanawake kadhaa, wakiwemo nyota wa Hollyowood kama vile Gwyneth Paltrow wamejitokeza kusema kwamba Harvey Weinstein aliwanyanyasa kijinsia, alijaribu kuwabaka ama aliwabaka.

Weinstein ni mmiliki wa kampuni ya filamu inayofanya vizuri sana nchini Marekani. Kampuni ya Weinstein imetengeneza filamu maarufu kama Django Unchained, The Fighter na Mandela: Long Walk to Freedom.



DW
 
Jamii ya kidunia inabidi ibadilishe mtazamo kuhusu unyanyasaji wa kingono maana tunapoelekea huku hata wake zetu watatuambia tumewabaka au tunawanyanyasa kijinsia

Naona kama hili ni vuguvugu la kuendelea kuonyesha udhaifu wa mwanamke hasa pale anapohusisha mwili wake,kazi na mambo ya kibinafsi kupata faida na umaarufu, Rose McGowan ndiye aliyeanzisha kashfa hii ili kupromote kitabu chake anachotaka kukitoa

Mr.Weinstein kama ulivyo utamaduni wa kibinadamu alikuwa anatumia influence yake hollywood ili kuwamega wanawake wazuri so sioni kosa lake maana asili ya mwanamke ili umpate lazima umshawishi kwa jambo fulani ambalo litampa manufaa na ndio maana yeye amesema wote aliowagonga aliwagonga kwa makubaliano

naona jamaa ndio the luckest guy in the world....hahahah kuanzia Jolie,Cercei lannister mpaka Lupita
 
Story haijakaa sawa! Kupokea ile award alitekeleza zoezi zima asimung'unye maneno! Mtuhumiwa akitaka kueleza ukweli anyways kitu ambacho hawezi sababu hukumu yake anaweza kukosa kuliona jua kwa muda mrefu. Lupita na mtuhumiwa walimalizanaa banaaaa!
 
Mkuu una uhakika hii habari aina part two?

Mbona tukio la Lupita aliliwa au hakuliwa ujaliweka
 
Alichokifanya Harvey ni unyanyasaji was kingono huwezi kupinga. Yeye kama tajiri angeweza kutongoza mwanamke yoyote Yuko mitaani na wakakubali kirahisi tu. Yeye alichokuwa anafanya Ni kutongoza wanawake waigizaji na ma model ambao wanahusika na Kazi yake, aidha wako kwenye interview process au Kuna potential ya kutaka kuwaweka kwenye movie zake. Sasa unakuta wakimkatalia anawatishia au wanaogopa wakimkatalia ndo mwisho wa Kazi . That is sexual harrassment and abuse of power.

Na kwa taarifa yako ndio Kuna uwezekano wa mume kupelekwa jela Kwa kubaka make. Marital rape is real.


Jamii ya kidunia inabidi ibadilishe mtazamo kuhusu unyanyasaji wa kingono maana tunapoelekea huku hata wake zetu watatuambia tumewabaka au tunawanyanyasa kijinsia

Naona kama hili ni vuguvugu la kuendelea kuonyesha udhaifu wa mwanamke hasa pale anapohusisha mwili wake,kazi na mambo ya kibinafsi kupata faida na umaarufu, Rose McGowan ndiye aliyeanzisha kashfa hii ili kupromote kitabu chake anachotaka kukitoa

Mr.Weinstein kama ulivyo utamaduni wa kibinadamu alikuwa anatumia influence yake hollywood ili kuwamega wanawake wazuri so sioni kosa lake maana asili ya mwanamke ili umpate lazima umshawishi kwa jambo fulani ambalo litampa manufaa na ndio maana yeye amesema wote aliowagonga aliwagonga kwa makubaliano

naona jamaa ndio the luckest guy in the world....hahahah kuanzia Jolie,Cercei lannister mpaka Lupita
 
Back
Top Bottom