WEIZEI: Changamoto ya uzushi imeondoa changamoto ya Kupumua nchini?

WEIZEI: Changamoto ya uzushi imeondoa changamoto ya Kupumua nchini?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Nimewahi kusikia Wachina wanamsemo unaitwa WEIZEI wakiamini kwamba katika kila janga/ tatizo/ taharuki kuna fursa.

Kwa mtazamo wangu taharuki dhahania inayotengenezwa kuhusu kuugua/ mahali alipo Mkuu wetu na kusingiziwa vifo kwa viongozi wa upinzani, nikiiangalia Kichina naona kuna fursa ndani yake.

Fursa: Mjadala wa uwepo wa Covid kama umekufa. Kujadili hii kitu ni kutifua hofu, na hofu ni nywila ya kifo. Kimsingi leo wapambe wa Covid ukiwashtukiza wanaweza kukunasa makofi kwa kuwa haipo ika wanataka tujadili uzushi Mpya.

Ninaomba matokeo ya dhahama na hizi zushi mbalimbali Iwe ni kufutika kabisa kwa hofu na changamoto ya upumuaji ili kila mtu arudi kwenye uzalishaji bila hofu.

Wataalam na wafuatiliaji wa mambo; je, ni kweli kwa taharuki zushi hii imetuondolea taharuki ya Changamoto ya kupumua nchini?
 
Wapinzani wameisaidia CCM bila wao kujua sasa nchi imetulia bado jpm kuanza ziara kila kitu poa.
 
Sio umepungua ila katika nchi yetu la Mh kufariki kama ni kweli au uzushi ni kubwa zaidi kuliko hili la ugonjwa. Ugonjwa utaendelea kuwepo lakini Hili la Mh likiwa la ukweli hututawexa kumuona tena. Na ndio utakua mwanzo wa mwelekeo mpya wa nchi.
 
Na ungekuwa na akili kidogo tu ndio ungejua kuwa hiki kinachoendelea kimeegemea hapo kwenye COVID.
 
Wameingizwa mkenge na Tundu Lisu wa Ubelgiji!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ila huyo mtu kuna kitu atakuwa alikufanya, siyo kwa mapenzi hayo aisee. Mkuu mbona wanasema hata jiwe ishu yake ni Covid?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ila huyo mtu kuna kitu atakuwa alikufanya, siyo kwa mapenzi hayo aisee. Mkuu mbona wanasema hata jiwe ishu yake ni Covid?
Wanasema akina nani?

Robert Amsterdam?!!!
 
Kenya wapo sasa wanapambana na awamu ya 3 ya hicho kirusi hili jidubwasha bado lipo na linaendelea kubana tu pumzi za watu endelea kuchukua tahadhari afya yako ipo mikononi mwako hakuna mwingine aliyeresponsible zaidi yako
 
Nimewahi kusikia Wachina wanamsemo unaitwa WEIZEI wakiamini kwamba katika kila janga /tatizo/taharuki kuna fursa....
Hahahahaha duh hii ni kweli kabisa, yaani kila mtu anamuwaza Dkt Magufuli, yaani hata wale waliojifanya kutomtambua wanasema rais wetu, so funny, naipenda Tanzania, Mungu umlinde Dkt Magufuli huko aliko
 
Tuliwaambia watu tangu ileee kitambo last year kwamba Mr Mzungu anamtambua Anko kuwa Rais wake tena kutoka moyoni, watu wakawa wanabisha tuuu -- nadhani sasa wamepata jibu kutoka kwenye the so-called ^reliable source^ baada ya kushuhudia & kutamka yeye mwenyewe kwenye media za mabeberu wake!
 
Back
Top Bottom