robbyr
Senior Member
- Apr 8, 2017
- 129
- 221
Image source: Pinterest
Nyumba si gereza. Kutokana na mfumo wa ujenzi wa sasa ambapo tunaweka chuma kila dirisha na baadae tunavisha madirisha ya vioo (Aliminium) ni mihumu kuweka dirisha la dharura ambalo halitakuwa na chuma au likiwa na chuma ziwe ni slide pia.
Naandika andiko hili baada ya kupitia miezi kadhaa nikishuhudia nyumba ikiungua moto na ndani kulikuwa na mtu.
Mungu ni mwema kwani alikimbia chooni na waungwana walijitahidi kuvunja dirisha ambapo mmoja aliingia na kumtoa ingalia alikuwa amesharizai.
Naamini wewe ni shahidi wa habari hizi. Nahisi kuwepo kwa existing window tofauti na mlango kwenye baadhi ya vyumba au chooni kunaweza kusaidia katika uokoaji wakati wa janga la moto.
Narudia nyumba si gereza lazima tahadhari za usalama zizingatiwe.
Pia, wale wenzangu ambao jiko lipo ndani ni muhimu kuweka mtungi wa kuzimia moto kwa usalama zaidi. Nadhani wengi tunahisi mitungi ni kwa ajili ya kampuni na ofisi ila hata katika makazi yetu ni muhimu.
Na kabla ya kuwasha jiko hakikisha umekagua mfumo wa gesi ili kuhakikisha usalama.
Mwisho, kama unapika na upo mbali na jiko, weka moto kidogo ili chukula kiendelee kuiva taratibu kwani moto mwingi unaweza kukausha maji na baadae chakula na hata kusababisha mlipuko wa moto. Hili lilinitokea bahati nzuri ni moshi ulijaa ndani tu.
Asante sana kwa usikivu wako