Weka hapa tabia za ovyo za madereva wa bongo zilizojaa ushamba, ubabe, chuki na usela

Weka hapa tabia za ovyo za madereva wa bongo zilizojaa ushamba, ubabe, chuki na usela

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
  1. Dereva anataka kuingia barabarani toka barabara ndogo, au kukatisha barabara kuingia kulia, na wewe hutaki kumruhusu au kusimama ili aingie au kukatisha barabara.
  2. Unaruhusiwa kuingia barabarani au kukatisha na dereva mwingine, na wewe hutoi shukurani kwa ishara ya taa au hata kupunga mkono wa asante au thumbs up, umekaza uso tu kama vile barabara ni ya baba yako. Kukosa kuonyesha shukurani ni tabia ya kishenzi
  3. Mtu anataka kuku-overtake na wewe unaongeza spidi ili asiku-overtake, au asiingie mbele yako, japo ulikuwa unaenda taratabu
  4. Una-overtake kwenye jam, na upapoona kuna gari zinakuja mbele yako na kulazimisha kurudi kwenye line kwa ku-bully gari ndogo au za gharama kubwa bila hata kuomba kuingia
  5. Una-overtake kwenye Zebra crossing, au unaona kuna group la watu wanataka kuvuka barabara kwenye Zebra crossing, na wala hujali kuwapa nafasi.
  6. Kuna trafic jam, na sasa upande wa jam wanatengeneza lane mbili na kuwaachia upande wa pili nafasi kidogo ili wapite. Wewe unaamua kutengeneza lane yako ya tatu na ku-block magari yanayokuja, japo tayari tumelazimisha kuwa na lane mbili na kuwaachia nafasi kidogo. Huu ni ushenzi, wewe unataka wao wapite wapi?
  7. Kutoa ishara za matusi unapofanyiwa kitu kibaya na dereva mwingine - kwani wewe hujawahi fanya hivyo?
 
Back
Top Bottom