Weka hapa Uwongo wako ambao uliwahi kumwambia Mzazi wako ukiwa Sekondari na ukakusaidia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Binafsi niliitumbua Hela ya Ada niliyopewa na kule ambako nilitegemea kuipata nyingine mipango ' ikabuma ' hivyo ikanibidi niingie katika dhambi ya Kudanganya ambapo nilimseti Askari mmoja kuwa apige Simu kwa Mzazi wangu na aseme kuwa nimevamiwa na Majambazi na Kuporwa kila kitu hadi Ada yangu.

Baada ya hilo Biti la Askari Mshua alijipanga na baada ya kama Wiki mbili hivi Ada ilitumwa ambapo nilitoa sehemu kidogo nikampa yule Askari na nyingine nikaongezea na niliyoibakisha nikakamilisha Ada ya Shuleni.

Na Wewe sema Uwongo wako ambao ulikuja Kukusaidia ulipokuwa Shule ya Upili ( Sekondari ) enzi zako.

Nawasilisha.
 
Nilimiss msosi wa home kipindi npo boarding nkajifanya naumwa ili niende home kufika home mguu kwa mguu na maza hadi hospital kupima!
Kupima nkajikuta Nina malaria na typhoid na nlikua siumwi ilinibidi nianze dozi na misosi ya kuzidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…