Weka jambo lolote ambalo "Celebrities" wamefanya katika kusaidia Jamii

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Jee kuna jambo lolote ambalo umewahi kulishuhudia ama kulijua ambalo watu mashuhuri wa Tanzania wamewahi kulifanya kwa faida ya jamii?

Enzi kina Mr Nice, TMK wanaume, Wema Sepetu na wengineo na mpaka sasa enzi za Kina Diamond na wenzake nini hawa watu mashuhuri wamefanya kinachobakia kama alama ya wao kuwa waliwahi kusaidia jamii?

Jee kuna shule, Maktaba, Kisima cha maji, barabara, Maabara, Kanisa, Msikiti, au umeme wa jua uliowahi kutolewa na watu wetu maarufu wa Tanzania kwa ajili ya watanzania wenzao?

Au ni hamasa gani wamewahi kuisimamia kwa ajili ya jamii kama vile kuhimiza watoto wa kike kupelekwa shule, kuzuia mimba na ndoa za utotoni, kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala, vita dhidi ya madawa ya kulevya ama kuhimiza vijana kutumia vipaji vyao kwa faida ya watanzania?

Kama una jambo unalijua weka hapa ili na wengine tufahamu nani amefanya nini katika kusaidia jamii.
 
mchango wao mkubwa unaonekana kwenye kusambaza grid ya taifa aka dally kimoko
 
Kutoa video za pilau hakika wamekuwa msaada mkubwa kwa wanachaputa nadhani ni vzur wengine waige mfano wao
Hawa watu

_ rutty
_merry birian
_ufufuo
 
kutufundisha wanaume kusuka nywele na kunyoa kiduku.

kutufundisha kutembea peku kama wehu-mpoto

kutufundisha matusi

kuuza ngada na ushoga+usagaji

UMALAYA ULIOTUKUKA NA PICHA CHAFU MITANDAONI.

Mamama makubwa kuolewa na vijana wadogo kabisa eti uhuru wa mahusiano.

Mimi nawakubali Sugu, Haule, Mwegelo, Makini na kidogo Fid Q.
 
Diamond kwenye Birthday yake mwaka jana kajenga maktaba Tandale, katoa Bima za afya, kagawa mitaji... mambo kibao.

Licha ya kuwa na makosa wapo waliofanya kitu kwenye jamii
 
Diamond kwenye Birthday yake mwaka jana kajenga maktaba Tandale, katoa Bima za afya, kagawa mitaji... mambo kibao.

Licha ya kuwa na makosa wapo waliofanya kitu kwenye jamii
Bila kusahau ametoa mil 68 kuchangia ujenzi wa shule Sumbawanga.
 
Samatta akishirikiana na Alikiba waliandaa NIFUATE kuchangia madawati ya wanafunzi shule za dar es salaam na mikoa ya jirani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…