Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Jee kuna jambo lolote ambalo umewahi kulishuhudia ama kulijua ambalo watu mashuhuri wa Tanzania wamewahi kulifanya kwa faida ya jamii?
Enzi kina Mr Nice, TMK wanaume, Wema Sepetu na wengineo na mpaka sasa enzi za Kina Diamond na wenzake nini hawa watu mashuhuri wamefanya kinachobakia kama alama ya wao kuwa waliwahi kusaidia jamii?
Jee kuna shule, Maktaba, Kisima cha maji, barabara, Maabara, Kanisa, Msikiti, au umeme wa jua uliowahi kutolewa na watu wetu maarufu wa Tanzania kwa ajili ya watanzania wenzao?
Au ni hamasa gani wamewahi kuisimamia kwa ajili ya jamii kama vile kuhimiza watoto wa kike kupelekwa shule, kuzuia mimba na ndoa za utotoni, kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala, vita dhidi ya madawa ya kulevya ama kuhimiza vijana kutumia vipaji vyao kwa faida ya watanzania?
Kama una jambo unalijua weka hapa ili na wengine tufahamu nani amefanya nini katika kusaidia jamii.