"Weka jicho la umakini kwa marafiki zako"

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
SHERIA 2: Usiwaamini sana marafiki. Jifunze jinsi ya kuwatumia maadui.

MHADHARA WA 29:
Hii ni sheria ya 2 kati ya zile sheria 48 zilizoandikwa na Robert Greene katika kitabu chake cha "THE 48 LAWS OF. POWER".

Mapitio:
Weka jicho la umakini kwa marafiki zako, ni watu ambao wanakuwa na wivu na hasira kwa urahisi, vinginevyo watakudhoofisha. Usiweke imani kubwa kwa marafiki, jifunze jinsi ya kuwatumia maadui.

Mara nyingi tunapohitaji msaada tunawafuata zaidi marafiki huku tukiwaelezea kila kitu, lakini unapaswa kufikiria mara mbili kuhusu kufanya hivi kwa sababu hujui marafiki zako wanawaza nini.

Mara zote marafiki hukubaliana na chochote unachosema au unachofanya ili kuepuka mabishano hata kama unakosea, hiyo ni mbaya sana. Pia mnapokuwa marafiki kila mmoja anaficha makucha yake ili kila mmoja asimkasirishe mwenzake, kwahiyo huwezi kujua kwa hakika makucha ya rafiki yako yakoje.

Unapokuwa katika nafasi ya madaraka, au kiongozi wa kampuni jihadhari sana na tabia ya kuajiri marafiki. Kuajiri marafiki kunaweza kukuangusha kwa sababu ni mara chache sana rafiki yako kumfokea au kumkalipia kwa mabaya anayofanya au kukosea kwa makusudi. Hakika usipozingatia sheria hii fadhila zako zitakuangusha.

Pindi utakapoajiri rafiki kila mara atahitaji upendeleo wako, kwako utakuwa ni mzigo wa miiba. Bila shaka wivu na hila zake hazitopenda kukuona wewe una nguvu siku zote hivyo atatamani siku moja uwe chini yake. Kumbuka, yeyote anayependa kukuona unafanikiwa, kamwe hatopenda ufanikiwe zaidi yake.

Right Marker
Dar es salaam
Oktoba 3, 2024
 
Ukweli mtupu.
 
Mimi ninarafiki mmoja Tu ambaye ninamuamin na pia me Nina hiyo tabia nikiwa na rafiki nakuwa namuamin San
 

Mimi ninarafiki mmoja Tu ambaye ninamuamin na pia me Nina hiyo tabia nikiwa na rafiki nakuwa namuamin San
inshort me ni mtu muaminifu kwa rafiki Yang na ndomaana nikiwa na rafiki nakuwa namuamin🄺
 
Mambo ya urafiki ni unafiki tu ,mkizidiana kitu lazima husuda na chuki iingie kati.
Nakumbuka wakati niko O-level mwanzo mwa miaka ya 2000 nilikuwa na rafiki yanu mmoja ,tulikuwa close sana.kwao walinipenda na kwetu jamaa walimjua.Urafiki ulikufa baada ya jamaa kufail form 4,ikaonekana eti sababu ilikuwa mimi.kwamba mimi nilikuwa nasoma halafu yeye nikawa namdananya.Familia yao ilinichukia sana hadi leo sijui yule jamaa huwa yuko wapi.Nilikwenda kwao kuwaaa nakwenda 5 mama yake niliona sura yake haikuwa na furaha

Baadee nikapata rafiki maisha ya chuo,tukainia wote uraiani ila nikagundua jamaa alikuwa anpenda uarfiki umkopeshe pesa yeye tu ,mara asikulipe yaani stranger flani.ukiwa na shida pesa yake mgumu hata kukuazima,ila mimi ilikuwa bora nikope hata kwa wife kucover issue zake mwanangu asipate tabu,ila yeye alikuwa mgumu nikampotezea mazima

Huyu mwingine nikamconnect kwenye ajira nikajua ni mshikaji wangu ,kumbe akaungana na wapuuzi wenzake wakanisukia njama ili wanipige chini kazini.Ila Mungu ni mwema mshare ule ulinikosa ingawa nilipitia mengi mazito
upuuzi wa marafiki sitaki kabisa ,mostly ni wanafiki tu na hawapendi uwazidi kwa chochote ,wanasahau riziki ni mipango ya Mungu
 
Mh pole ndug
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…