RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
SHERIA 2: Usiwaamini sana marafiki. Jifunze jinsi ya kuwatumia maadui.
MHADHARA WA 29:
Hii ni sheria ya 2 kati ya zile sheria 48 zilizoandikwa na Robert Greene katika kitabu chake cha "THE 48 LAWS OF. POWER".
Mapitio:
Weka jicho la umakini kwa marafiki zako, ni watu ambao wanakuwa na wivu na hasira kwa urahisi, vinginevyo watakudhoofisha. Usiweke imani kubwa kwa marafiki, jifunze jinsi ya kuwatumia maadui.
Mara nyingi tunapohitaji msaada tunawafuata zaidi marafiki huku tukiwaelezea kila kitu, lakini unapaswa kufikiria mara mbili kuhusu kufanya hivi kwa sababu hujui marafiki zako wanawaza nini.
Mara zote marafiki hukubaliana na chochote unachosema au unachofanya ili kuepuka mabishano hata kama unakosea, hiyo ni mbaya sana. Pia mnapokuwa marafiki kila mmoja anaficha makucha yake ili kila mmoja asimkasirishe mwenzake, kwahiyo huwezi kujua kwa hakika makucha ya rafiki yako yakoje.
Unapokuwa katika nafasi ya madaraka, au kiongozi wa kampuni jihadhari sana na tabia ya kuajiri marafiki. Kuajiri marafiki kunaweza kukuangusha kwa sababu ni mara chache sana rafiki yako kumfokea au kumkalipia kwa mabaya anayofanya au kukosea kwa makusudi. Hakika usipozingatia sheria hii fadhila zako zitakuangusha.
Pindi utakapoajiri rafiki kila mara atahitaji upendeleo wako, kwako utakuwa ni mzigo wa miiba. Bila shaka wivu na hila zake hazitopenda kukuona wewe una nguvu siku zote hivyo atatamani siku moja uwe chini yake. Kumbuka, yeyote anayependa kukuona unafanikiwa, kamwe hatopenda ufanikiwe zaidi yake.
Right Marker
Dar es salaam
Oktoba 3, 2024