Biashara vipo Kwa category,Kuna daraj ala chini ambavyo vingi ni copy,Kuna daraja la kati vichache ni copy na og na Kuna daraja la juu huko ni no fake zone na bei nimesimama,fake zipo ila unakuwa makini tu
Madaraja hayo yanategemea na mtaji wako,aina ya wateja na eneo unaolouzia walipo aina hiyo ya wateja.
Kama unakaa uswahilini kwenye mtaa wa kawaida tu utahitaji daraja la chini Kwa maana watumiaji wengi ni kipato Cha chini na mtaji sio mkubwa sana
Na kama unakaa mahali Kuna watu wa kipato Cha kati hata chini unaweza changanya
Na kama una target wenye kipato Cha juu wale sijui lotion yake inauzwa 40,000-80,000
Bado vinakaa seti unakuta seti 150,000-300,000
Kuna mpaka set za milioni mbili
Hawa unaweka maeneo yenye potential za kibiashara na yanafikika toka mjini na pande zote,kama sinza,mwenge,kinondoni,mikocheni,kkoo,mbezi nk
Hata walio daraja la chini wakivihotaji wataagiza ama watakuja.
Mdada hawezi funga safari toka uswahilini mtaani mfano kigogo kuja kununua lotion ya 5000 mwenge,ataipata hapohapo mtaani
,lakini Kwa Ile og ya 50,000 anakuja
Upo kundi lipi?