Wekeza biashara watu wanapozichomea pesa zao, sio unapopapenda au kumuiga aliefanikiwa

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kuna kitu kinaitwa CPI - Consumer Price Index; kuna udambwi dambwi mwingi sana wa kichumi lkn kwa lugha rahisi maana yake ni -> bidhaa na huduma zinazotumika zaidi kwa mwezi katika kundi fulani la watu. ripoti ya CPI ya Tanzania inaandaliwa kila mwezi na National Bureau of Statistics (Ofisi ya Taifa ya Takwimu)

Ukitaka kujua vipaumbele vya watanzania, tunazika hela zetu ktk bidhaa gani, vitu ambavyo watanzania hawajawahi kuvutiwa navyo - lazima upitie report kama hizi. Sio mjasiriamali unaona wamarekani Silicon Valley wanasuka Softwares na wewe upo Kimara Baruti unaanza kusuka App ambazo wabongo hawawezi kua na muda nazo. Dec 2019 Jumia *kampuni ya mauzo mtandaoni) walifunga kazi zao wakarudi walipotoka. Kama mjasiriamali lazima ujue wadau wanachoma hela zao kwenye bidhaa zipi, uende huko ukazikusanye hizo hela

Kuna jamaa zangu Software eng. waliunda mobile App kali sana ya wagonjwa kukutana na daktari. sasa hivi nawaona wamerudi kwenye vitu ambavyo waTZ wanavielewa kama ku-burn CD, kupiga window, kuInstall Anti virus, kuFormat flash na kuwadanlodia wakulangwa internet. Watanzania wana vitu vyao, na huwezi kuwabadili mtazamo kisa umesoma sijui Oxford. Takwimu inasema matumizi ya waTZ yapo hivi

1. Chakula na vinywaji baridi - 38.5%
2. Usafiri - 12.5%
3. Pango, umeme, maji & gesi - 11.6%
4. Pamba kali na viatu - 8.3%
5. Fenicha, vifaa & urembo wa ndani - 6.3%
6. Vifurushi vya mawasiliano - 5.6%
7. Misosi ya hoteli na bata - 4.2%
8. Pombe na sigara - 3.7%
9. Vitu baki km kuhonga, kuzurura usiku, bidhaa zisizo za msingi - 3.1%

Vitu vitatu vilivyoshika mkia kabisa, wabongo hawana muda navyo kabisa na huwaambii kitu ni

1. Huduma ya Afya - 2.9%
2. Elimu - 1.5%
3. Uwekezaji - 0.01%

Sasa ukiona mtu ana degree ya pharmacy na anapiga uwinga wa nguo na viatu hp IG na WhatsApp status, inabidi uelewe kua yupo sahihi, sababu kama mtanzania anapata mshahara mil 1 kwa mwezi, atatumia 83,000 kununua viatu na 29,000 kununua dawa. fuata mkondo wa pesa sio passion. Bishana na yeyote ila usibishane na namba. Usipoteze muda wako kufanya vitu vice versa. Utaliwa kichwa boss!

Credits: Sir_Jeff
 
Chakula ndo haswa huwa naamini dili namba moja ndo mengine yanafuata.. inachotakiwa tu ukae kwenye mstari
 
Bado hapo lazima uende ndani zaidi kwamna kwenye Chakula una Target watu gani?

Chukulia mfano wa Azam.

Jamaa kwenye vyakula ana target sana lower class kwa sababu anajua huko ndo pesa zilipo na ndo kuna kundi kubwa sana.

Ukiangalia Azam ukwaju ile ni kwa ajili ya lower class na ndo wateja waliko.

Ukiangalia azam cola au Azam mandazi zote hizo ni kwa ajili ya watu wa Chini.

Hivyo unapo wekeza kwenye Chakula au Mavazi lazima pia ujue unalenga watu gani?

Na Kaa ukijua watumai pesa wengi ni wale wa daraja la Chini kabisa iwe Chakula iwe nguo iwe usafiri.

Middle claas ni wachache na sio watumiaji ukilinganisha na Lower Class ambao ni wengi sana.

Kwenye Afya nakataa hapo kwa sababu Afya ni moja ya sehemu ambazo watu wana spend by force wapende wasipende yaani no Choice,

Afya kuna Expenditure kubwa sana kwa sasa, nenda Kwenye Zahanati, nenda Hospitali kubwa nenda Kwenye Maabara za mitaani nenda kwenye Maduka ya dawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
QIF4TNk.gif
 
Kuna vitu ambavyo havina Mbadalawa wale yaani no Choice
1. Chakula
2. Usafiri
3. Afya

Hivyo havina kukwepa lazima tu ugharamike, kwenye elimu unaweza hata mtoto usimpeleke shule

hapo naona havina mbadala ila cha muhimu zaidi ni chakula, sehemu nyingi mtu anaweza kukaa mwezi mzima hajaspend kwenye usafiri yeye ni mguu wake au baiskeli, kwa afya hadi mtu aumwe ndo ataenda pharmacy. kwa vitu visivyokwepeka kuna chakula, maji, malazi (pa kulala) na nguo
 
Hata hapo kwenye elimu na afya nampa big no.
Katika watu wanaotajirika haraka ni watu wa afya hebu angalia akina Docta Ndodi walivyotajirika na huduma zao ni za kienyeji tu.
Angalia mahospitali kama TMJ,Kairuki na Rabininsia wanavyopiga hela na hakuna matangazo na wala hubembelezwi jino likikuuma lazima utaenda mwenyewe.
Kwenye mawasiliano hapo takwimu zako ziko chini sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe mkuu kwenye afya hapo jamaa amechemka.
Bado hapo lazima uende ndani zaidi kwamna kwenye Chakula una Target watu gani?

Chukulia mfano wa Azam.

Jamaa kwenye vyakula ana target sana lower class kwa sababu anajua huko ndo pesa zilipo na ndo kuna kundi kubwa sana.

Ukiangalia Azam ukwaju ile ni kwa ajili ya lower class na ndo wateja waliko.

Ukiangalia azam cola au Azam mandazi zote hizo ni kwa ajili ya watu wa Chini.

Hivyo unapo wekeza kwenye Chakula au Mavazi lazima pia ujue unalenga watu gani?

Na Kaa ukijua watumai pesa wengi ni wale wa daraja la Chini kabisa iwe Chakula iwe nguo iwe usafiri.

Middle claas ni wachache na sio watumiaji ukilinganisha na Lower Class ambao ni wengi sana.

Kwenye Afya nakataa hapo kwa sababu Afya ni moja ya sehemu ambazo watu wana spend by force wapende wasipende yaani no Choice,

Afya kuna Expenditure kubwa sana kwa sasa, nenda Kwenye Zahanati, nenda Hospitali kubwa nenda Kwenye Maabara za mitaani nenda kwenye Maduka ya dawa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kinaitwa CPI - Consumer Price Index; kuna udambwi dambwi mwingi sana wa kichumi lkn kwa lugha rahisi maana yake ni -> bidhaa na huduma zinazotumika zaidi kwa mwezi katika kundi fulani la watu. ripoti ya CPI ya Tanzania inaandaliwa kila mwezi na National Bureau of Statistics (Ofisi ya Taifa ya Takwimu)

Ukitaka kujua vipaumbele vya watanzania, tunazika hela zetu ktk bidhaa gani, vitu ambavyo watanzania hawajawahi kuvutiwa navyo - lazima upitie report kama hizi. Sio mjasiriamali unaona wamarekani Silicon Valley wanasuka Softwares na wewe upo Kimara Baruti unaanza kusuka App ambazo wabongo hawawezi kua na muda nazo. Dec 2019 Jumia *kampuni ya mauzo mtandaoni) walifunga kazi zao wakarudi walipotoka. Kama mjasiriamali lazima ujue wadau wanachoma hela zao kwenye bidhaa zipi, uende huko ukazikusanye hizo hela

Kuna jamaa zangu Software eng. waliunda mobile App kali sana ya wagonjwa kukutana na daktari. sasa hivi nawaona wamerudi kwenye vitu ambavyo waTZ wanavielewa kama ku-burn CD, kupiga window, kuInstall Anti virus, kuFormat flash na kuwadanlodia wakulangwa internet. Watanzania wana vitu vyao, na huwezi kuwabadili mtazamo kisa umesoma sijui Oxford. Takwimu inasema matumizi ya waTZ yapo hivi

1. Chakula na vinywaji baridi - 38.5%
2. Usafiri - 12.5%
3. Pango, umeme, maji & gesi - 11.6%
4. Pamba kali na viatu - 8.3%
5. Fenicha, vifaa & urembo wa ndani - 6.3%
6. Vifurushi vya mawasiliano - 5.6%
7. Misosi ya hoteli na bata - 4.2%
8. Pombe na sigara - 3.7%
9. Vitu baki km kuhonga, kuzurura usiku, bidhaa zisizo za msingi - 3.1%

Vitu vitatu vilivyoshika mkia kabisa, wabongo hawana muda navyo kabisa na huwaambii kitu ni

1. Huduma ya Afya - 2.9%
2. Elimu - 1.5%
3. Uwekezaji - 0.01%

Sasa ukiona mtu ana degree ya pharmacy na anapiga uwinga wa nguo na viatu hp IG na WhatsApp status, inabidi uelewe kua yupo sahihi, sababu kama mtanzania anapata mshahara mil 1 kwa mwezi, atatumia 83,000 kununua viatu na 29,000 kununua dawa. fuata mkondo wa pesa sio passion. Bishana na yeyote ila usibishane na namba. Usipoteze muda wako kufanya vitu vice versa. Utaliwa kichwa boss!

Credits: Sir_Jeff
Kwa mara ya kwanza tangu COVID aingie nimeona mtu ambaye ameshughulisha ubongo wake.
Thanks bro,
Ngoja kwanza niingie huko NBS nikashughulishe macho
Big up bro
 
hata hiyo malazi na nguo sio kivile kwa sababu kuna watu wanaweza kununua suruali mbili wakatoboa mwaka mzima usiwaone tena.
Na malazi pia kuna watu huwa hawapangi chumba wala nyumba yuko tayari akalale kwenye stoo za maduka,ila kuna watu kama wasambaa na wagogo akipanga geto mmoja wanakuja kukaa watu watano au saba.

Back
Top Bottom