Wekeza Kwa ndugu zako usaidiwe Majukumu!

Wekeza Kwa ndugu zako usaidiwe Majukumu!

Tatizo kipato mkuu, tunaumizwa kweli na matatizo ya ndugu zetu ila tunaumia kimya kimya maana hata tukiwaeleza ukweli hawatuamini na hawakwishi lawama.

Na hivi tuko mbali na mboni za macho yao basi wanafikiri tunakula bata kumbe bila bila tu.

Bado tunapambana kwa imani ila ndg punguzeni lawama.
 
Kweli mkuu....na hasa ndo kama upo ughaibuni wanaona huko hela mnazo kama zote....kumbe hawajui gharama za Maisha zipo juu sana
 
Tabu ni ndugu wengi wanapenda kitonga tuu, kazi yao gahawa na kashata.
 
Sasa utanunuaje gari kwa ndugu yako wakati umehamua kujitegemea kwenye maisha yako. Ondoa hiyo mentality maana hata kununua gari kwa ndugu ni sehemu ya kutegemea vya ndugu.

Badilika mzee nakushauri. Simama wewe kama wewe na amini ndugu hawezi kukuangusha kama hujihusishi nae au kumtegemea/ Usimpe adui yako plans zako wala malengo yako na pia usimweke karibu mtu ambaye una mashaka nae.

Maisha yana kanuni zake za kibabe ili uweze kutoboa ukiendekeza sana ndugu haswa maskini hutoboi maana utakuwa na mentality ya kimaskini
Bado hujanielewa kiongozi, Ni ndugu yako amefika mbali kimafanikio kisha anakuja kwa lugha ya kindugu kwamba akuuzie gari (ambalo yeye anajua fika ni bovu na linaweza kukufilisi) kwa pesa yoyote mtakayokubaliana ili akuboost kwa mtindo huo, nawe bila kujua nia yake ovu ya kukufilisi ukakubali mkauziana. Umeingia barabarani siku mbili gari limegoma, peleka gereji injini mbovu na huyo ndugu yako aliyekuuzia alilijua hilo na lengo lake akudidimize kabisa. Huoni huo ni upumbavu uliotukuka kumfanyia hivyo ndugu yako!? Mara umejenga nyumba nzuri, kaiona au akaumia anaanza kutafuta namna ya kukuharibia hata kwa mbinu za kishirikina. Huyo ni ndugu yako damu ya baba yako au ya babu yako anakufanyia hivyo ilhali hakusaidii chochote kwny utafutaji wako. Mkuu inauma sana.
 
Pole kwa yaliyokukuta lakini bado naliona hapo ni kujiweka karibu kwako na hayo ndugu ambao unajua kabisa ni watu wabaya. Mfano wako wa gari si mzuri kwa kuwa taratibu za ununuaji wa gari ni lazima uende na fundi akaliangalie na kujiridhisha. Hayo ya kurogana nayo ni imani tu ya mtu

Piga tu kazi zako binafsi na achana na ndugu zako. Ndugu ni watu wazuri sana ambao Mungu ametupatia ila kama wakiwa positive

Natamani nikushauri kitu ila ndio hivyo labda uje inbox. Mie nina tabia ya ajabu sana ambayo nilijifunza toka kwa wazungu (wajerumani) wakati nasoma huko. Wale hawachekeani na kila mtu anakomaa kivyake ili afikie malengo yake na mtoto akifikia 18 anaanzisha life kivyake. Kule mtu anajali mbwa wake kuliko ndugu yake. Kwetu huku sio vizuri kufanya hivyo ila wenzetu wana discipline sana na maisha

Nakuomba kama una ndugu haeleweki mweke mbali sana nawe maana nina imani hata kama mtu ni mbaya ukimweka mbali nawe inakuwa ngumu kukudhuru iwe kiroho au kiuchawi
 
Kuna kitu kimoja umegusia hapo khs wazungu kujali Sana mbwa kuliko ndugu yake....kiukweli wapo uzeeni wanajuta Sana hao wazungu...wanakuwa wapweke Sana kwakuwa hawakujali ndugu...wanabakia ktk majumba ya kulelea wazee na hakuna WA kuwatembelea...kwahiyo vyovyote itakavyokuwa tusiwatupe ndugu zetu.

Ila nakubaliana na wewe....wale wanaotudhuru tukae nao mbali.
 
Kwenye hiyo ya kujali mbwa nimesema kabisa kuwa kwa kwetu huku haitakiwa niliweka angalizo
 
Admin wa ndugu wa kiafrika ni mathias pogba anakiwasha kweli kweli huko.
 
Sina hakika kama umenielewa mkuu.
Haya. Mfano ndugu yako yuko juu na uwezo wake kiuchumi, ila wewe hata humtegemei yeye, unapambana kivyako, sasa umeanza kuzipata kiasi kwamba umeanza kumkaribia hivyo yeye anaanza kuwa na hofu kwamba sasa heshima yake itapungua akipata ndugu mwingine mwenye uwezo, anajaribu kukuangusha usifanikiwe mathalan anakuuzia gari ambalo anajua kabisa ni bovu ili ukilinunua likuhangaishe hadi uishe kabs au likupotezee muda na pesa nyingi udidimie. Ndugu wa aina hii ndio nimewazungumzia mimi. Hawafai kabs.
Sinunui kitu alichotumia mtu hata anishauri vipi, nitanunua changu basi, la sivyo anipe bure kikinishinda namrudishia

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Hii ndio ilipelekea TRA, Jeshini na CRDB kujaa watu wanaofanana fananafanana. Connection uncle
 
Sijamiss point yoyote. Nachokisema nimekiishi na nilihamua kufuata yangu na nimefanikiwa sana kimaisha ukilinganisha na watanzania wengi sana na nimewasaidia ndugu kwa mipaka kwa kuwa ukifungua milango kwa kila mtu ni tatizo kubwa sana

Nasaidia mtu lakini akiwa huko huko kwake na simzogezi karibu kwa kuwa wengi wanataka kula samaki bila kujifunza kuvua samaki

Nina miradi ambayo ndugu zangu walifilisi kabisa mpk nilihamua kutumia approach nyingine. Hapa nilipo nasomesha watoto watatu wa ndugu zangu na mmoja wa baba yangu alizaa uzeeni.

Tanzania ukiwa na uwezo na moyo wa huruma, nyumbani kwako kunaweza kugeuka kituo cha kulelea watu wazima waliobweteka kimaisha. Nililiona hilo mwanzo kabisa na niliweka kanuni za maisha

Ulevi na uzinzi wa ndugu zinarudisha nyuma sana wenzao katika familia zetu za kitanzania. Nimeongea machache tu kutoa sumu mwilini ila muhimu tufanye kazi na kujitegemea wenyewe na tuache kutegemea ndugu
Mkuu, unamzungumziaje ndugu ambae kafanikiwa ila yeye hataki wewe ufanikiwe!? Yan kwa sababu yeye kafanikiwa anaabudiwa ktk ukoo kama mtu muhimu mno (ubwana) sasa anaona nawe umeanza kuja juu kiuchumi, anakasirika na kuugulia moyoni, anakuwa anaongea na wewe vzr ila kinafiki huku akikutafutia tu pa kukuangushia nawe huna hata chembe ya shaka nae. Huyo ndugu unamzungumziaje!?
 
Kwanza mimi sijui kama ndugu wenyewe ninao,
 
Jamii zetu nyingi ni masikini na ni watu wachache Sana ambao ndio wamefanikiwa na hivyo kuwafanya wawe na majukumu mengi Sana katika ukoo....na kuwafanya wawe kimbilio ktk maswala mbali mbali yawe ya furaha na kuhuzunisha.

Na kibaya Zaidi ni kama vile watu hawa waliofanikiwa wanainjoi Sana kuwa wabwana wakubwa ktk ukoo au jamii Yao inayo wazunguka.....najua hapo akili yako imekliki paap je kwanini nasema hivyo! Relax....kama kawaida nyuzi zangu huwa zinasindikizwa na maudambu udambu...kamata popcorn au tende twende pamoja...

Naam wanapenda kuitwa mabwana wakubwa kwasababu....Ile Hali ya watu kuwafuata fuata na Kulia shida kwao wanaona raaaha Yani buruuudani! Yaani mtu akimcheki yeye kuwa ''anko Leo sipo vizur hata hela ya kula sina tafadhali naomba msaada wako'' wanapenda Sana yale mambo.....au ''brother Ada ya mwanangu imepelea naomba msaada wako'' ofcoz mifano IPO mingi Sana nadhani hata wenyewe mnaijua Sana Tu.

Na wengi wao kwakuwa wanapenda ukubwa ktk ukoo matokeo yake wanashindwa kuwasaidia ndugu kutoka kimaisha...ili waendelee kulambwa miguu kila siku ktk ukoo wao...kwasababu wengi wakifanikiwa ukubwa unaisha!

Napenda kuwashauri hawa mabwana kuwa hakuna ufahari wowote WA kuendelea kuwa hivyo kumbuka kuna kufa na kuna Leo na kesho....vipi mara paap! Kazi huna tena au biashara imeanguka hamuoni kwamba hapo ndo ukoo mzima umeanguka?

Ebu badilikeni sasa...Una uwezo wa kusomesha ndugu zako fanya hivyo,unauwezo wa kumpa mtu mtaji WA biashara fanya hivyo...Una konection ya kazi sehemu mpachike ndugu Yao aweze kujisimamia na kuendesha Maisha yake....hii itasaidia kuinua uchumi wa ukoo wenu na kesho au kesho kutwa mnasaidiana ktk majukumu mbali mbali na kukuondolea mzigo mzito ambao ulikuwa unaubeba wewe mwenyewe. Na kumbuka hata Kwa Mwenyezi Mungu utapata fungu lako kwani kusaidia watu ni IBADA.

Mtume Muhammad (rehma na Amani ziwe juu yake) alipohama kutoka Makka kwenda Madina....alimtengenezea mazingira swahaba wake mmoja aliyeambatana naye ili ajikwamue kimaisha au Kwa lugha ya sasa alimtafutia connection! Alikuwa Anaitwa Abdallarahmani raufu kama nitakuwa nimekosea hili Jina naomba nirekebishwe....sasa pale Madina kulikuwa kuna mtu mmoja Anaitwa Abu sadi...huyu alikuwa miongoni mwa matajiri wa pale Madina.

Basi Mjumbe wa Mwenyezi akamwambia Yule Tajir kuwa...nakukabidhi huyu bwana Abdallahraman umsimamie malazi yake na Kula yake...basi Yule Tajir hakuchukua uamuzi wa kukaa naye pale nyumbani na kumlisha na kumpa sehemu ya kulala Ila alitaka Ampe ndoano avue samaki mwenyewe...hakutaka ubwana ukubwa!

Cha Kwanza alimwambia ndugu yangu Nina wake wawili hapa basi chagua yoyote unayempenda Kati Yao kisha Mimi nitamuacha kisha umuoe wewe...najua baadhi yenu msio waislamu mnaweza shangaa daah inakuwaje tena jamaa anampa mwamba achague mke wake? Hayo yalikuwa mambo ya kawaida Sana Kwa waislamu kufanyiana kipindi kile ambacho waislamu walipotoka Makka kwenda Madina kukimbia mateso waliyokuwa wanafanyiwa na washirikina wa Makka....kwahiyo ndugu zao wa Madina waliwakirimu kwa kuwapa wake zao...tena sio kwamba labda anamwacha mke Fulani na kumpa ndugu yake muislamu laa! Bali anamwambia chagua unayempenda wewe nimwache umuoe Mashallah walikuwa wakarimu Sana...

Pili yule Tajiri akamwambia...katika hii Mali yangu...nitaigawa nusu mbili,moja yako na moja yangu tuendeshe Maisha yetu...ebu angalia jinsi hawa watu WA enzi zile wenye hofu ya Mungu walivyokuwa wanajali! Lkn ndugu yako Tu anakuomba laki mbili ya mtaji unamnyima na uwezo huo unao...pumbavu Sana! Lakini Yule anayesaidiwa akamwambia mwenyeji wake naomba tu unionyeshe soko lipo wapi penye kuuza na kununua Kwa maana akafanye biashara na hakuhitaji hela zake...ingawa huenda alimpa cha kuanzia biashara au mtaji.

Undugu ni kusaidiana kuonyeshana njia....kupeana ramani na kupeana ushauri ili wote msonge mbele na si kuwabania wenzako ili ubakie bwana mkubwa na kupata sifa za kijinga.

Ni hayo tu
Mabro wapo level za management kwenye taasisi mbalimbali ila hawataki kutupa connection za job , ila izi koo zimekuja kuwa za kiwaki wa juu hataki wenzake wafike juu, na mwenye success hataki wengine wawe successful
 
ndugu Wengi ni nux sana familia chache zinaweza kunyanyuana ila ndugu wengi wapo kukudidimiza me sinaga shobo na ndugu zaidi ya kujuliana hali kukutana kwenye matukio ya kifamilia ila swala la kufanya jambo la maendeleo pamoja mhh naona anguko langu hili hapa[emoji41]
 
Back
Top Bottom