Wekeza Kwa ndugu zako usaidiwe Majukumu!

Tatizo kipato mkuu, tunaumizwa kweli na matatizo ya ndugu zetu ila tunaumia kimya kimya maana hata tukiwaeleza ukweli hawatuamini na hawakwishi lawama.

Na hivi tuko mbali na mboni za macho yao basi wanafikiri tunakula bata kumbe bila bila tu.

Bado tunapambana kwa imani ila ndg punguzeni lawama.
 
Kweli mkuu....na hasa ndo kama upo ughaibuni wanaona huko hela mnazo kama zote....kumbe hawajui gharama za Maisha zipo juu sana
 
Tabu ni ndugu wengi wanapenda kitonga tuu, kazi yao gahawa na kashata.
 
Bado hujanielewa kiongozi, Ni ndugu yako amefika mbali kimafanikio kisha anakuja kwa lugha ya kindugu kwamba akuuzie gari (ambalo yeye anajua fika ni bovu na linaweza kukufilisi) kwa pesa yoyote mtakayokubaliana ili akuboost kwa mtindo huo, nawe bila kujua nia yake ovu ya kukufilisi ukakubali mkauziana. Umeingia barabarani siku mbili gari limegoma, peleka gereji injini mbovu na huyo ndugu yako aliyekuuzia alilijua hilo na lengo lake akudidimize kabisa. Huoni huo ni upumbavu uliotukuka kumfanyia hivyo ndugu yako!? Mara umejenga nyumba nzuri, kaiona au akaumia anaanza kutafuta namna ya kukuharibia hata kwa mbinu za kishirikina. Huyo ni ndugu yako damu ya baba yako au ya babu yako anakufanyia hivyo ilhali hakusaidii chochote kwny utafutaji wako. Mkuu inauma sana.
 
Pole kwa yaliyokukuta lakini bado naliona hapo ni kujiweka karibu kwako na hayo ndugu ambao unajua kabisa ni watu wabaya. Mfano wako wa gari si mzuri kwa kuwa taratibu za ununuaji wa gari ni lazima uende na fundi akaliangalie na kujiridhisha. Hayo ya kurogana nayo ni imani tu ya mtu

Piga tu kazi zako binafsi na achana na ndugu zako. Ndugu ni watu wazuri sana ambao Mungu ametupatia ila kama wakiwa positive

Natamani nikushauri kitu ila ndio hivyo labda uje inbox. Mie nina tabia ya ajabu sana ambayo nilijifunza toka kwa wazungu (wajerumani) wakati nasoma huko. Wale hawachekeani na kila mtu anakomaa kivyake ili afikie malengo yake na mtoto akifikia 18 anaanzisha life kivyake. Kule mtu anajali mbwa wake kuliko ndugu yake. Kwetu huku sio vizuri kufanya hivyo ila wenzetu wana discipline sana na maisha

Nakuomba kama una ndugu haeleweki mweke mbali sana nawe maana nina imani hata kama mtu ni mbaya ukimweka mbali nawe inakuwa ngumu kukudhuru iwe kiroho au kiuchawi
 
Kuna kitu kimoja umegusia hapo khs wazungu kujali Sana mbwa kuliko ndugu yake....kiukweli wapo uzeeni wanajuta Sana hao wazungu...wanakuwa wapweke Sana kwakuwa hawakujali ndugu...wanabakia ktk majumba ya kulelea wazee na hakuna WA kuwatembelea...kwahiyo vyovyote itakavyokuwa tusiwatupe ndugu zetu.

Ila nakubaliana na wewe....wale wanaotudhuru tukae nao mbali.
 
Kwenye hiyo ya kujali mbwa nimesema kabisa kuwa kwa kwetu huku haitakiwa niliweka angalizo
 
Admin wa ndugu wa kiafrika ni mathias pogba anakiwasha kweli kweli huko.
 
Sinunui kitu alichotumia mtu hata anishauri vipi, nitanunua changu basi, la sivyo anipe bure kikinishinda namrudishia

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Hii ndio ilipelekea TRA, Jeshini na CRDB kujaa watu wanaofanana fananafanana. Connection uncle
 
Mkuu, unamzungumziaje ndugu ambae kafanikiwa ila yeye hataki wewe ufanikiwe!? Yan kwa sababu yeye kafanikiwa anaabudiwa ktk ukoo kama mtu muhimu mno (ubwana) sasa anaona nawe umeanza kuja juu kiuchumi, anakasirika na kuugulia moyoni, anakuwa anaongea na wewe vzr ila kinafiki huku akikutafutia tu pa kukuangushia nawe huna hata chembe ya shaka nae. Huyo ndugu unamzungumziaje!?
 
Kwanza mimi sijui kama ndugu wenyewe ninao,
 
Mabro wapo level za management kwenye taasisi mbalimbali ila hawataki kutupa connection za job , ila izi koo zimekuja kuwa za kiwaki wa juu hataki wenzake wafike juu, na mwenye success hataki wengine wawe successful
 
ndugu Wengi ni nux sana familia chache zinaweza kunyanyuana ila ndugu wengi wapo kukudidimiza me sinaga shobo na ndugu zaidi ya kujuliana hali kukutana kwenye matukio ya kifamilia ila swala la kufanya jambo la maendeleo pamoja mhh naona anguko langu hili hapa[emoji41]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…