Wekeza sasa kwa Scandinavia Express ijayo | Biashara ya Mabus

Hapa kuna co-member ambaye pia ni mmoja wapo wa atakayekuwa msimamizi nadhani maybe kwa kumfahamu yaweza kukupa picha ya kuwa tunaenda kutengeneza kitu kikubwa muda si mrefu

CC. Mshana Jr
 
Bahati nzuri nilipata pia nafasi ya kuongea naye ana kwa ana
 
Kwa kampuni changa ya kuunga unga kuanza kununua Scania kwa 710m sio sawa.

Anza na Chinese buses, ambazo angalau ni nafuu na pia ni Wazuri kwwnye kutoa mikopo
 
Kwa kampuni changa ya kuunga unga kuanza kununua Scania kwa 710m sio sawa.

Anza na Chinese buses, ambazo angalau ni nafuu na pia ni Wazuri kwwnye kutoa mikopo
Ni gari nzuri mno kimuoneka like Yutong,Higer etc,

Life Span ya gari la kichina maximum ni 3 years wanakupa guarantee ya matengenezo ya mwaka mmoja

Model ya business ya mabus yoyote ile inaweza kulipa gharama za manunuzi ya Bus ndani ya Miaka 3 nje na interest

Ikiwa na maana Gari litakufa kabla hujamaliza kulilipia interest, faida utaipatia wapi??

kwa kampuni zilizokuwa like Shabiby etc anatumia gari mwaka mmoja guarantee ya matengenezo ikiiisha naye analiuza linaenda kumfia mwingine

UPANDE WA SCANIA
Bei iko juu kiasi hatukatai
Life span ya Bus ni matunzo yako ukilipa matunzo bora linaweza kukaa barabarani zaidi ya Miaka 10
Service Guarantee wanakupa ya Miaka 3
Hivyo unaweza malizia mkopo wa bus na ukawa na muda mrefu wa kutafuta faida yako ya kukutosha
 
Mkuu wazo zuri,Ila nafikiri utekelezaji wake unaweza badili approach

Mabus Tayari yapo Barabarani mengi tu ila mfumo wa usimamizi ndio changamoto.
Pili Gharama za Kumiliki Mabus zinachangamoto zake ila unaweza kuanzisha kama BUS Management Company ambapo wamiliki wa Mabasi wa sasa na Wapya wanaweza kuwa na Option ya Kuwakodishia mabus Yao.Mnachopaswa kuwekeza ni nini?

Mtandao Mzuri wa Vituo vya kupakia na kushusha Abiria,Mtaji hisa kwa ajili ya Gharama za uendeshaji,Vituo vya mafunzo maalum kwa ajili ya usimamzi wa Magari.Kituo cha Miito ya huduma kwa wateja,
 
Shukrani kwa wazo mkuu
 
Mawazo yako ni mazuri. Tena sana tu! Ila rangi yako ya mwili ndiyo itakuponza. Maana rangi nyeusi haiaminiki popote pale hapa Duniani. Tungekuwa ni Wachina, au Wazungu; muda si mrefu tungekuwa matajiri kupitia hili wazo lako.

Ingawa pia siungi mkono kwa route fupi na isiyo na misuko suko mingi ya Dar Dodoma; kutumia mabasi ghali kutoka kampuni ya Scania. Mchina tu (Yutong, Zhontong, Higer, Dragon nani sijui, nk) alikuwa anatosha kabisa kwa hiyo route..
 
Unaijua Mr Kuku, Vanilla International, Deci, Bravo Mills, Jatu?
Mkuu even kwa Marekani wameface utapeli mkubwa na failures kubwa kupitia Start-Up tokea zamani na hata sasa

Mfano
1.Theranos ya Mwanadada Elizabeth Holmes

2.FTX

3.Windows Phone toka Microsoft

4.Unaikumbuka Blackberry

5.Nikola, Electric Trucks

6.Worldcom

7.Quibi

8.Wirecard

9.WeWork Disaster

10.Enron

etc

Hatuwezi kuendelea ikiwa tunadhani kila project ama proposal inayokuja mbele yetu tukaitupa kwenye dustbin ya utapeli

Mara mia ukajaribu kuuliza ama kushauri tuweke kipengele gani ambacho kitawalinda wawekezaji kuliko kuishia kukosoa ukabaki hapo wadhani huo ndo uGreat Thinker??
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri.

Wacha nitarudi na info kidogo na maswali zaidi baada ya muda
 
Mimi nadhani kama mna hiyo 300m undeni kampuni ila watu waje na mabasi yao wawekeze. Nyie muwe wasimamizi wa shughuli zote za kampuni. Hao watakaoweka mabasi yao wawe wanapata tu mgawo. Kule Kenya kuna hizi gari ziko chini ya kampuni za namna hiyo.. kwa mfano NAEKANA SACCO ya Namanga - Nairobi. Hawa wamiliki wa mabasi machache wajisalimishe kwenu. Wawe shareholders. Kampuni yenu itakuwa imara maana kuna shareholder Mshana ambaye ni mchawi mwandamizi.
 
ungeomba kibali latra, bus zako tatu zifanye route ya dar to moshi na arusha (hakuna kulala), asubuhi zinageuka kurudi dar na abiria kama kawaida. hii route ina hela kinyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…