Wekeza sasa kwa Scandinavia Express ijayo | Biashara ya Mabus

Wekeza sasa kwa Scandinavia Express ijayo | Biashara ya Mabus

Hayo maelezo hayawezi kumshawishi mtu kuwekeza.
Kwanza lazima wenyewe wenye wazo muwe na kianzio au muoneshe taaluma yenu na uzoefu. Halafu muweke mpango wa biashara 'business plan'
Halafu muangalie sheria zinasemaje kuhusu kuitisha hisa au kuuza hisa bila kupitia soko la hisa.
Biashara ya usafiri ni rahisi kuanzisha ukiwa na mtaji ila ngumu kuifanya idumu.
Hapa kuna co-member ambaye pia ni mmoja wapo wa atakayekuwa msimamizi nadhani maybe kwa kumfahamu yaweza kukupa picha ya kuwa tunaenda kutengeneza kitu kikubwa muda si mrefu

CC. Mshana Jr
 
Biashara ya Mabasi ni moja ya boashara ngumu kama tu ya usafiri wa anga, na ukiangalia staffu ndio shida na hiu ni nature, ulimsikiliza yule tajiri wa Summury kitu alicho elezeaga kuhusu Biashara ya Mabasi?

Unawekeza pesa nyingi sana lakini mwisho wa siku kuba uzembe mkubwa sana hasa kwa Madereva.

Biashara ya mabasi ni sawa na biashara ya ndege,

Ila ni wazo jema
Bahati nzuri nilipata pia nafasi ya kuongea naye ana kwa ana
 
Kwa kampuni changa ya kuunga unga kuanza kununua Scania kwa 710m sio sawa.

Anza na Chinese buses, ambazo angalau ni nafuu na pia ni Wazuri kwwnye kutoa mikopo
 
Kwa kampuni changa ya kuunga unga kuanza kununua Scania kwa 710m sio sawa.

Anza na Chinese buses, ambazo angalau ni nafuu na pia ni Wazuri kwwnye kutoa mikopo
Ni gari nzuri mno kimuoneka like Yutong,Higer etc,

Life Span ya gari la kichina maximum ni 3 years wanakupa guarantee ya matengenezo ya mwaka mmoja

Model ya business ya mabus yoyote ile inaweza kulipa gharama za manunuzi ya Bus ndani ya Miaka 3 nje na interest

Ikiwa na maana Gari litakufa kabla hujamaliza kulilipia interest, faida utaipatia wapi??

kwa kampuni zilizokuwa like Shabiby etc anatumia gari mwaka mmoja guarantee ya matengenezo ikiiisha naye analiuza linaenda kumfia mwingine

UPANDE WA SCANIA
Bei iko juu kiasi hatukatai
Life span ya Bus ni matunzo yako ukilipa matunzo bora linaweza kukaa barabarani zaidi ya Miaka 10
Service Guarantee wanakupa ya Miaka 3
Hivyo unaweza malizia mkopo wa bus na ukawa na muda mrefu wa kutafuta faida yako ya kukutosha
 
Mkuu wazo zuri,Ila nafikiri utekelezaji wake unaweza badili approach

Mabus Tayari yapo Barabarani mengi tu ila mfumo wa usimamizi ndio changamoto.
Pili Gharama za Kumiliki Mabus zinachangamoto zake ila unaweza kuanzisha kama BUS Management Company ambapo wamiliki wa Mabasi wa sasa na Wapya wanaweza kuwa na Option ya Kuwakodishia mabus Yao.Mnachopaswa kuwekeza ni nini?

Mtandao Mzuri wa Vituo vya kupakia na kushusha Abiria,Mtaji hisa kwa ajili ya Gharama za uendeshaji,Vituo vya mafunzo maalum kwa ajili ya usimamzi wa Magari.Kituo cha Miito ya huduma kwa wateja,
 
Mkuu wazo zuri,Ila nafikiri utekelezaji wake unaweza badili approach

Mabus Tayari yapo Barabarani mengi tu ila mfumo wa usimamizi ndio changamoto.
Pili Gharama za Kumiliki Mabus zinachangamoto zake ila unaweza kuanzisha kama BUS Management Company ambapo wamiliki wa Mabasi wa sasa na Wapya wanaweza kuwa na Option ya Kuwakodishia mabus Yao.Mnachopaswa kuwekeza ni nini?

Mtandao Mzuri wa Vituo vya kupakia na kushusha Abiria,Mtaji hisa kwa ajili ya Gharama za uendeshaji,Vituo vya mafunzo maalum kwa ajili ya usimamzi wa Magari.Kituo cha Miito ya huduma kwa wateja,
Shukrani kwa wazo mkuu
 
Habari Wakuu,
Matumaini yangu mko njema na kwa wale wanaopitia heka heka na magumu Mungu abariki mihangaiko yenu iwe yenye kulipa fadhila la jasho lenu linalochuruzika kila kukicha.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye kiini cha uzi huu.

Kwa miaka kadhaa sasa baada ya anguko la iliyokuwa kampuni bora ya usafirishaji wa Abiria, Parcels na Mizigo ya kati na mikubwa ya Scandinavia Express, hakuja tokea kampuni yenye kutoa viwango vya huduma katika level waliyokuwa nayo.

Hii nikutokana na kuwa wafanyabiashara wengi wanaoingia katika tasnia hii kutokuweka kipaumbele katika utoaji wa huduma nikiwa na maana huduma za kabla ya kupanda basi (kukata tiketi, ukkabidhiji wa mizigo, booking system etc) na zile za baada ya abiria kupanda basi (kauli nzuri, chakula standard, mwendo mzuri wenye kuzingatia mashimo ama matuta usioumiza shingo wala mgongo)

Hivyo basi uzi huu ni special kabisa kwa wawekezaji wote watakaopenda kuwekeza kwenye kampuni tutakayoianzisha ambayo itaenda kuwa zaidi ya ilivyokuwa Scandinavia Express.

Nini tunapanga kuoffer kuweza kufikia ama kuzipita level za ilivyokuwa Scandinavia Express

1.Kutengeneza Private Stand zenye Standards bora kwa gharama nafuu

Hapa ikijumuisha design bora ya kuruhusu bus kuingia, kupark na kutoka kiurahisi.

Sehemu maalumu ya kupokea, kupangilia na kutumia mizigo ambapo tutaongezea na huduma za ziada kama custom packaging design za kampuni yetu ambapo itajumuisha printed sticker zinazoonyesha ni nani anatuma mzigo na nani ndiye mpokeaji....gharama hizi zitakuwa mficho kwenye gharama za utumaji mzigo.

Mfano Wake:
View attachment 2504999

2.Printed tickets
Tutatoa Tickets ambazo ziko printed instead ya zile za kuandikwa kwa mkono

3.Door to Door delivery
Baada ya mizigo kufika destination tutaweza kuwafanyia wateja wetu a door to door delivery kwa gharama za chini kuna project special ambayo kwa kuitumia tutaweza kuminimize cost kwenye ufanyaji huu wa delivery.

4.Standard Food na kwa bei affordable
Tutawezesha abiria kuweka booking ya chakula atakachohitaji through applikesheni ambayo bus host atakuwa nayo, gharama za chakula ni mficho kwenye nauli ya kusafiria.
Tutatengeneza simple resteurant ambayo ndiyo itakayokuwa inatengeneza chakula hicho kuhakikisha standards zimezingatiwa halikadhalika hatupotezi hela kwenda nje ya eco-system yetu.

5.Mafunzo kwa Madereva na Hostess
K
abla ya kampuni kuanza rasmi kusafirisha tutawapiga brush la nguvu hostess na madereva wetu, upande wa Madereva kuna special kozi kwa kushirikiana na Scania Tanzania wataweza kuipata juu ya namna bora ya uendeshaji wa Mabus yao etc

na hata baada ya kuanza rasmi kila siku kabla na baada ya safari watapitia kumbusho la mafunzo na msisitizo wa yapi yafanywe ama kutokufanywa kipindi chote cha safari hii yote ni kumaintain standards za huduma.

Haya ni machache kati ya mengi tutakayoweza kuyafanya kuhakikisha huduma zetu zinakuwa bora muda wote.


Mchanganuo wa Biashara kiufupi.
B
iashara ya Mabus si lelemama yahitaji usimamizi yakinifu wa kila siku ...

Nimebahatika kufanya mazungumz na kampuni 5 za watengenezaji wa Mabus,
1.Higer 2. Scania 3.Yutong 4. Asia Star 5. Volvo

Kwa kuzingatia huduma, upatikani wa vipuri, Guarantee ya uhakika gari kuwepo barabari kwa muda mrefu etc

Imeiweka mbele zaidi kampuni ya Scania kuwa chaguo letu bora zaidi

GHARAMA ZA UANZILISHWAJI WA PROJECT HII
1.Mabus 6

Ambapo kwa Scania wanatoa ofa ya mkopo kwa kulipia kianzio cha 25% cha bei ya bus huku mkikubaliana kipindi cha kufanya marejesho aidha siku,week,mwezi ama miezi etc

Bus moja ni Tsh. 710M
25% YA Bus ni Tsh. 177.5M
25% Kwa Mabus 6 ni Tsh. 1.065B

2. 3 (Three) Private Stands/Yard
Target yetu ni kuanza na route moja ya Dar - Dodoma
Hivyo tutakuwa na main two private stands + 1 stand itakayokuwepo Morogoro ikijumuisha na resteurant etc

Kila moja kuanzia gharama za kiwanja, matengenezo na vifaa tunakadiria 100M each hivyo kwa stand 3 itacost
Tsh. 300M

3.Total Cost
6 buses + Stands + Gharama mficho hadi kuanza kuingiza pato la mwanzo = Tsh 1.5B



KWA UZINGATIVU
K
wa watakaopenda kutoa maoni mawazo ama maswali uwanja huu ni wenu.

Uwekezaji wowote kuanzia Tsh. 500 000 unakaribishwa, karibu kwenye project itakayoenda kubadilisha ulimwengu wa usafirishaji Tanzania na East Africa

Mchanganuo huu ni kwa ufupi mno kwa yoyote atakaye hitaji kufanya uwekezaji basi ninaunda group WhatsApp
ambapo nitaweza kutoa ufafanuzi wa vipi faida utakavyoweza kuipata wewe muwekezaji na vipi usimamizi utakavyokuwa

Mshana Jr Bavaria Shimba ya Buyenze Kasie Herbalist Dr MziziMkavu Bujibuji Simba Nyamaume
Mawazo yako ni mazuri. Tena sana tu! Ila rangi yako ya mwili ndiyo itakuponza. Maana rangi nyeusi haiaminiki popote pale hapa Duniani. Tungekuwa ni Wachina, au Wazungu; muda si mrefu tungekuwa matajiri kupitia hili wazo lako.

Ingawa pia siungi mkono kwa route fupi na isiyo na misuko suko mingi ya Dar Dodoma; kutumia mabasi ghali kutoka kampuni ya Scania. Mchina tu (Yutong, Zhontong, Higer, Dragon nani sijui, nk) alikuwa anatosha kabisa kwa hiyo route..
 
Unaijua Mr Kuku, Vanilla International, Deci, Bravo Mills, Jatu?
Mkuu even kwa Marekani wameface utapeli mkubwa na failures kubwa kupitia Start-Up tokea zamani na hata sasa

Mfano
1.Theranos ya Mwanadada Elizabeth Holmes

2.FTX

3.Windows Phone toka Microsoft

4.Unaikumbuka Blackberry

5.Nikola, Electric Trucks

6.Worldcom

7.Quibi

8.Wirecard

9.WeWork Disaster

10.Enron

etc

Hatuwezi kuendelea ikiwa tunadhani kila project ama proposal inayokuja mbele yetu tukaitupa kwenye dustbin ya utapeli

Mara mia ukajaribu kuuliza ama kushauri tuweke kipengele gani ambacho kitawalinda wawekezaji kuliko kuishia kukosoa ukabaki hapo wadhani huo ndo uGreat Thinker??
 
Ni gari nzuri mno kimuoneka like Yutong,Higer etc,

Life Span ya gari la kichina maximum ni 3 years wanakupa guarantee ya matengenezo ya mwaka mmoja

Model ya business ya mabus yoyote ile inaweza kulipa gharama za manunuzi ya Bus ndani ya Miaka 3 nje na interest

Ikiwa na maana Gari litakufa kabla hujamaliza kulilipia interest, faida utaipatia wapi??

kwa kampuni zilizokuwa like Shabiby etc anatumia gari mwaka mmoja guarantee ya matengenezo ikiiisha naye analiuza linaenda kumfia mwingine

UPANDE WA SCANIA
Bei iko juu kiasi hatukatai
Life span ya Bus ni matunzo yako ukilipa matunzo bora linaweza kukaa barabarani zaidi ya Miaka 10
Service Guarantee wanakupa ya Miaka 3
Hivyo unaweza malizia mkopo wa bus na ukawa na muda mrefu wa kutafuta faida yako ya kukutosha
Asante kwa ufafanuzi mzuri.

Wacha nitarudi na info kidogo na maswali zaidi baada ya muda
 
Mimi nadhani kama mna hiyo 300m undeni kampuni ila watu waje na mabasi yao wawekeze. Nyie muwe wasimamizi wa shughuli zote za kampuni. Hao watakaoweka mabasi yao wawe wanapata tu mgawo. Kule Kenya kuna hizi gari ziko chini ya kampuni za namna hiyo.. kwa mfano NAEKANA SACCO ya Namanga - Nairobi. Hawa wamiliki wa mabasi machache wajisalimishe kwenu. Wawe shareholders. Kampuni yenu itakuwa imara maana kuna shareholder Mshana ambaye ni mchawi mwandamizi.
 
ungeomba kibali latra, bus zako tatu zifanye route ya dar to moshi na arusha (hakuna kulala), asubuhi zinageuka kurudi dar na abiria kama kawaida. hii route ina hela kinyama
 
Back
Top Bottom