Usipoteze siku yako kwa kuwekeza kwenye huzuni.Siku unayoanza kwa matatizo, mambo yako ovyo, huna kitu ndiyo siku unapaswa kuwa na furaha maishani mwako; kwasababu, pamoja na changamoto hizo, bado upo hai.Kumbuka, ukiishiwa kodi hujaishiwa dunia, ukiishiwa hela, hujaishiwa pumzi, ukiachwa na umpendaye hujaachwa na Moyo, macho, akili na kila kitu kilichokusaidia kumpata; hata dunia mlipokutania bado haijakuacha_
*Wewe jiamini, jisemee "mimi ni mshindi" pamoja na changamoto hizo bado unaye Roho Mtakatifu wa Mungu afanyaye kazi ndani mwako. Usijidharau.
[emoji871]