Wema aachiwa, akamatwa tena, azua kizaa zaa mahakamani

Wema aachiwa, akamatwa tena, azua kizaa zaa mahakamani

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amezua kizaa zaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akigoma kukamatwa na polisi baada ya mahakama hiyo kumwachia huru na kisha kumkamata tena na kumuweka mahabusu ya mahakama hiyo.

Wakati askari wakimkamata kwa nguvu, Wema aligoma kukamatwa hali iliyosababisha mvutano kwa muda kati askari na mawakili wake, Albert Msando na Reuben Simwanza.

Hata hivyo, askari hao walifanikiwa kumkamata msanii huyo aliyetoka Mahabusu ya Gereza la Segerea Juni 24, mwaka huu ambapo alifika mahakamani asubuhi kwa ajili ya kusikiliza kesi yake inayoendelea mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai hana shahidi baada ya shahidi aliyemuandaa, Koplo Safi kudai ni mgonjwa.

Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa Wema, Albert Msando kwa madai kwamba haina mashiko, mahakama ilishatoa ahirisho la mwisho hivyo hawawezi kuahirisha tena.

“Mheshimiwa shauri lipo zaidi ya siku 60, upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi, tunaomba chini ya kifungu namba 225(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 mshtakiwa aachiwe huru,” alidai.

Wakili Mwenda alipinga akidai sheria ya siku 60 inatumika pale tu ambapo upelelezi haujakamilika hivyo aliomba kesi iahirishwe.

Hakimu Kasonde alisema anakubaliana na maombi ya upande wa utetezi, sheria hiyo inatumika wakati wowote hivyo mahakama inamuachia huru mshtakiwa.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.
 
Huu ni wakati wake wa kujifunza, mamake hakumfunza sasa dunia imechukua nafasi kumfunza kama wasemavyo wahenga "asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu"
Pole Wema, mtoto mrembo ambaye hajafaidi urembo wake zaidi ya kula bakora
 
Sometime tuwaangalie tu hawa kama bongo movies au 'wapinzani' lakini tusipojifunza kuziheshimu taasisi zetu na maamuzi yake siku moja badala ya kufanya reference ya scenario za case tutakuwa kila mmoja anaamua lake na hapo ndipo tutajua kuwa polisi wasiozidi laki moja hawana uwezo wa kuwadhibiti watu milioni 55!
 
Hizi mahakama bana zinapoteza sana muda na kutumia rasilimali fedha vibaya, wanahitaji shahidi wa nini wakati video ziko mitandaoni? Huyo askari anaesubiriwa kutoa ushahidi ndio alikuwa anarekodi kwani? wema alirekodi mwenyewe na kuutambulisha uma kuwa huyo ndie future husband wake. Wamuhukumu au wamuachie huru sio kesi za kila siku .
 
Ila huyu mtoto mzuri jamani ngoja nitafute hela
 
Back
Top Bottom