Wema acha roho mbaya

Wema acha roho mbaya

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
9,552
Reaction score
24,166
Katika gazeti la leo la Mwanaspoti 29/05 huyu Wema ametoa kauli za ajabu kabisa kuhusu Kajala.

Anasema hatokaa kumsamehe katika maisha yake yote na hata akifa Kajala asisogelee kaburi lake.

Jamani sasa huyu mama roho mbaya anapoelekea anahitaji kusaidiwa na wataalam wa masuala ya jamii/mahusiano.

Unakuwaje na hatred mbaya namna hii kwa binadamu mwenzako...!!?? Ugomvi wenyewe ni wa kuporana mwanaume ambaye ni MUME wa mtu.

Msaidini huyu Wema jamani na nafikiri sasa asiitwe tena hilo jina lake la Wema awe anaitwa CHUKI.
 
Bado ana machungu ukichangia na million kumi na Tatu alizotoa. Ila Kajala naye ni mshe... Mno wa tabia hata kama ingekua ni mume wa mtu Ku date naye ni vibaya mno na inaumiza. Kajala acha unafiki wewe ni bigwa wa kuchukua waume za watu. Wema atasahau tu na kusamehe jinsi mda unavokwenda kusalitiwa na shostito kunauma. Wema msamehe huyu Kajala.
 
Katika gazeti la leo la Mwanaspoti 29/05 huyu Wema ametoa kauli za ajabu kabisa kuhusu Kajala.
Anasema hatokaa kumsamehe katika maisha yake yote na hata akifa Kajala asisogelee kaburi lake.
Jamani sasa huyu mama roho mbaya anapoelekea anahitaji kusaidiwa na wataalam wa masuala ya jamii/mahusiano.
Unakuwaje na hatred mbaya namna hii kwa binadamu mwenzako...!!?? Ugomvi wenyewe ni wa kuporana mwanaume ambaye ni MUME wa mtu.
Msaidini huyu Wema jamani na nafikiri sasa asiitwe tena hilo jina lake la Wema awe anaitwa CHUKI.

wanapenda kutoa kauli nzito mwisho wa siku zitakuja kuwakosti, kama Kajala katambua makosa yake na kakiri kwanini asisamehewe??
 
Sasa atamsamehe mtu ambae hajamwomba msamaha?
Maana mimi nimeona kajala ana sifia msaada wa wema na kumshukuru ila sijaona kama ameomba msamaha.
Ajaribu kuomba msamaha sasa
 
Chanzo nini?,au muhogo wa jang'ombe?,ha ha ha wanagombea ndizi wakati mgamba si wao?...
 
Mie hata sielewi hatomsamehe kwa lipi?

Kumlipia atoke jela au kusema alitoka na mume wa mtu ambaye alitoka nae na kutemwa?

Hayo aliyasema kwa kusisitiza kwenye kipindi chake ni ya mume wa mtu CK alimtaja kama vile ni single man na maumivu ya kuchukua mali zake alizompaga (kideo kipo youtube).
 
Huyu Wema MICHIRIZI hizi team zake za Instagram zinamfanya agombane na kila mtu huyo CK wanaemgombania alikuwa ni mume wa mtu maombi na Sara za mwenye mume ndio laana zinawapata wanadhalilishana mitandaoni na ktk magazeti
 
wanapenda kutoa kauli nzito mwisho wa siku zitakuja kuwakosti, kama Kajala katambua makosa yake na kakiri kwanini asisamehewe??

Hajakiri makosa wala hajaomba msamaha alichofanya aliandika kwenye page yake insta kuapreciate alichofanyiwa na wema
 
Alietoa post kaegemea upande mmoja. Team kajala nn???. Uamuzi wa kusamehe au kutokusamehe ni wa wema. Aliyekosea pia kuomba msamaha au kutokuomba ni uamuzi wake. Bse ktk insta page ya kajala sijaona sehemu kajala naomba msamaha zaidi ya kushukuru kwa kusaidiwa na wema na petitwakuache na kusema iko siku watakua km zamani basi. Mi nadhani haijalishi ni kosa dogo au kubwa kiasi gani but km umekosea sema nimekosea. Na ambae hatakusamehe unamwachia Mungu sasa hapo.
 
Nadhani inatakiwa apewe muda maana huwezi kusema umesamehe ilhali hujasahau, muda utafika tu maumivu yataisha na atasahau ikumbukwe wema pia ni binadamu pia, cha muhimu ni kumwombea na kumshauri pia
 
alietoa post kaegemea upande mmoja. Team kajala nn???. Uamuzi wa kusamehe au kutokusamehe ni wa wema. Aliyekosea pia kuomba msamaha au kutokuomba ni uamuzi wake. Bse ktk insta page ya kajala sijaona sehemu kajala naomba msamaha zaidi ya kushukuru kwa kusaidiwa na wema na petitwakuache na kusema iko siku watakua km zamani basi. Mi nadhani haijalishi ni kosa dogo au kubwa kiasi gani but km umekosea sema nimekosea. Na ambae hatakusamehe unamwachia mungu sasa hapo.

nimekupenda bure mkuu
 
Itabidi niwalete hapa jf ili kajala atueleze alimkosea nini madame hadi hataki hata kusikia jina lake.
 
Huyu Wema MICHIRIZI hizi team zake za Instagram zinamfanya agombane na kila mtu huyo CK wanaemgombania alikuwa ni mume wa mtu maombi na Sara za mwenye mume ndio laana zinawapata wanadhalilishana mitandaoni na ktk magazeti

CK alikuwa bwana wako? team za simba na yanga hujaziona umeona ya wema tu? mwenye mume unamjua au unaropoka tu? kama hujui bora ukae kimya si lazima kukomenti
 
Back
Top Bottom