Wema ajuta kuweka kope za bandia

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
BEAUTIFUL-Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa anajuta kutumia kope za bandia kwa muda mrefu kwani zimeharibu kope zake za asili’.Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema alisema awali alikuwa hawezi kutoka kwenda kokote bila kuweka kope hizo na hata asipozibandika anajisikia vibaya lakini baada ya kumharibia muonekano wake wa asili, hataki hata kusikia.“Jamani hakuna kitu ambacho nimekichukia kwa hivi sasa kama kope za bandia sina tena ushawishi nazo kabisa zimeharibu macho yangu, situmii tena,” alisema Wema.
 
Attachments

  • 1422914935096.jpg
    54.1 KB · Views: 4,188
Huyu sidhani kama kuna sehemu kasalimika manake!

Kila kitu fake isipokuwa hicho kipilipili kilichodunda kemikali za mzungu!

NB:I heard that mbele mwenyeji na nyuma mzoefu!
 
Hata akijamba Wema nayo habari. Haya Airtel wamuongezee mihelaaaa.
 
Huyu sidhani kama kuna sehemu kasalimika manake!

Kila kitu fake isipokuwa hicho kipilipili kilichodunda kemikali za mzungu!

NB:I heard that mbele mwenyeji na nyuma mzoefu!

Hahahahaaa ila wema ana kipilipili mbuzi aisee.

Mnhhh I heard too from chickmaget
 
Last edited by a moderator:
Ukute mtu kabandika kope halafu hajui kubandika, zinaonekana kabisa kope za bandia. Utataka kutapika.
 
Ukute mtu kabandika kope halafu hajui kubandika, zinaonekana kabisa kope za bandia. Utataka kutapika.

Jumamosi nikiwa Target kwenye check-out register mdada cashier alikuwa nazo hizo halafu zinameta meta.

Nikamtizama nikaishia kumuonea huruma. Lakini uzuri mtu kipenda roho. Kama yeye karidhika wala si shida.
 
Halafu hapo ujue kuna mtu analazimishwa kusema "baby, that looks so pretty on you".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…