Wema akimbilia zanzibar kujificha baada ya kumjeruhi meneja wa hoteli, polisi wavamia nyumbani kwake

Wema akimbilia zanzibar kujificha baada ya kumjeruhi meneja wa hoteli, polisi wavamia nyumbani kwake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
WEMA AKIMBILIA ZANZIBAR KUJIFICHA BAADA YA KUMJERUHI MENEJA WA HOTELI, POLISI WAVAMIA NYUMBANI KWAKE NA KUFANYA UPEKUZI MKALI...!!






POLISI wapatao sita Jumamosi iliyopita walivamia nyumbani kwa staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu maeneo ya Kijitonyama kwa lengo la kumkamata kufuatia kesi iliyofunguliwa katika Kituo cha Polisi Kawe jijini Dar.

Awali taarifa zilidai kuwa, tuhuma zinazomkabili staa huyo asiyekaukiwa na matukio ni za kumtukana na kumpiga vibao Godluck Kuyumbu ambaye ni meneja wa hoteli moja maarufu jijini Dar.

Baada ya kesi hiyo yenye jalada KW/RB5988/2013 SHAMBULIO kufunguliwa kituoni hapo Julai 6, mwaka huu mishale ya saa 5 asubuhi, maafande hao wakiwemo wa kike wawili wakiwa wamevaa kiraia walifika mtaa anaoishi staa huyo na kuufunga kabla ya kwenda kugonga katika geti la nyumba yake.
Mara baada ya kugonga geti hilo, alitoka mwanaume aliyefahamika kwa jina la Petman, alipoulizwa kuhusu Wema, alijiumauma huku kijasho kikimtoka kabla ya kutoa jibu la kwamba hakuwepo.
Majibu hayo hayakuwaridhisha polisi hao ambapo walilazimika kuzuia kila gari lililokuwa linat

oka getini hapo wakiamini huenda Wema angetolewa kiujanjaujanja.

Hata hivyo, hawakufanikiwa kumuona ndipo walipolazimika kumuita mjumbe wa eneo hilo na kuomba ruhusa ya kuingia ndani kufanya upekuzi lakini hawakumtia mikononi na taarifa zikawa mwanadada huyo yuko Zanzibar.

Maafande hao waliomba namba ya simu ya Wema na walipompigia alisema yuko Zanzibar, kesi hiyo anaijua na atakaporejea atajisalimisha mwenyewe polisi.


SOURCE: GPL

WEMA AKIMBILIA ZANZIBAR KUJIFICHA BAADA YA KUMJERUHI MENEJA WA HOTELI, POLISI WAVAMIA NYUMBANI KWAKE NA KUFANYA UPEKUZI MKALI...!! - GUMZO LA JIJI
 
Inashangaza polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake wakati mwenyewe hayupo! Kosa la shambulio na upekuzi wapi na wapi! It doesn't make sense to me.
 
Inamaana alila hotelini?Na huku ana kwake?Duu wakubwa wanafaidi
 
Anapigwa vibao na demu halafu polisi wanamtafuta demu badala ya kumsweka ndani huyo poyoyo? Hawa polisi vipi?
 
Aliyepigwa vibao tena ni ndugu yangu upande wa mama yangu mzazi anaitwa goodluck Kayumbu labda jina liwe linafanana! Ni bonge la bouncer na karateka haiwezekani kupigwa vibao labda katukanwa! Natuma picha yake. ImageUploadedByJamiiForums1373516782.665141.jpg
 
Najaribu kutafuta namba yake ya simu nipate uhakika! Haiwezekani kupigwa vibao na wema.
 
Hapa ndo zanzibar na kipara chake eti kaamua kunyoa kwa kujiandaa na maisha ya selo, selo akuna wigi mwanzo mwenga
mchibuyu.
kipara.jpg
 
Inashangaza polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake wakati mwenyewe hayupo! Kosa la shambulio na upekuzi wapi na wapi! It doesn't make sense to me.

walipitia kwa mjumbe wa nyumba kumi ....

Yani mwanaume mzima ananyukwa vibao na mwanamke tena mlaini, halafu anaenda kushtaki polisi,!

nchi inaongozwa na sheria ....

Anapigwa vibao na demu halafu polisi wanamtafuta demu badala ya kumsweka ndani huyo poyoyo? Hawa polisi vipi?

nchi inaongozwa na sheria , hawa wanawake maraafu hawakawii kukugeuzia kibao kama ile kesi ya mange kimambi na yule lawyer hadi akadai alienda kufanyiwa surgery

Huyo kayumbu lazima atakuwa punga tu yani wema anakulamba vibao?

piga wewe mwanamke wa watu alafu aende polisi ndio utajua ni punga au alikuwa mwerevu
 
Yani mwanaume mzima ananyukwa vibao na mwanamke tena mlaini, halafu anaenda kushtaki polisi,!

Mkubwa jamaa angereact zaid nadhan ndo mambo yangekua mabaya kwake mana angemvimbsha sura ila sasa hivi dada wa watu lazma alipe faini ya ukwel
 
Aliyepigwa vibao tena ni ndugu yangu upande wa mama yangu mzazi anaitwa goodluck Kayumbu labda jina liwe linafanana! Ni bonge la bouncer na karateka haiwezekani kupigwa vibao labda katukanwa! Natuma picha yake.View attachment 101635

ikiwa ni huyu, basi atakuwa ni chakla....
 
He he he he he, ha ha ha ha haha, hihihihihihihihihihi
Ukiangalia sana muvi unawehuka
 
Anakimbia nini sasa wakati aliwaambia waende kushtaki kokote hawezi kufanywa kitu,angekaa kama mwanamke kweli
 
kesi ya kipumbavu hivi, inasimamiwa na Pilisi sita? kweli Polisi wa tz ni wapumbavu!!
 
Aliyepigwa vibao tena ni ndugu yangu upande wa mama yangu mzazi anaitwa goodluck Kayumbu labda jina liwe linafanana! Ni bonge la bouncer na karateka haiwezekani kupigwa vibao labda katukanwa! Natuma picha yake.View attachment 101635

Inawezakana jamaa hakutaka kujichukulia sheria mkononi kwa naye kumpiga Wema...fikiria angempiga wema, unadhani huyu baunsa angekuwa wapi leo kama sio selo...nadhani baunsa anajitambua hana nguvu ya kipesa wala influence so akaona kitu sahihi cha kufanya ni kutorudisha makofi kwa wema na kwenda kushtaki polisi.
 
Anayemlala lazma magamba, she acts however she wants and get away with it (magamba's day to day routine)
 
Back
Top Bottom