Wema anafanyiwa upasuaji India

Wema anafanyiwa upasuaji India

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema itatoa amri endapo msanii wa filamu nchini Wema Sepetu atashindwa kuwasilisha uthibitisho wa nyaraka za matibabu yake.

Hatua hiyo imetokana na mshtakiwa huyo kutofika mahakamani hapo kwa mara mbili mfululizo kwa madai kuwa ni mgonjwa na yupo nchini India kwa ajili ya matibabu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu na mahakama imesema endapo Wema hataleta vielelezo hivyo, mahakama itatoa amri.

Amri hiyo imetolewa leo, Mei 29, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya mdhamini wa Wema, Mariam Sepetu ambaye ni mama yake mzazi kuwasilisha mahakamani tiketi ya ndege badala ya nyaraka za matibabu.

Wakili wa Serikali Costatine Kalula, ameieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa hao kujitetea, lakini mshtakiwa wa kwanza Wema hakuwepo Mahakamani.

Baada ya Kakula kueleza hayo mahakamani, Mariam Sepetu alisimama na kuieleza mahakama kuwa, Wema ni mgonjwa tangu Mei 14, mwaka huu na sasa yupo India kwa ajili ya matibabu.

“Mheshimiwa hakimu, Wema yupo nchini India kwa ajili ya matibabu, ameenda kufanyiwa upasuaji kwa sababu tangu siku ile. (Mei 14, 2018) hali yake si nzuri na hapa tuna fomu ya matibabu, tunaomba kuzitoa mahakamani," amedai mama yake.

Baada ya kuwasilisha fomu hizo za matibabu na kupitiwa na Wakili wa Serikali zilibainika kuwa si fomu za matibabu badala yake zilikuwa nyaraka za tiketi ya ndege.

Chanzo: Mwananchi
 
Pamoja na drama zako Wema, still nakutakia upone katika madhaifu yalikupelekea kwenda India!

Wewe ni Best kabisa. Achana na maneno ya watu. Yaishi maisha yako utakavyo!
 
Wema alikuwa kwenye miss morogoro nimemuona" live" kwa macho yangu huko india amekwenda lini? bongo hii drama sana
 
Hii habari ya mwaka gani kwanza mwandishi unazungumzia habari za Mei na Juni sisi tuko Julai?
 
huko india atakuwa kaenda kufanyiwa upasuaji wa kupunguza miaka

india inawezekana
 
Hii habari ya zaman,leo kaenda mahakaman hukumu kama sio ijumaa basi wiki ijayo
 
Hii mahakama nayo imekuwa ya kibabaishaji na inanitia shaka kuwa na mahakimu incompetent. Kama nakumbuka Wema alishakiri kosa. Sasa kwa nini wasitoe hukumu kazi kurefusha shauri hili ili waendelee kupata promo! Useless kabisa.
 
Akatwe utumbo uongezewe kwenye ubongo apate akili
 
Back
Top Bottom