Wema aonyesha jeuri ya pesa nchini China

Wema aonyesha jeuri ya pesa nchini China

Jamani wekeni channel 5 Daimond anacheza, shemeji huyoooo hhhhhaa mpenzi yupo China
Pesa nzuri jamani Dai kapendezaaa tusemage ukweli tu Kim nana
 
Last edited by a moderator:
WAKATI bebi wake, Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya kuzomewa
na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita , Wema Sepetu ‘ Madam’ anaponda raha ya maisha nchini China.

Chanzo makini kilicho ‘ kloz ’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini , kimesema Wema alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache kabla ya Tamasha la
Fiesta, akiwa ameandamana na wanaume wawili, ambao ni meneja wake , Martin Kadinda na Petit Man , wote wakiwa wamekaa daraja la kwanza la dege hilo.

Chanzo hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo zilibebwa na Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la Guangzhou nchini humo ,Wema na wanaume hao wawili walichukua
vyumba katika Hoteli ya Holiday Inn ,
inayotajwa kuwa moja ya hoteli ghali zaidi huko China.
“Yaani Wema jamani ana mambo,
inavyoonekana lile rhumba la wakati ule ameshalisahau, amesahau kabisa kama alishafulia, sasa Mungu kamjaalia kapata pesa anavyoitapanya ovyo mpaka roho
inauma .

Wewe fikiria mtu amekwenda
kuchukua vifaa vya biashara , unakwenda na
hao wanaume wa kazi gani kama siyo kupoteza fedha tu , ” kilisema chanzo hicho.

Inadaiwa kwamba kilichompeleka Wema katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi kuliko yoyote duniani , ni ununuzi wa vipodozi , kwani ana mpango wa kufungua duka kubwa
katika eneo ambalo halijatajwa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kufika huko, chanzo kinasema kuwa watu hao watatu wamekuwa wakiishi maisha ya starehe , wakila bata katika klabu
mbalimbali za usiku , ambako
wanajichanganya na watanzania wengine kuponda raha.

“Kwa matanuzi anayofanya kule , hata hiyo biashara aliyoifuata haina maana , angekuwa mtu mwenye nia ya biashara kweli , angetafuta tu hoteli ya kawaida ili kubana
matumizi aweze kuja na mzigo mkubwa, sasa wewe mwenyewe fikiria, hii wiki ya pili sasa ,
tena na wanaume wawili wanakutegemea , hizo pesa si kuzitapanya tu jamani , ” kilisema chanzo hicho kikionyesha kutofurahishwa na maisha ya staa huyo.

Hapa naona hakuna chochote cha kumtuhumu wema.
Wewe kama umeshindwa kushughulikia mambo yako mwenyewe haya ya wema achana.nayo kwa sababu moja kati ya falsafa za kimaisha zinasema ukitaka ushindwe kusonga mbele fuatilia ya wengine.
 
Hawa waandishi nao wakati mwingine hata siwaelewi. Kusafiri VIP na kufikia hotel ya 5 Stars ndo kumefanywa habari?!
Haya bwana, kila mtu mtu na kazi yake.
Ova
 
tatizo la hawa wasanii wetu wanahisi muda wote wanaigiza,hatumuombei mabaya lakini siku wema anapata akili ya maisha ndio na hizo pesa zinakata,wakati huo hatamuona ata mmoja wakumuhonga tena km kweli anahongwa.
 
Ni shidaaaaaaaaaaaaaa

nimeona mahali walikwenda mwangalia zebra mwenzao macau.nadhani wametumwa wao ndo vijakazi.na wamekwenda sasa kwasababu upepo imepoa serikali imehamishia nguvu kwa ebola.ila wakirudi watatumwa tena kumtoa chidi.ila za mwizi 40 iko siku Titajua.watu wanaangamia wao wanafurahi
 
nimeona mahali walikwenda mwangalia zebra mwenzao macau.nadhani wametumwa wao ndo vijakazi.na wamekwenda sasa kwasababu upepo imepoa serikali imehamishia nguvu kwa ebola.ila wakirudi watatumwa tena kumtoa chidi.ila za mwizi 40 iko siku Titajua.watu wanaangamia wao wanafurahi

Jack atafurahiajee ila ni vizuri kama wameenda kumsalimia nae ajisikie vizurii jamanii
Mi natamani Wema akamatwe na madawa ya kulevyaa
 
Umbea tu kuandika mnajua vipicha vya insta wanavopost insta mbona vitawatoa roho!! Akipiga picha pembeni ya ikulu ya china mtakuja na thread mpya wema agawa papuch kwa rais wa naniliu! Hahahahaha chezea smarthphone na washamba!! Utalala mdomo waziiii
 
Umbea tu kuandika mnajua vipicha vya insta wanavopost insta mbona vitawatoa roho!! Akipiga picha pembeni ya ikulu ya china mtakuja na thread mpya wema agawa papuch kwa rais wa naniliu! Hahahahaha chezea smarthphone na washamba!! Utalala mdomo waziiii

Sawa wema wamekusikia
 
Back
Top Bottom