Bado nakaa natafakari. Kwa nini mtu uamue kutunga uongo ili kumchafua mwingine. Kwa nini Wa-tz tufikie hapo. Hatuna jambo lingine la kufanya la kulisaidia taifa letu lisonge mbele?
Nasema hivi. Hata hii audio clip inayosambaa sasa ikitaka kutuaminisha ile iliyotangulia ni ya kweli nayo ni manufactured. Imetengenezwa. Narudia tena, kwa utaalam wangu, hii audio ya pili imetengenezwa, na in short, ina vipisi si chini ya vitatu vilivyoungwa. Kipisi cha kwanza kinaisha kabla ya kutaja neno mwenyekiti. Kipisi cha pili ni neno mwenyekiti na kipisi cha tatu ni pale anaposema ahh bwana Steve me nimechoka. Hizo ni three different pieces za wema halisi zilizoungwa. Nataka kuamini alizizungumza huko nyuma kwenye matukio mengine na sasa zinatumika kuhalalisha uovu. That is my believe. Ukisikiliza kwa makini utaelewa. I stand to be corrected though.