Ryan Holiday
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 3,499
- 5,956
Hello, JF Members,
Kama wewe ni shabiki mkubwa na number one die hard fan wa Hilary Swank na Alan Ritchson basi hii movie ya Ordinary Angels (Malaika wa Kawaida) sio ya kukosa.
Ordinary Angels, 2024 ni filamu yenye mguso wa kihisia, inayoelezea maisha ya Sharon (Hilary Swank), mwanamke jasiri aliyepitia changamoto nyingi maishani mwake lakini anaamua kusaidia familia yenye matatizo makubwa. Hili ni tukio la kweli kabisa, na filamu hii ikipokea alama ya juu kabisa ya A-plus ( A+) katika CinemaScore, huku ikisifika kwa uigizaji wake wa hali ya juu pamoja na hisia za kweli zilizomo ndani ya filamu hii.
Kwa yale machache, Sharon anakutana na Ed Schmitt (Alan Ritchson), baba mgane anayepambana kulea binti yake mgonjwa. Licha ya hali yake, Sharon anafanya kila awezalo kuhakikisha binti huyo anapata matibabu anayohitaji.
Kwa kumalizia, kupitia hii movie, mimi kama shabiki wa Ordinary Angels nimejifunza vitu vingi sana katika haya maisha tunayoishi kila siku hapa Duniani. Imenikumbusha kuwa wema hauhitaji utajiri, bali moyo wa kusaidia, mshikamano na matumaini, vinaweza kuleta miujiza katika nyakati ngumu zozote.
Kila mmoja wetu anaweza kuwa 'malaika wa kawaida' (Ordinary Angel) kwa mwingine.
You can create miracles even in the darkest times.
Peace be upon you.