Wema,kajala watibuana

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Ule ushoga wa mastaa wa kike bongo,wema sepetu na kajala masanja umefikia pabaya kisa kikidaiwa ni maneno ya wapambe wa wema.hivi karibuni wema alimlalamikia wazi wazi shosti wake huyo kuwa anamsema vibaya kwa watu,pia inasemekana kipindi cha nyuma kajala alipata dili la kwenda kucheza filamu china lakini ikadaiwa kuwa wema alichomoa hivyo muigizaji huyo hakwenda.chanzo kingine ni zile millioni kumi na tatu alizomtolea kajala inasemekana zinamkosesha raha kajala yaani amekuwa mtumwa wa wema,atakachosema wema basi kajala anafauata hata kama yeye hakupenda kufanya hivyo kisa kikiwa ni zile million kumi na tatu alizomtolea kajala.hivi sasa kila mtu kaamua kufanya yake
 
Tatizo warumi huaminiki stor zako zakidau zaidi,japo unaakaunt jing tukana upigwe ban ila ujumbe umefika kwako
 
Tatizo warumi huaminiki stor zako zakidau zaidi,japo unaakaunt jing tukana upigwe ban ila ujumbe umefika kwako

Udaku maana yake umbea si ndio??,na mbea siku zote hasemi kitu cha uongo
 
kama umeitoa global publishers si habari ya kuaminika.
 

source tafadhali,manake sitaki kusikia chanzo ni mtu wa karibu wa wawili hao.
 
kwaiyo warum unauwakika unakisema?mbona muongo sana siku utakuwa serious watu watakupotezea.hawana ugomv hao trust this.
 
Hii kitu nahisi ni kweli coz walikua wanatabia wanapiga pic pamoja na kuongozana na wanazipost instagram...na ht km wema au kajala akipiga pic lazma atamtag au kucomment kwa mwenzie sasa hivi ni mchuno..kajala kaenda mwanza huko aliko anaonekana hana raha na anapost vijembe..na wema pia anapost vijembe....ila me navyoona wema atakua na matatizo...yn hakai na marafiki..kwanza hiyo milion 13 hakumuomba amtolee kajipendekeza mwenywe
 
Haya mengine wataelewana huwa wanagombana na kupatana
 
Yofali jamani kumsaidia mtu si kujipendekeza sema alifanya vema sema ndo tenda wema uende zako ukumkuta mtu na ukurutu ukamfumdisha kuoga badae akajifanya kujua we mwachie mungu kwani atarudi kwenye ukurutu wake kama zamani ndo asili yake wema alitenda wema basi aendelee na shughuli zake kimya huongea hizo pesa atazipata zingine
 
Poa tuu kwani ni vipi?

"To know the enemy is half the victory"
 
Tatizo warumi huaminiki stor zako zakidau zaidi,japo unaakaunt jing tukana upigwe ban ila ujumbe umefika kwako

Mimi nipo kwenye mtandao wa instagram,pia uwa nachek updates za hao mastaa,najua whats going on,tofauti na wewe kila siku jamii forum tu,pia uwa natembelea blogs za mastaa mbalimbali
 
[h=3]WEMA, KAJALA WATIBUANA[/h]Posted by GLOBAL on June 21, 2013 at 8:30am14 Comments 0 Likes
Na Musa Mateja


KIMENUKA! Utabiri wa wengi kuwa ushosti wa waigizaji masistaduu wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja kutumbukia nyongo unadaiwa kutimia na sasa wametibuana, Ijumaa limenyetishiwa.

Wema katika pozi na Kajala.
Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu (jina linahifadhiwa), mwanzoni baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya Sh. milioni 13 na kumnusuru kutokwenda Segerea a.k.a Segedansi, wawili hao walikuwa marafiki kama pete na kidole.
SIKU KAMA HIZI

“Walishinda wote, walilala wote, walikwenda klabu wote yaani Kajala alikuwa anamnyenyekea ‘madam’ Wema kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7…
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/wema-kajala-watibuana
Na Musa Mateja

KIMENUKA! Utabiri wa wengi kuwa ushosti wa waigizaji masistaduu wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja kutumbukia nyongo unadaiwa kutimia na sasa wametibuana, Ijumaa limenyetishiwa.

Wema katika pozi na Kajala.
Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu (jina linahifadhiwa), mwanzoni baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya Sh. milioni 13 na kumnusuru kutokwenda Segerea a.k.a Segedansi, wawili hao walikuwa marafiki kama pete na kidole.
SIKU KAMA HIZI
“Walishinda wote, walilala wote, walikwenda klabu wote yaani Kajala alikuwa anamnyenyekea ‘madam’ Wema kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Kuna wakati hapa katikati Kajala alikuwa kama katibu muhtasi wa madam, si unajua lazima atumikie fedha za watu?
“Kabla hajaenda Mwanza kwa ajili ya mapumziko kwa bibi zake, nilimsikia Kajala akilalama kuwa madam aliamka siku moja akawa amemchunia, unaambiwa hata salamu ikawa hakuna.
Wema akimlisha keki Kajala wakati wa sherehe ya kumkaribisha uraiani.
TATIZO NI WAPAMBE
“Hapo ndiyo maneno ya pembeni yakaanza kwa sababu mbali na Kajala, Wema pia ana wapambe wengine na mbali na Wema, Kajala naye ana kampani. Kwa hiyo sosi ya manenomaneno ni hizo kampani zao.
“Ipo siku kabisa Wema alimlalamikia Kajala hadharani kuwa amekuwa akimsema vibaya kwa watu.
“Yale maneno yalimuuma sana Kajala, ikabidi arudi nyumbani kwao lakini akawa anaogopa kumwambia mama yake kuwa ametibuana na Wema hadi alipotimkia Mwanza.
KUMBE ALIMKOSESHA DILI?
“Lakini kabla ya hii ishu ya kulaumiana, kipindi cha nyuma kidogo Kajala alipata dili la kwenda kurekodi filamu nchini China na mastaa wengine lakini ikadaiwa kuwa Wema alichomoa hivyo mwigizaji huyo hakwenda pamoja na kwamba alishapewa baraka zote na baba yake.
“Unaambiwa alikuwa amekamilisha taratibu zote za kwenda China, hadi tiketi alikuwa ameshakata lakini suala hilo lilipotua kwa Wema, ilidaiwa kuwa alikataa kumruhusu.
TATIZO MILIONI 13?
“Mimi nakwambia zile milioni 13 zinamkosesha raha Kajala hadi unamuona kabisa kwamba ana stress (msongo wa mawazo).
“Wewe fikiria, kazi inayomwingizia mkwanja ni filamu, sasa unaambiwa inadaiwa kuwa madam hataki acheze filamu za watu wengine, sasa ataishije jamani?
SASA NI KUNUNIANA KWA KWENDA MBELE
“Mimi nakwambia ndiyo maana ameamua kwenda kupumzika Mwanza baada ya kuwa wananuniana kwa kwenda mbele.”
Baada ya kupata habari hizo, Ijumaa lilimtafuta Wema kwa njia ya kilongalonga chake cha kiganjani ili kupata undani wa sakata hilo lakini hakupatikana hewani.
NYUMBANI KWA WEMA
Baadaye mwanahabari wetu alisaga lami hadi kwa staa huyo Kijitonyama, Dar, alipogonga geti alitoka mlinzi aliyedai kuwa ‘malkia’ alikuwa ndani amelala na hakuhitaji usumbufu pamoja na kwamba ilikuwa saa 6:30 mchana.
MENEJA WAKE ANASEMAJE?
Hata hivyo, Ijumaa lilibisha hodi ofisini kwa Wema, Mwananyamala-Komakoma ili kuzungumza na meneja wake, Martin Kadinda ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli Kajala yupo Mwanza, aliomba ruhusa ya kwenda kupumzika tukampa. Hayo mengine ya kutibuana na madam siwezi kuyasemea kwa sababu yapo nje ya uwezo wangu.
“Lingekuwa ni suala la kazi hapo sawa lakini ni vizuri ukazungumza na mkurugenzi mwenyewe (Wema) lakini sidhani kama ataweza kuzungumza kwa sababu alikuwa anaumwa, amezidiwa na kupelekwa hospitali.”
WEMA ANAUMWA NINI?
Alipoulizwa Wema anaumwa nini, Kadinda alifunguka: “Sijajua lakini ugonjwa ni siri kati ya mhusika na daktari, cha msingi wewe ujue tu anaumwa.”
HUYU HAPA KAJALA
Baada ya kupita kote huko kusaka undani wa sakata hilo, Ijumaa lilimgeukia Kajala kwa njia ya simu ya mkononi akiwa jijini Mwanza na kumuuliza kulikoni kutibuana na Wema.
Huku sauti ikiwa chini, Kajala alisema: “Ni kweli kuna hali ambayo hata mimi mwenyewe nashindwa kuelewa lakini siwezi kuzungumzia kwa leo nikiamini yatapita.”

 

Umbea hauna kwao!!!!🙂
 
Toa huu ujinga huni tuna mambo serious ya kujadili sio haya mautumbo ya kina kajala sijui mara wema!! Mxxxxx
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…