Wema kawekeza zaidi ya bilioni 7 kwenye biashara ya vipodozi

Wema kawekeza zaidi ya bilioni 7 kwenye biashara ya vipodozi

Taarifa kutoka mtu wa ndani kabisa wa endless fame zinasema mwanadada mrembo Wema Sepetu katumia zaidi ya bilioni 7 to get her business up and running.Mrembo huyo ambaye ni miss Tz 2006 ambaye kila siku anazidi kuwa mrembo na kijana zaidi ukilinganisha na 2006 amepata hela zote hizo toka mauzo ya kazi zake za sanaa kutoka soko la nyumbani pekee.

Habari zinadai kuwa baadhi ya pesa hizo amewekeza kwenye viwanda vinavyotengeneza bidhaa zake huko China na zingine akiwekeza kufungua maduka makubwa ya kisasa Afrika Mashariki na Kati.Mtonyaji huyo amedai bila Wema Sepetu Bongo movie ingekufa miaka mingi iliyopita lkn Wema amekua akipambana kutengeneza kazi nzuri na za maana wakati movie yake ya mwisho iliuza kopi milioni 2 (ni kama double platinum hivi).

Wema na meneja Kadinda walipotafutwa kuongelea suala hilo hawakupokea simu lkn tulipojaribu kumpigia mdau wa karibu Petiman alidai yuko kwenye besidei ya dada diamond na akitoka angetutafuta.

CHANZO :GPL

Bilioni 7 za ki-bongo muvi.
 
Endless fame si iliporwa vitendea kazi na mtu aliemnunuliaga akaahidi baby "diamond" atamnunulia lakini wapi, kwaio mimi nilipo hapa nashangaa imefufuka vipi?
 
Hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaha
 
Mwakani kuna elimu ya bure inaanza itatubidi tusome ili tuongeze maarifa na kupunguza ama kuondoa kabisa kamasi vichwani mwetu.
 
billion saba labda kama kaziomba benk akatoa photocopy, yeye hata nyumba ya mil 150 hanna, anapanga sinza kwa wajanja.
 
Taarifa kutoka mtu wa ndani kabisa wa endless fame zinasema mwanadada mrembo Wema Sepetu katumia zaidi ya bilioni 7 to get her business up and running.Mrembo huyo ambaye ni miss Tz 2006 ambaye kila siku anazidi kuwa mrembo na kijana zaidi ukilinganisha na 2006 amepata hela zote hizo toka mauzo ya kazi zake za sanaa kutoka soko la nyumbani pekee.

Habari zinadai kuwa baadhi ya pesa hizo amewekeza kwenye viwanda vinavyotengeneza bidhaa zake huko China na zingine akiwekeza kufungua maduka makubwa ya kisasa Afrika Mashariki na Kati.Mtonyaji huyo amedai bila Wema Sepetu Bongo movie ingekufa miaka mingi iliyopita lkn Wema amekua akipambana kutengeneza kazi nzuri na za maana wakati movie yake ya mwisho iliuza kopi milioni 2 (ni kama double platinum hivi).

Wema na meneja Kadinda walipotafutwa kuongelea suala hilo hawakupokea simu lkn tulipojaribu kumpigia mdau wa karibu Petiman alidai yuko kwenye besidei ya dada diamond na akitoka angetutafuta.

CHANZO :GPL
Nashukuru sana kwa wazazi wangu kunipatia elimu.
Shule muhimu sana wana jamvi
 
Kwa kweli nahisi sipotezi mengi kwa kutokuwa mdau mkubwa wa hizi bongo muvi, hivi hizi habari huwa zinaandikwa kwa malengo gani? Kuyakuza maneno ili kumpaisha mtu? (mpaka tuamini lakini). Au kuandika uongo ili kukuza mauzo ya gazeti huku kinadharia wakichonganisha wasomaji na mtolewa habari? (manake msomaji lazima aone ni uongo na kuishia 'kumchamba' anayeongelewa kwenye hiyo habari)..
Teh teh watakuwa walimhoji na akasema hivyo....!
 
Acheni kumpamba huyo Wema..hv mnafanya mchezo na uwekezaji wa Billion.7?uwekezaji wa Billioni saba ndo uishie kwenye ka Frame ka Pale Mwenge karibu na maghorofa ya jeshi?nyie watuu..daah..iko hv..huyo wema kimsingi anatumika na jamaa mmoja ambaye ana kampuni inayouza software inayoitwa Problem Solved,Software inayotumika kwa maduka/supermarkets kwa ajili ya mauzo..sasa alimpa mtaji na kumtumia Wema kuwa Front..unafanya mchezo na Billion.7?na kwa taarifa yenu,lile gari alilopewa kwenye birthday ya mwaka jana,ambalo lilivunja uhusiano na diamond,pamoja na hili la mwaka huu,yote yametoka kwa Sebastian Ndege,yeye ndo yuko nyuma ya pazia..Wema ataendelea kuishi kwa kutegemea watu kumuweka mjini mpaka hapo atakapojipanga yeye kama yeye..Eti Billion.Saba..mfyuuuuuu++++

Yaani mie ile frem ya pale Mwenge ndio iliniacha hoi.... All the places ndio akaona pale kweli..

Ilikua kila nikipita natizama hilo duka linalopewa promo liko wapi kuja kuliona nilichoka ndani kwenyewe kweupe duka halijajaa kihivyo wala nini. Sembuse hizo bilioni 7.
 
Nina aleji na hesabu habari yoyote ikiwa na namba/hesabu huwa sielewi kabisa
 
Nahisi kakosea tu ni laki 7....!!! hahahaaaaaa!!!! Vigodoro amuachie nani huyo Wema, ana akili hata ya kufanya biashara ya mtaji wa laki moja yule... tuondole ----- hapa... story zenu za vijiweni ndio unatuletea hapa ili tufanyeje.
 
Wema ana nyumba tangu lini. Na sio yeye tu, sidhani kama kuna msanii hata mmoja wa kike bongo mwenye nyumba, zaidi ya kupanga na kuishi maisha ya kifahari kwa kutegemea wanaume waliokosa akili.

Wema hana hata kibanda?

Unacheza wewe. Wema ana nyumba ya milioni 400
 
Sal kweli maana ray c alikuwa najenga moja sijui wapi kule lakini akaishia njiani akaiuza
 
Back
Top Bottom