warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Hatimaye ! Manguli wawili wa Bongo Movies
waliokuwa mahasimu wakubwa na
kusababisha tafrani kubwa , Wema Isaac
Sepetu Beautful Onyinye na Kajala Masanja
K hatimaye wamekutana uso kwa uso ( live)
na kumaliza bifu lao saa chache kabla ya
kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ,
NI KWENYE VUNJA JUNGU
Tukio hilo la heshima lilijiri wikiendi iliyopita
nyumbani kwa staa mwenzao wa sinema za
Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson,
Mwananyamala jijini Dar ambapo baadhi ya
mastaa walikuwa wakivunja jungu katika
sherehe ya kumpongeza rafiki yao almaarufu
kwa jina la Wise Ime aliyejifungua mtoto wa
kike hivi karibuni .
KWA MARA YA KWANZA TANGU
WAGOMBANE
Katika tukio hilo, mastaa wenzao walipigwa
na butwaa kuwaona wawili hao wakiwa
pamoja kwa mara ya kwanza tangu
wagombane. miezi kadhaa iliyopita.
WALA UJANA KAMA ZAMANI
Mastaa hao walinaswa pamoja wakiwa kama
kumbikumbi wakila ujana kama zamani,
kitendo kilichowafurahisha marafiki zao
wengine waliofika nyumbani hapo
wakimpongeza Aunt kwa kuwaweka pamoja
kwani tangu wapatanishwe hawakuwahi
kukaa pamoja wala kula sahani moja kama
walivyofanya siku hiyo .
Ukweli sisi tumefurahishwa na ukaribu wa
hawa mashosti tuliwamisi sana kuwaona
hasa kwenye shughuli kama hizi za kibao
kata , leo wameshirikiana kama zamani ,
wamezungumza, wamecheka na kukata
mauno pamoja , alisikika mmoja wa mastaa
aliyehudhuria katika shughuli hiyo .
MAUNO MWANZO -MWISHO
Kwenye shughuli hiyo kulipambwa na mauno
mwanzo-mwisho yaliyoongozwa na wapiga
ngoma ya Kibao Kata ambapo kila mmoja
aliinuka na kuonesha ustadi wake wa kukata
mauno .
HADI MAJOGOO
Shughuli hiyo iliendelea hadi majogoo kwani
baada ya Kibao Kata , mastaa hao
walifunguliwa disko lililokuwa likiongozwa na
madj maalum wa Pro24 djs huku MC akiwa ni
Maimartha Jesse.
Katika shughuli hiyo , Wema , Kajala na Aunt
walipagawishwa na wimbo wa mpya wa
mpenzi wa Wema , Nasibu Abdul Diamond
Platnumz wa Mdogomdogo ambapo
waliingia kati na kuachia mauno hadharani .
Kuna wakati Kajala na Wema waliachiwa
nafasi ambapo walitoana jasho kwa kukata
mauno huku wakifuatisha vizuri wimbo huo
utadhani walikuwa wamefanya riheso .
NENO LA WEMA
Sasa hivi tupo vizuri sana. Yes tupo bega
kwa bega ukizingatia ndiyo tunaingia kwenye
mwezi mtukufu. Nimefurahi sana kushea naiti
na Kajala , alisema Wema .
NAYE KAJALA
Kwani kuna tatizo? Hakuna tatizo. Sisi tupo
vizuri kama alivyosema Wema tumeinjoi
sana, alifunguka Kajala .