Wema na Kajala watoana "JASHO" polisi

Wema na Kajala watoana "JASHO" polisi

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Kufuatia matusi ya mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu kwenda kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay', mastaa hao wamejikuta wakitoana jasho kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu Mabatini jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.

DURU ZA ‘KIUBUYU

Duru za ‘kiubuyu' zilidai kwamba Kajala, baada ya kuchoshwa na matusi hayo ambayo yalianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Wema, alijikuta akiishiwa na uzalendo kisha kuingia mzigoni ili kukomesha matusi hayo kwenye mitandao ya kijamii.

MATRIDA MBARONI

Ilidaiwa kwamba, Kajala akiwa na timu yake (Team Kajala) alifanikiwa kumtia mbaroni dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Matrida akidaiwa kwamba ni mfuasi wa Wema (Team Wema). Ilisemekana kwamba Matrida anayetumia jina la ‘Mat Kiboko Yao' kwenye ukurasa wake wa Instagram ndiye ambaye amekuwa akiongoza jahazi la kumtusi Kay.

Ilizidi kunyunyizwa kwamba sakata hilo la kuanikwa Instagram lilianza siku mbili baada ya ile pati ya kuzaliwa ya Wema ambapo Mat Kiboko Yao alimtukana Kajala matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini) kupitia ukurasa wake kwenye mtandao huo.

KAJALA ACHOKA, AKIMBILIA POLISI

Ilidaiwa kwamba Kajala alipoona amechoka kutukanwa, alitafuta wataalam ili kujua namna ya kumkamata na alipomjua ndipo akakimbilia Kituo cha Polisi cha Mabatini kwenda kutoa taarifa. RB Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.

Gazeti hili lilifanikiwa kunasa namba ya jalada la kesi hiyo iliyosomeka KJN/RB/8854/2014-

MATUMIZI YA MATUSI MTANDAONI.

Ilisemekana polisi walitumia mbinu zao na kufanikiwa kumkamata Mat Kiboko Yao na kumweka nyuma ya nondo za mahabusu kituoni hapo ndipo sarakasi za pande mbili zikaanza. KWANZA Mara tu baada ya Mat Kiboko Yao kukamatwa mishale ya saa 2:00 usiku, taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu ndipo Team Wema ikaingia mzigoni kutaka kumtoa mwanadada huyo lakini wakagonga mwamba.

WEMA, PETIT MAN WATINGA MABATINI

Ilidaiwa kwamba, baada ya Mat Kiboko Yao kutiwa mbaroni, Wema na jeshi lake akiwemo Petit Man walitinga Mabatini kwa ajili ya kumtoa mwanadada huyo lakini aligonga mwamba na kumuacha akilala kituoni hapo. "Yaani ulikuwa ni usiku wa kutoana jasho na kupimana ubavu kwamba nani ni nani.

Ilikuwa akitoka Kajala kuhakikisha kwamba mtuhumiwa wake aachiwi, Wema naye anatinga kituoni kwa mbwembwe kutaka Mat Kiboko Yao aachiwe kwa gharama yoyote. "Hapo ndiyo ngoma ilikuwa nzito, kila mmoja alikuwa anamuonyesha mwenzake kuwa ni zaidi na ni maji marefu hadi kulipokucha muvi likaendelea," alisema shuhuda aliyefuatilia sakata hilo kinagaubaga.

Mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu.

WAANDISHI WAPEWA UBUYU, WATINGA MABATINI

Kulipokucha, waandishi wetu walipewa ubuyu huo ndipo wakatinga Mabatini kisha wakatega ‘rada' zao na kuweka doria. Wanahabari wetu, wakiwa kituoni hapo walimshuhudia Kajala akilinda kituoni hapo asitokee mtu yeyote akamtoa Mat Kiboko Yao. Hata hivyo, alipoulizwa Kay kulikoni kuwa eneo hilo alisema alikuwa ameitwa kwa ajili ya kusuluhishwa badala ya kupoteza muda kwa jambo kama hilo.

KAJALA NA KUNDI LAKE

Awali Kay alionekana akiingia kituoni hapo na kundi lake la watu watatu akiwemo mwanaume mmoja ambapo yeye aliingia mpaka kwenye chumba cha mkuu wa kituo. Kajala akiwa kwa mkuu wa kituo, haikujulikana kilichokuwa kikiendelea ndani kwani kulikuwa na kikao cha muda mrefu ambapo ghafla Kajala na mtuhumiwa wake waliyeyuka.

WEMA AINGIA MITINI

Wakati hayo yakiendelea kituoni hapo, si Wema wala jeshi lake waliofika kwa ajili ya kumtetea Mat Kiboko Yao ambaye ndiye kiongozi wa Timu Wema kwa kutukana. Hata hivyo, baadaye alionekana mmoja wa marafiki wa karibu ambaye ni ndugu wa Mat Kiboko Yao aliyekuwa akihaha kumtoa mwenzake.
 
Ivi na wewe pet man si umeoa wewe? Hayo mambo ya kuambatana na mama ubaya kwenda kusutana na wanawake unayatolea wapi? Mmh kazi unayo mwaka huu
 
mmmhhhh!!!kazi ipo
kay nae ana mkono mrefu asa hv
 
Sijaelewa chochote.

Hata hivyo, ahsante kwa taarifa.
 
warumi hii habari ni mpya au ile nayoijua ?

unamlaumu petit man wakati babu yetu le mutuz ndio alisimamia show.
 
Last edited by a moderator:
warumi hii habari ni mpya au ile nayoijua ?

unamlaumu petit man wakati babu yetu le mutuz ndio alisimamia show.

Nakumbuka vizur ile campaign ya lemutuz ndo imeibua hii ishu, ila matikiboyao kihere here na kutafuta umaarufu kupitia wema ndo kumemponza, halafu pia alikuwa anaji expose sana mitandaoni ndo maana imekuwa rahis kukamatwa, tofauti na akina dogie masta,usipojipanga na team ukweli, naona matilda wale wanajifichaga nyuma ya keyboard kama akina warumi

Peti man nimempa makavu kwa sababu yeye sasa ivi ni mume wa mtu, kitendo cha kubebana na wema kwenda polisi kushabikia upuuzi ni aibu bhana, hayo mambo kwake yamepitwa na wakat
 
Last edited by a moderator:
Ha ha mahabati yake kwa mama ubaya kumeponza bichwa lake aache kutukana wenzake mitandaoni na sasa atakoma kimbele front chake
 
Kwa hiyo le mutuz ndio team kajala?????

Hata hivyo mati alitoka....jana alikuwepo kwenye kumvika miss tanzania bongesta taji
 
Halafu ile rekodi ya kajala kumteta wema hujaipata full???? Utuwekee

Ck anawatafuna bongo mavi kama bigjii ikiisha utamu tupa huyu vuta yule
 
we ambae hujaelewa sio bure ubongo wako ni kilobyte[kbz]...... nazingua no offence
 
Kwa hiyo le mutuz ndio team kajala?????

Hata hivyo mati alitoka....jana alikuwepo kwenye kumvika miss tanzania bongesta taji

Hahahahaha BADILI TABIA unajua utafungwa na lebaharia?

Jf ni mwisho wa matatizo hakika! Kwenye hii habari nimecheka hapo kwenye neno "DURU ZA KIUBUYU"
Nikavunjika mbavu zaidi na wewe ulipo uliza swali hilo kwenye red!

Halafu huyu aliyepelekwa polisi ndio yule aliyemuomba msamaha le baharia akamsamehe?
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo le mutuz ndio team kajala?????

Hata hivyo mati alitoka....jana alikuwepo kwenye kumvika miss tanzania bongesta taji

alitoka baada ya kumuomba msamaha kajala, maana boss wake aliyemtegemea kumtoa aligonga mwamba, ndo akome ushabiki maandazi
 
alitoka baada ya kumuomba msamaha kajala, maana boss wake aliyemtegemea kumtoa aligonga mwamba, ndo akome ushabiki maandazi

Warumi baada ya kuona hii habari nimekumbuka haya maneno ya lemutuz kwenye thread ya kuhusu kupambana na cybercrime!


"- Well, jana nzima nilikuwa Mwanza kwenye Instagram Party ambayo tumeweka record ya wananchi 5,000 waliojitokeza kuitikia mwito, so ndio kwanza nimerudi bongo maneno yako ni upotoshaji mtupu ukweli ni kwamba:-

1. Baaada ya kifo cha Betty ambaye kifo chake kunasaidikiwa kuchochewa na Cyber Abuse niliamua kuchukua initiatiave za kutaka kujua chanzo cha hili tatizo na kamba linaweza kupatiwa dawa, ni kweli nilionana na Cyber Polisi na Wakuu wengi wanaohusika na hii sekta Tanzania.

2. Majuzi kuna mtu alikamatwa baada ya kumtukana sana mtu mwingine ambaye alikuwa na akili za kwenda polisi na kutoa ushahidi kamili ambao uliishia kumnasa mtu huyu aambaye amekuwa akitukana sana Ma-Super Star karibu wote Tanzania bila kujali nani ni nani mpaka anakamatwa alikuwa amewatukana wengi including me.

3. Polisi wa Cyber walinifahamisha kuhusu kunaswa kwa mtu huyu na kunitaka niende kituoni, nilipokwenda kituoni nikashitushwa sana na yote niliyoyaona kuanzia nje ya kituo hasa waliokuwa wamekuja kumtetea yule mtu na wakipigana sana kumtoa kwa dhamana, binafsi pia alikuwa amenitukana sana lakini sikuona sababu ya kufanya anything kutokana na kumuona mtu mwenyewe anavyofanana.

4. Yule mtu kesho yake aliamua kusema ukweli mwingi sana kuhusiana na kazi yake hiyo ya kutukana watu asiowajua mitandaoni, ukweli ambao mpaka leo nashindwa kuuamini kutona na kuwajumuisha watu wengi niliokuwa ninawaheshimu sana kwamba kumbe wana tabia za kuwanunulia simu watu masikini wasiokuwa na uwezo na kuwanunulia bundle za internent ili wawatukane wasio wataka, na ili wawatukane wale wote wanaoshirikana na maaudi zao.

5. Kwa kweli yule mtu alisema mengi sana na aliomba sana radhi na msamaha kwa wote aliowahi kuwataukana na kuahidi kwamba hatarudia tena, so from there nikajifunza one lesson kwamba huyu mtu masikini wa Mungu ameonewa bure tu kwa sababu ya umasikini wake nikarudi Cyber Polisi na kuwaomba kuwakutanisha wale wote waliotajwa na huyu mtu ili wawapatanishe na kuwepo na amani baina yao kupunguza hivi vurugu kwenye mitandao ya kijamii.

- Otherwise mimi as me I make big money from mitandao na Isntagram iikiwa one of them pamoja na mtandano huu pia wa JF nao unanisaidia sana kutengeneza money, na nimesema siku nyingi sana kwamba biashara kama yangu ya mitandao ni kama biashara ya utumbo haikosi harufu so unapima uzito wa harufu na malipo bado malipo yanazidi harufu kwa mfano jana Mwanza tumefanya Instagram Party matokeo yamekuwa historia kubwa sana wananchi 5,000 walijitokeza, na hawa wote wananifahamu kutokea kwenye hiyo hiyo Instagram na JF kwa sababu kila dakika moja ilikuwa ni lazima mtu aniombe ku[piga picha huku akisema ananifuatilia from JF au Instagram,

- So naamini unaiona my point kwamba mimi unaweza kutukana as much as you want ila nakuhakikishia kwamba hupungzi anything in my life infact unazidi kuniongezea umaarufu, jana nilipofika Mwanza Tajiri mmoja mkubwa sana wa kule aliponiona Airport ya pale akaniomba sana niende nyumbani kwake maana mke wake ananipenda sana from Instagram nikaenda na nikakutana naye she was very happy,

- Mimi nipo kwenye Mitandao almost for the last 20 years now najua how this game works na wala sina wasi wasi na lolote I just sit back na kupima nini cha kujibu na nini sio cha kujibu katika kusimamia my interest. Kwenye Mitandao ninawatangazia biashara za Makampuni makubwa kama Airtel na Vodacom, wale wakiamini kwamba unachotukanwa ni kweli wanakukata mara moja kwenye pay roll yao, sasa ni miaka 3 nipo nao kuacha makampuni mengine mengi makubwa ninaofanya nao biashara online, so naomba kukwambia kwamba maneno yako juu hayana ukweli wowote lakini nakushukuru tu kwa kuniongezea umaarufu ambao unaishia kunilipa na kuniletea heshima kubwa sana NA WALE walio muhimu sana kwa maisha yangu ya kila siku, so wasiokuwa muhimu kwenye my life ya kila siku mna haki ya kusema kama mnavyofanya ila nawaambia kwamba nia na lengo lenu la kuniharibia toka muanze hamjafanikiwa na wala hamtafanikiwa kwa sababu watu wanahukumu baada ya kumuona mtu mwenyewe so watu wanasoma ujinga humu wakiniona wanajionea mtu ambaye wala hafanani kabisa na haya maneno ninazidi kupata kiki, so please keep on doing it mnanisaidia saana!!

- NA SASA THE NEXT INSTAGRAMNA PARTY NI MBEYA IN 2 WEEKS SO GET READY TUPO KWENYE TANZANIA TUOUR 2014"

Le Big Show
 
Back
Top Bottom