Wema ni chanzo cha matatizo, roho mbaya ni kinga dhidi ya majanga

Panda mti usiotegemea kutumia kivuri chake, saidia mtu usitegemee kulipwa chochote ukitegemea kulipwa ukafanyiwa vibaya mwisho utajilaumu tuu
 
wema usizidi uwezo
 
Kama mlikubaliana kuwa kila mwezi utoe Asante tekeleza ahadi ndugu. Hapo wewe ndio unashida
 
Ndugu elewa ukiwa unamwokoa nge kwenye kifo usidhani hatakuuma kwasababu asili yake nikuuma hata umuokoe bado atakuona adui hiyo ni asili kuna watu asili yao ndio hivyo huwa wanashindwa kujionyesha uhalisia wao sababu hana uwezo au hajafikia hiyo nafasi.

Tambua watu hubadilika kulingana na mazingiza na mabadiliko ya kiuchumi.
Kuna ambae akiwa kwao kijijini anakua mpole ila ukimleta mjini anabadilika hadi wewe uliemleta anakuona mbaya yaani unaweza msaidia mtu mchele mboga yaani kila kitu kasoro kibiriti cha kuwashia jiko la gesi lakina akakutangaza umemnyima kibiriti usishangae kaka.

Kuna ambae akiwa hana pesa anakua mpole muunganishe na kazi au mpe kazi atabadilika bila kukutambua

Ila usiache kusaidia wengine kumbuka kunawengine wanaitaji msaada wako ila hao sii kama nge ni kama jongoo au konokono tu hawana shida japo wanaweza wasiseme asante ila mtaachana kwaamani hata mkikutana hamnashida.

Mimi siwezi kusaidia mtu tena hua namwelekeza pita hivi imetosha unavyoona watu wanasema wananyanyaswa na ndugu zao wote sio kweli bali kila atakachokifanya anajiona yupo sawa na ukitaka aishi kwa namna hii anasema ananyanyaswa nibora kumsaidia mtu mwingine kuliko ndugu usitoe msaada bila kujua unampa msaada mtu wa namna gani nasema hiviiii? USIMSAIDIE MAMBA UKAMHIFADHI KWENYE SWIMING POOL YAKO, USIFUGE MAMBA KWENYE KARAI.
Ukiwa unampa punda chakula usimpe bali mtupie.
Usimpe mbwa chakula ikiwa unajua utachukua hiyo sahani akiwa bado anakula utapigwa jino yeye hatajua kama ulimpa au unataka kuwekea nyama ataona unamnyang'anya na hapo atakuhukum chap na ndio binadam tulivyo usisahau asili yetu.
 
wema unaponza jaman yaliyonikuta sina hamu ungekuta naitwa chizi naokota makop
yule unaye mpa msaada
hugeuka kuwa adui namba moja
kama unauwezo wa kusaidia
nenda kwenye vituo vya watoto yatima au mahospitalin saidia
au msaidie mtu ambae hakujui wala humjui na si mahali pa kazi nimejifunza
 
Risk kubwa ni pale Mungu anapokua amekujibu lakini wewe bado hujui na unaendelea kumuomba.
 
Pole sana, niliacha kusaidia hata ndugu
 
Wema ni mbaya sana kama utatenda wema ukasubiri shukran , ila wema ni jambo jema sana, kama utatenda wema na kwenda zako.
 
Unapomsaidia MTU usiweke ile nia ya kusubiri kulipwa na huyo MTU uliyemsaidia maana utalipwa kwa njia tofauti.

Kinachofanya watu mliosaidia watu kuishi kwa mashaka ni pale mnaposaidia mkiwa mnanungunika Sana .this is hell.


Ukiona unataka msaidia MTU Ila unaumia nakushuri huyo MTU usimsaidie maana wewe unakuwa hauja-Qualify kusaidia.


Giver hawezi kuwa taker and taker hawezi kuwa Source.

Na mwisho watu weusi hawajawa na ufahamu wa mambo mengi so play but play precautionary.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…