ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Mama yake Wema Sepetu, Bi Mariam Sepetu afunguka kwa ghadhabu akiwatakia wale wote ambao wamekuwa wakifuatilia maisha ya mwanae hasa waandishi wa habari za Udaku waache mara moja vinginevyo atakula nao sahani moja.
Akieleza kwenye Kipindi cha "Take One" kinachorushwa na Clouds TV, amejigamba kuwa mwanae alikuwa na "tabia nzuri" lakini baadhi ya marafiki wamemharibu japo bado anakubalika na watanzania wote.
Amesema wengi wa marafiki walifikia hata kumpeleka kwa waganga wa Kienyeji, na kuna wengine amefikia kuwafukuza kabisa wasikanyage nyumbani kwake kutokana na tabia zao.
Akifunguka kwa maneno tata mama huyo amesema kuwa ana mchukia sana Diamond kutokana na "kumtumia mwanae" kwa ajili ya mafanikio yake ya kimuziki (hakufafanua kimtumia mwanae kivipi?) ila alisema kuwa ameyajua hayo baada ya kuzunguka.
Alieleza pia kuwa amehangaika sana kumrudisha Wema hapa alipofikia sasa. Aalisema kuwa amegundua mengi sana ambayo marafiki zake walikuwa wakimfanyia (hakuwataja zaidi ya Jackline Whopper) ambae anasema aliwahi kumtusi mwanae wakati fulani kuhusu maangaiko yake na kusema hana pa kuishi.. "Huyo Whopper aelewe Wema hapa ndio nyumbani kwao alipozaliwa" aling'aka mama huyo.
Kuhusu mahusiano ya Wema na Diamond alisema, alimchukia sana Diamond tokea walipoanza mahusiano na Wema kwani Diamond alilenga kumtumia tu mwanane kufika pale alipo lakini atashuka muda si mrefu. "Diamond hana adabu hata kidogo, kijana huwezi kumchukua binti wa watu ukaenda kumvisha pete ukumbini hata wazazi wake hawajui wala hujaenda kujitambulisha kwa wazazi wake...hii ni dharau kubwa sana aliyoifanya na mimi nilisema, kamwe asingeweweza kuishi na mwanagu kama mimi mzazi wake sijapenda".
Alionya kuwa kwa sasa mwanae WEMA amemtengeneza na hakuna atakaweza tena kumvuruga kama mwanzo.... Hata hivyo, Mzazi huyu aliyeonekana akiongea kwa machungu hakuweza kufafanua mwanae amemtengeneza namna gani....
Pata Majigambo mazima ya mama huyo hapa:

Last edited by a moderator: