Wema Sepetu akesha akimlilia Tundu Lissu

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598

Wema Sepetu.

TUKIO la kushambuliwa kwa kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida-Mashariki, Tundu Lissu ambaye ni wakili na Mwanashieria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limewaliza wengi akiwemo staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ambaye anadaiwa kukesha akilia hivyo kuibua sintofahamu kwa watu waliomzunguka.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Wema ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, taarifa hizo zilimchangaya hasa ukizingatia kuwa Lissu ni ndugu yake na pia ni wakili wake katika kesi inayomkabili ya matumizi ya madawa ya kulevya.

“Taarifa za Lissu kupigwa risasi zilimchanganya sana Wema. Tangu apate taarifa hizo amekuwa akilia sana hadi kila mtu akaogopa. Tulihisi anaweza akapoteza fahamu au akapata ugonjwa hivyo tulitaka kumpeleka hospitalini, akapumzishwe,” kilisema chanzo hicho.




Tundu Lissu.

Chanzo hicho kiliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya Wema kuangua kilio usiku kucha na mchana kutwa, mwishoni mwa wiki iliyopita alibadilisha staili ambapo alikuwa halii, badala yake aliamua kujifungia ndani akimuombea kiongozi huyo.

“Huwezi kuamini, sasa Wema amekuwa ni mtu wa kusali tu akimuomba Mungu ampe Lissu ahueni na hali yake ilirudi kama zamani,” kilisema chanzo.

Katika kutafuta ukweli wa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Wema ili kuthibisha madai hayo ambapo alisema kuwa, hakuna kitu kilichomuuma kama hicho na bado kitaendelea kumuumiza hadi aone hali ya Lissu inatengemaa na kurudi kwenye majukumu yake ikiwemo kumtetea kwenye kesi yake.

“Naendelea kuumia hadi nitakapomuona Lissu akiwa katika hali nzuri kama mwanzoni,” alisema Wema.


Muungwana
 
Huyu nae ni chizi tuu..sasa kwanini asiende kenya? Na hivi Lissu alitengana na mkewe basi huyu chawote ameshaona fursa...
Mbona mke wa TL amekuwa akionekana wazi wazi? Mfano wakati wa uchaguzi wa rais wa TLS, wakati TL alipokamatwa na kutakiwa kupimwa mkojo mkewe alihojiwa akiwa maeneo ya mahakama na wakati wa hili tukio Mkewe yuko naye Nairobi.Lakini TL mwenyewe kuna clip anasema sipendi kulala mahabusu, mahabusu si pazuri ,nina mke ,nina watoto na nyumba nzuri kabisa. Sasa unaposema TL hana mke mbona kama sikuelewi mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisapoti kupigwa risasi Lissu, na ninamuombea afya njema arudi kulitumikia taifa, ila hii mada title yake inachekesha sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni haki yake kumlilia kwa kuwa ni Lissu aliyemsaidia kwenye kesi yake ya madawa ya kulevya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…