Wema Sepetu amefiwa, kesi yake yapigwa kalenda

Wema Sepetu amefiwa, kesi yake yapigwa kalenda

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
301,221
Reaction score
1,172,274
Kesi ya kutumia madawa ya kulevya inayomkabili Malkia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu imeahirishwa leo katika Mahakama ya Mkazi Kisutu hadi Desemba 14 mwaka huu.

Akieleza sababu za kuahirishwa kwa kesi hiyo Wakili anayemsimamia Wema Sepetu, Peter Kibatala amesema mteja wake amefiwa hivyo asingeliweza kufika Mahakamani leo.

Wema Sepetu anakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya aina ya Bangi na tayari pande zote mbili zimesha wasilishaushahidi mahakamani.

=======
Wema Sepetu kukamatwa na kuhukumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya
Yaliyojiri katikati ya mchakato wa upelelezi wa kesi ya wema
Wema kukutwa na kesi ya kujibu
Kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini
 
Anajichelewesha kujumuika na mwenzake,shauri yake,akija kuhukumiwa mwenzake atakuwa anatoka atabaki peke yake kule.
 
Bado yupo huko,nadhan kaenda kuhan msiba wa shemeji ndiku ndo maana mahakaman wakasema kafiwa,ila insta na snapchat yupo na furaha kubwa ya kutoka nje ya nchi kupunga upepo
Amerud toka Rwanda kwani
 
Bashite katumia kodi za wananchi na makelele kibao anatafuta dawa za kulevya, mwisho kaishia na Wema Sepetu na kipisi cha bangi. Huu si ulofa huu?
 
Kodi Zetu zinatumika vibaya,naomba DPP afute hii kesi asiendelee nayo,kuna kesi za msingi nyingi zipo pending zinahitaji kusikilizwa,tuachane na kesi za kutafuta mileage kisiasa (kiki).
 
Back
Top Bottom