
Ishu ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutopata ujauzito imeshazungumzwa mara kadhaa na hata yeye mwenyewe alishawahi kujitokeza na kuizungumzia lakini safari hii amelizungumzia kwa njia tofauti. Wema ambaye pia ni muigizaji wa filamu, awali alisema sababu kubwa ya kutopata ujauzito ni masuala ya kiafya lakini safari hii ametoa kauli tata ambayo inahusiana na imani za nguvu za giza.
Wema ambaye alifunguka hayo hivi karibuni, anadai kuwa yawezekana marehemu Steven Kanumba anahusika kwenye suala hilo. Mizimu ya Kanumba "Unajua hili suala la mtoto linanisumbua sana yaani na linaniuma kwa sababu napenda watoto sana na pia napenda kuitwa mama, nimehangaika sana katika kuhakikisha nafanikiwa katika hili lakini ndiyo hivyo imeshindikana.
"Serious! Ilifika kipindi yaani nilikuwa nachukia nilipokuwa nikiziona siku zangu, nilikuwa sipendi kukutana na hiyo hali kwa sababu naumia sana lakini ndiyo hivyo baada ya kuhangaika sana inabidi nimwachie Mungu tu. Nahisi kukata tamaa lakini bado sijakata tamaa.http://www.bongonewstz.com/2015/06/wema-sepetu-amtaja-mtu-anayemzuia.html