Wema Sepetu apata ushauri kwa kutokuwa na mtoto

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Ni ndefu lakini someni itawasaiDia huyu dada alie toa ushauri anaitwa rose

ashukuriwe MUNGU wetu kwa kutubariki kuiona siku hii yamleo tukiwa wazima wenye afya na akiwa ametuandalia baraka tele siku nzima hii ya leo basi tuwe tayari kuzipokea
Part 1....leo naomba niandike hii kwa Wema Sepetu sijui kama ananifollow lakini najua wapo wengi wanaonifollow ambao anawafollow kwahiyo wakirepost inaweza kumfikia alipo
Dear Wema kabla hujaja humu duniani MUNGU alikujua na alikuumba wewe kwa mikono yake, akaweka hiyo sura yako nzuri, akakupa huo mwili wako ambao wanawake wengi wanaupenda wangekua nao, akakupa na sauti ambayo ukiongea kila mtu anataka asikie unasemaje, amekupa mikono ambayo unafanya kazi kwa njia yoyote hukosi kuweka chakula mezani na sio kula mwenyewe tu bali kuwalisha na wengine pamoja na watoto yatima MUNGU amekubariki unaishi sehemu nzuri ambazo watu wengine wanatamani japo waingie kwa siku moja tu, unamagari ya kifahari ambayo yanakufanya mwili wakao mzuri usiungue na jua kali wala mvua nzito ikinyesha, unawatu wanaokuhudumia with first grade kila unapoingia wakati watu wengine kutaka kuhudumiwa hivyo mpaka wahonge, watoe miili yao ama waongee kuonyesha hawapati huduma lakini for you watoa huduma wanakukimbilia kama malkia, unamarafiki wengi wanaokupenda na kua nawe, unafollowers lukuki ambao wanaokupenda watakaosimama na wewe kwa lolote mpaka MUNGU atakapoamua kukuchukua unapia watu wanaokuchukia hawa ndio wanaokupa baraka zaidi maana wanavyotaka kukuleta chini bila sababu MUNGU ndio anakuinua mara saba kwa mema unayoyafanya duniani
My dear post yako imeniuma sana na kujitahidi kuvaa viatu vyako lakini vimepywaya nimeshindwa, MUNGU alipokuumba alikua na sababu ya kukumba mwanamke na akajua kwa wakati wake yeye atakubariki upate mtoto kama wanawake wengine wengi, lakini pia watu wote tujue ni huyo huyo MUNGU ambaye hawapi wanawake wengie watoto sio kwamba kwasababu hawastahili hapana bali........INAENDELEA
 
Part 2....hajawapa uwezo wa kupata mtoto kwakua wanauwezo wa kua na watoto zaidi ya mmoja wema unamoyo wa kupenda mkubwa sana, unauwezo wa kukaa na watoto yatima hata watano ukawalea kama wanao nguvu hizo, mali hizo na uwezo huo unao tena ukawasomesha, wakala, wakalala, wakavaa na wakaenjoy maisha NI WANAWAKE WACHACHE SANA WALIOBARIKIWA KAMA WEWE
Post nyingi sana na mikasa mingi sana niliyosolve hapa kwenye page wanawake wakipewa mimba tu wanahaha mpaka kutoa wengine wametoa mara nne kwanini wanaogopa kulea huyo mtoto mmoja tu MUNGU aliyewapa mmoja tu mwanamke anaona bora atoe kwakua anaogopa maisha ya kumlea duniani mwanamke kama huyu naye awekwe kwenye kundi gani ungekua na wewe umepata na ukatoa bado wangekusema hata kama ingetoka bahati mbaya ungeambiwa umetoa kilazima, ama kisa umepata danga kumbe imetoka tu bahati mbaya
Lakini pia MUNGU hajakupa mtoto kwasababu bado anakutengenezea mtoto wa kufanana na wewe, wewe ni mpiganaji mwenye moyo mzuri MUNGU hataki huwahi kupata mtoto ambaye atakusumbua awe mchoyo, mwenye kiburi, awe msema watu, mtukana watu, mwizi kwasababu anasema mtoto wa aina hiyo yupo mbinguni hajapata mama wa kuwekewa tumboni je unamtaka????
Pia MUNGU bado anakutafutia mwanaume mwenye uwezo wa kuzaa na wewe, umeshakua na wanaume wengi ndio ulitaka kuzaa nao kipindi hiko labda wao walikua tayari lakini wewe hukua tayari ama wewe ulikua tayari lakini wao hawakua tayari ama wote mlikua tayari lakini MUNGU akasema hakuna mbegu kati yenu inayofaa kwa mimi kumpa Wema mtoto mwanaume ambaye nataka Wema azae naye sio kati ya hao wanaume nitamuandaa na kumpa Wema wakati ambapo nitaona wote wawili wapo tayari kupokea huyu mtoto wa kuendana nao....INAENDELEA
 
Part 3...So honey take your time and enjoy the ride, mpaka hapo MUNGU atakaposema muda wako umefika ndio utakua umefika kila mtu anamuda wake na wakati wake wa CHANGES honey wako upo haujafika tu na hao wote wanaokusema kama wamezaa waambie wakusanye watoto zao wote wakuletee nyumbani uwasaidie kulea ili wao wawe free kuzidi kutunga na kuandika maneno kuhusu wewe maana wewe ni motherly figure na upo tayari kulea wakati hao ni talk n write figure wamejaaliwa kusema ya watu tu na sio malezi na tena sintoshangaa wengine wanaokusema jana ama juzi wametoka kutoa mimba, ama kusafishwa ili wapate mimba yani hawana hata watoto uwezo wa kua nao hawana
Honey you are a STAR nyota ambayo inawaka na kuwaumiza wao sasa, itawaumiza macho hata wakiwa wamebeba mimba, na hiyo nyota yako itawaumiza hata watoto wao baadae wakishakua maana kama MUNGU atakupa maisha marefu bado nyota yako itang'aaaa miaka na miakaa mingi ijayo hadi wajukuu zetu waikute...nani ambaye hataki hiyo hahahaha girl you are blessed start counting the blessings you can see and touch and let GOD count for you those you cant see and touch
Naomba jana iwe mara ya mwisho ya wewe kujitetea kwa wanadamu kwanini hupati mtoto maana wanadamu hawatakusaidia sanasana watakuumiza kwa maneno yao ya kashfa wewe mlilie MUNGU wako tena ukiwa peke yako chumbani endelea kumuiliza if the time is here or not and if its not usiumie moyo maana utakufuru endelea kufurahia maisha huku ukisubiri wakatu wa MUNGU akupe mtoto na kumbuka ITS NOT OVER UNTIL GOD SAY ITS OVER....
 
Huo ni ushauri au mahubiri? Halafu hakuna kitu hapo zaidi ya kumsifia.Anatafuta kick tu huyo hana lolote.
 
ivi wema aoni kuwa anazidi kujidhalilisha? ye anaona sifa kutangaza eti hazai
aoni mwenzake jide kauchuna tu
 
Sijaona jipya hapo zaidi ya kuzidi kumdanganya na kuto mwambia ukweli kuwa wanao mtukana wana mtukana kwa kuwa wameona matusi hayo yana mfaa na ndio maisha aliyo yachagua!

Yeye si wa kwanza kutokupata mtoto kwanza ni ajabu kwa umri wake mdogo kuanza kulia lia na kutafuta huruma as if nchi hii ni yeye pekee ambaye hana mtoto!

Mshaurini aache kugeuza mitandao kuwa sehemu ya maisha yake .na atalia sana hasipo badilika!
Baada ya kumshauri atafute mume aolewe mna mpa mahubiri yasiyo na tija ..atapataje mtoto bila mwanaume.

Anavuna anacho panda wala tatizo lake si kupata mtoto kwa sasa bali anajaribu kujifananisha na watu ndio tatizo lake!

Wema ana tafuta huruma zisizo na msingi ni bora akakimbilie masjid au kanisani kuliko kukimbilia insta..
Na washangaa mnao muonea huruma bila sababu.

Hii ni kick tuu...anavuna alicho panda.
 
Uyu alishachomoe zakutosha! kizazi kipo km hakipo!
 
Huo ni ushauri au mahubiri? Halafu hakuna kitu hapo zaidi ya kumsifia.Anatafuta kick tu huyo hana lolote.

Kweli tupu hivi kama alichezea na kutupa huko Mungu atampa kweli mtoto maisha ya ujana ni kuwa nayo makini.
 
Kweli tupu hivi kama alichezea na kutupa huko Mungu atampa kweli mtoto maisha ya ujana ni kuwa nayo makini.

Wewe acha tu.Mungu na atuepushie. Ila mimi naona wema bado mdogo tu asikate tamaa.
 
Mpe basi wema hata mtoto mmoja shem, ile timu yako si mchezo

Hahahaaa,itabidi nimpe kweli shem wangu.
Wewe pia nitakupa wawili ili niokoe ndoa yako ambayo iko katika hatua za tia maji tia maji! Miaka 10 bila mtoto sio mchezo ati?
Hongera kwa uvumilivu laki si pesa!
 
Last edited by a moderator:
Eti kick tuu.....!
Nyie nyie ndo mnaomprovoke halafu leo ndo mnajifanya majudge!
Jide mwenyewe huwa haongelei suala la kutopata/kupata mtoto lakini binadamu haweshi kumtukania.

Wahila wahila tu hata kama angeufyata bado watatafuta la kuongea.

 
Huyu binti sio mzima... Hujafikisha miaka 30 huna mume umejuaje kama huzai?
Tatizo hatulii na mwanaume mmoja japo miaka miwili ikapita. Leo huyu, kesho yule, mimba itatunga saa ngapi. Mastress ya kujitakia kibao, huwezi shika mimba.
Atulie hata kama hajaolewa lakini awe na mahisiano na mwanamme mmoja kwa muda mrefu, mimba naamini insha allah itashika. Uzazi kwa wanawake haulingani. Kuna wenye uzazi mwepesi, one kick kiti hicho mradi ziwe siku za kupata mimba. Mwingine unahitaji good relaxation and out of stress ndio mimba inashika.
Amepata ugonjwa ule wa wanawake wote.
Mkiwa group moja marafiki, wanaolewa wenzako wote unabaki wewe, unachanganyikiwa. Mwisho unatafuta nungayembe wenzio ndio frnds wako, anaanza kuzaa mmoja baada ya mwingine hadi wote wana watoto, unabaki wewe. Unachanyikiwa x 2, ndio hali aliyonayo Wema kwa sasa, japo kasahau she's still very young.
 
Kweli tupu hivi kama alichezea na kutupa huko Mungu atampa kweli mtoto maisha ya ujana ni kuwa nayo makini.

Kwahiyo Mungu anawaadhibu tu wanaotoa mimba ila wanaozini aakhaaa!!!
Maana kuzini na kuabort zote ni dhambi na mshahara wa dhambi ni mauti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…