Glasnost
JF-Expert Member
- May 18, 2017
- 266
- 259
Wakati Bodi ya Filamu ikiwa imemfungia mwigizaji na mfanyabiashara Wema Sepetu kwa mda usiojulikana kujihusisha na masuala ya filamu, huku Chama cha Waigizaji Wilaya ya Kinondoni (TDFAA) kikimfungia kwa miaka miwili. Kimezitaka Mamlaka za Serikali zipuuze utetezi wa Wema Sepetu kwa kudai kuwa una lengo la kuzipumbaza zisimchukulie hatua.
Baadhi ya wasanii hawakuwa nyuma “kumvaa” Wema Sepetu. Muigizaji Ray Kigosi alimshauri kutumia mitandao kuingiza fedha na sio kufanya mambo ya hovyo huku Kulwa Kikumba “Dude” akiuliza kwamba, “tutalea ujinga huu mpaka lini?”, nakuishia kuipongeza bodi ya filamu kwa adhabu aliyopewa.
Kwa jinsi jambo hili lilivyochukuliwa na watawala na baadhi watu inasikitisha na kushangaza kwa namna ya kukasirisha na kuchekesha. Sheria za kukandamiza sanaa kama kufungia miziki, filamu, magazeti na mitandao ya kijamii kama njia ya kupunguza vitendo hivyo ni kutojua tulipotoka na tunapokwenda. Pia uelewa mdogo wa watawala,wananchi na viongozi mbalimbali katika kufanya maamuzi ni tatizo sugu na umefika mda wa kukemea na kufuta fikra hasi juu ya nini hasa maana ya uhuru na haki za mwanadamu.
Wema Sepetu hukutakiwa kuomba msamaha na hustahili adhabu ulizopewa na Bodi ya filamu Tanzania na Chama cha Waigizaji Wilaya ya Kinondoni (TDFAA) au hata kutoka mamlaka zingine ikitokea hapo baadae kwasababu ni jambo binafsi na wala serikali au mtu yeyote haitaji kulifanya ni jambo lake hata kama lamchukiza au hapendi. Kulifanya ni jambo la kitaifa ni kukosa maarifa na uvumilivu wa desturi tafauti na zisizo na madhara yeyote kwa mtu mzima.
Kuomba radhi Watanzania ni kosa kubwa ulilofanya aidha kwa kujua ua kutojua au kwa shinikizo la watu fulani. Ona sasa ulivyoabikia kwa kutokuwa na msimamo juu ya nini unataka au unachoamini. Kosa lako lilikuwa ni nini?. Nani kasema watanzania wote wamechukizwa na wewe kuweka kitu hicho kwenye akaunti yako? Hakuna kosa pale, lile ni jambo lako binafsi. Na nataka kuamini ni furaha tu na ulitaka mashabiki wako wajue kinachoendelea.
Tunajenga jamii ya kuamini kuwa kila jambo la mtu fulani awe maarufu au sio maarufu ni la kitaifa na ni lazima afanye vile watu fulani wanataka kwakua ni watawala au wana nguvu kutokana na vyeo vyao au imani za kidini hata kama wanakosea au kuingilia uhuru wa mtu.
Tuache “kudanganyana” na kulazimisha kutumia sheria kandamizi katika suala la utamaduni wa Mtanzania. Fikra za aina hii ni za kupigwa vita siku zote kwani zinajenga jamii ya watu wasiojitambua na wenye ufahamu mdogo au sifuri kabisa juu ya nini maana ya haki za mwanadamu na uhuru wa kuishi maisha utakayo bila kuingiliwa na mtu au serikali.