Wema Sepetu hukutakiwa kuomba radhi

Wema Sepetu hukutakiwa kuomba radhi

Glasnost

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2017
Posts
266
Reaction score
259
Wakati Bodi ya Filamu ikiwa imemfungia mwigizaji na mfanyabiashara Wema Sepetu kwa mda usiojulikana kujihusisha na masuala ya filamu, huku Chama cha Waigizaji Wilaya ya Kinondoni (TDFAA) kikimfungia kwa miaka miwili. Kimezitaka Mamlaka za Serikali zipuuze utetezi wa Wema Sepetu kwa kudai kuwa una lengo la kuzipumbaza zisimchukulie hatua.

Baadhi ya wasanii hawakuwa nyuma “kumvaa” Wema Sepetu. Muigizaji Ray Kigosi alimshauri kutumia mitandao kuingiza fedha na sio kufanya mambo ya hovyo huku Kulwa Kikumba “Dude” akiuliza kwamba, “tutalea ujinga huu mpaka lini?”, nakuishia kuipongeza bodi ya filamu kwa adhabu aliyopewa.

Kwa jinsi jambo hili lilivyochukuliwa na watawala na baadhi watu inasikitisha na kushangaza kwa namna ya kukasirisha na kuchekesha. Sheria za kukandamiza sanaa kama kufungia miziki, filamu, magazeti na mitandao ya kijamii kama njia ya kupunguza vitendo hivyo ni kutojua tulipotoka na tunapokwenda. Pia uelewa mdogo wa watawala,wananchi na viongozi mbalimbali katika kufanya maamuzi ni tatizo sugu na umefika mda wa kukemea na kufuta fikra hasi juu ya nini hasa maana ya uhuru na haki za mwanadamu.

Wema Sepetu hukutakiwa kuomba msamaha na hustahili adhabu ulizopewa na Bodi ya filamu Tanzania na Chama cha Waigizaji Wilaya ya Kinondoni (TDFAA) au hata kutoka mamlaka zingine ikitokea hapo baadae kwasababu ni jambo binafsi na wala serikali au mtu yeyote haitaji kulifanya ni jambo lake hata kama lamchukiza au hapendi. Kulifanya ni jambo la kitaifa ni kukosa maarifa na uvumilivu wa desturi tafauti na zisizo na madhara yeyote kwa mtu mzima.

Kuomba radhi Watanzania ni kosa kubwa ulilofanya aidha kwa kujua ua kutojua au kwa shinikizo la watu fulani. Ona sasa ulivyoabikia kwa kutokuwa na msimamo juu ya nini unataka au unachoamini. Kosa lako lilikuwa ni nini?. Nani kasema watanzania wote wamechukizwa na wewe kuweka kitu hicho kwenye akaunti yako? Hakuna kosa pale, lile ni jambo lako binafsi. Na nataka kuamini ni furaha tu na ulitaka mashabiki wako wajue kinachoendelea.

Tunajenga jamii ya kuamini kuwa kila jambo la mtu fulani awe maarufu au sio maarufu ni la kitaifa na ni lazima afanye vile watu fulani wanataka kwakua ni watawala au wana nguvu kutokana na vyeo vyao au imani za kidini hata kama wanakosea au kuingilia uhuru wa mtu.

Tuache “kudanganyana” na kulazimisha kutumia sheria kandamizi katika suala la utamaduni wa Mtanzania. Fikra za aina hii ni za kupigwa vita siku zote kwani zinajenga jamii ya watu wasiojitambua na wenye ufahamu mdogo au sifuri kabisa juu ya nini maana ya haki za mwanadamu na uhuru wa kuishi maisha utakayo bila kuingiliwa na mtu au serikali.
 
Mwenye hio video ya wema anitumie whatsapp chap ili nijue natoaje comment hapa
No: 0683011003
 
We na we sasa TCRA walivyoipitisha sheria ya kuzuia maudhui ya kingono ulidhani wanamaanisha nini?

Hata kama angesapotiwa na wasanii wote mwisho wa siku sheria ndiyo inasema alichofanya ni kosa kisheria.
 
Hilo ndo jibu
Hope mleta mada hazijui sheria za nchi yetu
 
sheria itafuatwa tu no matter wapuuzi wangapi wanapinga
 
Kwani Muendelezo wa ile Video umetoka?
Badala kuleta muendelezo analeta samahan.
 
Bila shaka wema ana matatizo ya akili, kwa hali ya kawaida hayupo sawa kabisa
 
Nimemtizama msanii mwenzie Jimmy Mafufu YouTube nikavutiwa zaidi na mawazo yake juu ya hii kadhia, wema anatakiwa apewe lifebun kwenye sanaa, dawa ya mtu mpuuzi ni kuwa mpuuzi zaidi yake.
 
Wakati Bodi ya Filamu ikiwa imemfungia mwigizaji na mfanyabiashara Wema Sepetu kwa mda usiojulikana kujihusisha na masuala ya filamu, huku Chama cha Waigizaji Wilaya ya Kinondoni (TDFAA) kikimfungia kwa miaka miwili. Kimezitaka Mamlaka za Serikali zipuuze utetezi wa Wema Sepetu kwa kudai kuwa una lengo la kuzipumbaza zisimchukulie hatua.

Baadhi ya wasanii hawakuwa nyuma “kumvaa” Wema Sepetu. Muigizaji Ray Kigosi alimshauri kutumia mitandao kuingiza fedha na sio kufanya mambo ya hovyo huku Kulwa Kikumba “Dude” akiuliza kwamba, “tutalea ujinga huu mpaka lini?”, nakuishia kuipongeza bodi ya filamu kwa adhabu aliyopewa.

Kwa jinsi jambo hili lilivyochukuliwa na watawala na baadhi watu inasikitisha na kushangaza kwa namna ya kukasirisha na kuchekesha. Sheria za kukandamiza sanaa kama kufungia miziki, filamu, magazeti na mitandao ya kijamii kama njia ya kupunguza vitendo hivyo ni kutojua tulipotoka na tunapokwenda. Pia uelewa mdogo wa watawala,wananchi na viongozi mbalimbali katika kufanya maamuzi ni tatizo sugu na umefika mda wa kukemea na kufuta fikra hasi juu ya nini hasa maana ya uhuru na haki za mwanadamu.

Wema Sepetu hukutakiwa kuomba msamaha na hustahili adhabu ulizopewa na Bodi ya filamu Tanzania na Chama cha Waigizaji Wilaya ya Kinondoni (TDFAA) au hata kutoka mamlaka zingine ikitokea hapo baadae kwasababu ni jambo binafsi na wala serikali au mtu yeyote haitaji kulifanya ni jambo lake hata kama lamchukiza au hapendi. Kulifanya ni jambo la kitaifa ni kukosa maarifa na uvumilivu wa desturi tafauti na zisizo na madhara yeyote kwa mtu mzima.

Kuomba radhi Watanzania ni kosa kubwa ulilofanya aidha kwa kujua ua kutojua au kwa shinikizo la watu fulani. Ona sasa ulivyoabikia kwa kutokuwa na msimamo juu ya nini unataka au unachoamini. Kosa lako lilikuwa ni nini?. Nani kasema watanzania wote wamechukizwa na wewe kuweka kitu hicho kwenye akaunti yako? Hakuna kosa pale, lile ni jambo lako binafsi. Na nataka kuamini ni furaha tu na ulitaka mashabiki wako wajue kinachoendelea.

Tunajenga jamii ya kuamini kuwa kila jambo la mtu fulani awe maarufu au sio maarufu ni la kitaifa na ni lazima afanye vile watu fulani wanataka kwakua ni watawala au wana nguvu kutokana na vyeo vyao au imani za kidini hata kama wanakosea au kuingilia uhuru wa mtu.

Tuache “kudanganyana” na kulazimisha kutumia sheria kandamizi katika suala la utamaduni wa Mtanzania. Fikra za aina hii ni za kupigwa vita siku zote kwani zinajenga jamii ya watu wasiojitambua na wenye ufahamu mdogo au sifuri kabisa juu ya nini maana ya haki za mwanadamu na uhuru wa kuishi maisha utakayo bila kuingiliwa na mtu au serikali.
Weka picha ya rais Durtete akimkisi mwanamke jukwaani
 
Nijuavyo ukitenda dhambi basi usiseme kwa watu ama kuhadithia, we omba toba kwa mola wako yatosha....
Kwa mujibu wa imani yangu lakini
 
Mie mwenyewe nachukia kabisa kuvaa nguo,kiufupi sizipendi yaani....ila ndo nalazimika kuvaa tu,kwa faida ya jamii.
 
Naendelea kusaka pesa.siku zikitimia naenda kumtafuna wema sepetu hata kama kaniacha miaka kama 6.
Ntamtafuna vizuri tu niache historia ya ajabu na mimi
 
Mwenye video ile ya makonda akimtetea wema kuwa ni Tanzania sweet heart naiomba
 
Back
Top Bottom