Wema Sepetu kupandishwa kizimbani

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mkono wa sheria ! Achana na drama zake na aliyekuwa mwandani wake , Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz' , mcheza sinema ' grade one ' Bongo , Wema Isaac Sepetu ' Madam' anapandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kujibu kesi ya kushambuliwa vijana wawili, Rashid Balazi na Juma Bushiri , wakazi wa jijini Dar , Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.

HAYUKO PEKE YAKE

Katika kujibu kesi hiyo , Madam Wema hatakuwa peke yake kwani mpambe wake , Petit Man naye anahusika katika kesi hiyo kwa kuwa ndiye mshtakiwa wa kwanza .

KESI YENYEWE NI IPI ?

Hivi karibuni kabla Madam Wema hajasafiri kwenda nchini Ghana kufanya kazi na staa wa huko , Van Vicker , Petit Man alidaiwa kuhusika kuandaa mchezo mchafu wa kuwateka na kuwashushia kipigo cha mbwa mwitu Rashid na Juma, tukio ambalo lilichukua nafasi nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani , Kijitonyama jijini Dar .

Ilidaiwa kwamba , Petit Man alipoteza simu na kuwahisi vijana hao ambao mmoja wao alikuwa ni fundi bomba ,ambaye alikuwa akitengeneza bomba nyumbani hapo.Mmoja wa vijana walioshambuliwa kwa kipigo nyumbani kwa wema.

WALIVYOWA- TEMBEZEA KICHAPO

Baada ya kuwabana vijana hao na kutotoshelezwa na majibu yao , ilidaiwa kwamba Petit Man , kwa kushirikiana na Wema waliwaita vijana wa kihuni ' mbwa mwitu' na kuwafungia nyumbani kwa Wema kisha kuwapa kipondo ' hevi ' ili watoe simu hiyo lakini hadi dakika za mwisho walikataa kuwa hawakuchukua.

WASHITAKI MABATINI

Ilifahamika kwamba walipoachiwa baada ya kusulubiwa , vijana hao, wakiwa na majeraha ,walikimbilia Kituo cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu Mabatini na kufungua jalada la kesi namba KJN /RB /11250 /2014 na KJN / RB / 11220 / 2014 SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI . Hata hivyo Wema na Petit walikamatwa na kuachiwa kwa dhamana kisha walisafiri nje ya nchi.
KESI KUUNGURUMA LEO

Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya mahakama hiyo, Wema na Petit Man watakuwa kizimbani asubuhi ya leo , kujibu mashtaka yanayowakabili ya kuwasulubu kwa kipigo cha mbwa mwizi vijana hao wawili. "Wema na Petit Man watapandishwa kizimbani Jumatatu (leo ) , kesi imewakalia vibaya , kifungo njenje katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni tayari kwa kujibu kesi ya shambulio la kudhuru mwili kwa mujibu wa shitaka lililofunguliwa kituoni hapo.

"Kimsingi Wema kaponzwa na huyo Petit Man na ukizingatia tukio lenyewe lilifanyika nyumbani kwake . "Hapo kesi ya Wema itakuwa ni kuthibitisha kama kweli tukio lilitokea nyumbani kwake siku hiyo na kwa nini aliamua kuruhusu ukiukwaji wa sheria kutokea nyumbani hapo wakati yeye kama mkuu wa familia alikuwepo na hakutoa taarifa ya aina yoyote kwenye mamlaka ya juu ya serikali , " kilidai chanzo chetu .

Hata hivyo , habari zilizolifikia gazeti hili wakati linakwenda mitamboni zilieleza kuwa bado Wema na Petit Man walikuwa hawajatua Bongo .Siyo mara ya kwanza kwa Wema kufikishwa mahakamani kwani aliwahi kushtakiwa kwa kesi ya kumpiga mtu na ile ya kuvunja vioo vya gari la aliyekuwa msanii wa filamu , marehemu Steven Kanumba.

Credit: GPL
 

Attachments

  • 1419321477179.jpg
    54.8 KB · Views: 2,410
Wema na mahakama ni sawa na maji na samaki!!
 
Mhhhhh,shoga na wewe una ki 'vanilla' chako nini?

mmh mi kivanila changu ni kibinadamu kabisa, kijibwa nakiogopa...
naeza kukiambia kilambe mchudhi chenyewe kile hadi nyama si majanga hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…