Wema Sepetu, Lulu, Hamisa na Tessy Chocolate wapagawa na uwezo wa Zuchu

sinza pazuri

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
3,344
Reaction score
9,066
Mastaa wa kike wenye ushawishi mkubwa haswa kwa wanawake na wenye mamilioni ya mashabiki, wameonyesha kuchanganyikiwa na kipaji pamoja na kazi za Zuchu msanii wa kike toka WCB.

Wamekuwa wakipost mfululizo wakiserebuka na nyimbo nzuri za msanii Zuchu.

Wataalam wa mambo ya muziki wamesema hii ni ishara nzuri kwa msanii huyu kutoboa zaidi kimataifa.

Ama kwa hakika Zuchu kapendwa na kila mtanzania. Kongole kwake.

 
Ukitaka Kiki town lazima uwatumie hawa jamaa wa WCB in either way, positive or negative.
 
alafu huyu zuchu ana likiuno flani hivi lain kama urojo
Na hichi ndicho nilichokiona na kasura kake kazuri..
Mkuu hivi mbinguni tutafika kweli..πŸ˜‚
 
Zuchu mnamchukia BURE.
Ila yuko vizuri..
Wala habebwi na brand ya wcb.
Unaanza kwanza uwezo alafu ndo brand
 
@sinzapazuri Yupo good ana vocal nzuri Sana nilianza kumkubali kwanza kwenye zile jingles alizokuwa anafanya wasafi media alafu anajua kubadilika naamini soon ataanza kuleta Radha tofauti na hii ya sasa nilijua Hili kupitia ngoma yake ya two by two akiwa hapo bado hajasainiwa wasafi hiyo ngoma acha kabisa Ni club bang fulani hiv amaizing.Kwa sasa nakubali ngoma yake ya #Raha
 
Kuna WAtu wanapata tabu kwelikweli,.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…