Wema Sepetu: Msinifanye mimi kuwa daraja, Sitahudhuria maombi yaliyotangazwa na huyo Mchungaji

Wema Sepetu: Msinifanye mimi kuwa daraja, Sitahudhuria maombi yaliyotangazwa na huyo Mchungaji

Pastor Commando lazima apige hela wiki hii. Yaani nimecheka aisee!
Wema kawa ubaya badala ya wema hataki mwenzake avune sadaka pia hapendi ulokole kwani akiokoka ataacha kwenda night club kujiachia viwanja mbalimbali.
 
Wema si atende wema aende lakini wagawane sadaka kiwema zaidi.
 
View attachment 924809

Muigizaji Wema Sepetu ameonesha kuchukizwa na kitendo cha mchungaji kutaka kutumia jina lake kama sehemu ya kupata watu wengi watakao hudhuria ibadani kwake kwa kusema kuwa atamuombea.

Wema Sepetu ameamua kuvunja ukimya na kusema hatoshirki kwenue maombi hayo ambayo mchungaji huyo amekuwa akiyatangaza.

“Hakuna kitu kinachouma kama kuhusishwa kwenye jambo nisilokuwa hata na habari nalo.
Naona sasa inakuwa TOO MUCH…
Hizo habari za kuwa na Mkesha wa Ibada sina habari nazo… Nilivyosikia kwa mara ya kwanza nilichukulia poa na pia maana ni sehemu ya kumuomba Mungu nikaona ni sawa”

“Ila sasa naona imekuwa kama “Wasafi Festival” jamani… Maana ni ma Interview na matangazo utasema ni Show, Sababu kwa kuwepo sitokuepo as it is.
Ninaumwa sana na bado sija recover vizuri… So even nilivyosikia kwamba kutakuwa na watu wamejikusanya kufanya mkesha wa Ibada ya kuniombea nilijiskia faraja BUT haikuwa ni kitu ambacho nimepanga mimi”

“INSTEAD I was happy that kuna watu wamenifikiria hata kunifanyia maombi .
Sasa Kaka/Baba angu Mchungaji… Mbona naona kama umenifanya Daraja jamani…
Ndo haya haya Zama aliosema ya kufanywa Daraja…
Nimelivunja DARAJA , Halipo tena…
Na sitokubali kuendelea kufanywa Daraja na mtu yoyote yule”

“Kwenye mambo mengine Inabidi nianze kua MKALI Cause I think its getting outta hand So with all due RESPECT, Natamka Leo hii… Mimi kama Wema Sepetu siwezi kuwepo katika hilo tamasha na haikuwa katika plan yangu.
Naliita tamasha sababu Maombi huwa hayaendi kwa mtiririko huu ".
Mchungaji wa mitume, manabii na maaskofu Tanzania... Duuu
 
Najiuliza hiv ingekuwa Wema yuko kwenye mchakato wa kugombea miss world 2018 na ili kufanikisha hilo pastor komando pia kaandaa ibada ya maombi ya Wema kama alivyofanya ila hajamuambia Wema. Swali ni je Wema pia angevunja daraja? Au kwa kuwa tukio la sasa ni la aibu ndio maana analaumu kutoambiwa kuhusu maombi? Nakumbuka tulifanya ibada za kumuombea Mwal Nyerere apone bila yy wala familia kuambiwa lakini hakukuwa na malalamiko
 
Pastor 'msanii' katafuta msanii mwenzake wakaliamshe, kamwagwa. Hivi, hilo kanisa lina waumini kabisa, na zaka wanatoa, mapambio wanaimba na biblia wanabeba, akili zao zipimwe ASAP!
 
Still naona hajabadilika wala hajajifunza kutokana na makosa yake.
Karudi mapema sana kwenye social networks. Inaonekana hawezi kuishi bila Instagram.
 
Naona sasa Wema Sepetu akili zake zimeanza kurejea mahala pake sahihi tofauti na ilivyokuwa awali. Ni mwanzo mwema na hatua nzuri pia.
 
Inamaana wema siku zote hizi hajui kama anamajini?
 
Sio Sepenga kweli kwenye kale ka-video ka Baba Askofu?
 
Back
Top Bottom