WEMA SEPETU mtoto wa kiislam huyupo hivyo!

WEMA SEPETU mtoto wa kiislam huyupo hivyo!

Mwacheni wema anawashwa yule hajapata wa kumnunga kisawasawa akipata ataacha upuuzi wote na mtashangaa? Wapi sinta?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Maimamu kwa kupenda uroda, hapo ameshatangaza tenda kwa Maimamu na Masheikh ubwabwa.
 
wengine wakiambiwa wataje listi yao wanajaza costa tatu, ila wanamshangaa wema......
 
Hakana dini inayoruhusu uzinifu wala matendo machafu. Na mwanamke mwenye akili timamu hawezi kutangaza wanaume alotembea nao hadharani. Ni upuuzi mtupu.
 
wengine wakiambiwa wataje listi yao wanajaza costa tatu, ila wanamshangaa wema......


Ha ha ha kuna mtu aliwahi niuliza nikamwambia akasema yaani wewe hata Hiace haijai? Mimi Dar Express kumi hazitoshei itabidi niongeze Saibaba, Kilimanjaro Express, Mohamed trans na Ngorika ndo zitatoshea
 
Wengine wakipangwa mstari wanatokea posta mpya hadi chalinze mzee!
wengine wakiambiwa wataje listi yao wanajaza costa tatu, ila wanamshangaa wema......

Ha ha ha kuna mtu aliwahi niuliza nikamwambia akasema yaani wewe hata Hiace haijai? Mimi Dar Express kumi hazitoshei itabidi niongeze Saibaba, Kilimanjaro Express, Mohamed trans na Ngorika ndo zitatoshea
 
Mtoa mada amekerwa na wema 'kukiri' hiyo list. Na hapo hajataja wale waume za watu na wanasiasa. Bora anaejitamvua yu mkosaji manake dhamiri itamsuta atubu. Kuna wale holier than thou, anatembea na tasbihi na huku ni teja wa dhambi kadhaa. Hao hawakumbuki kutubu!
 
Kumbe watu wanaishi na misheni za kujaza mabasi,,,,
 
labda mtoa thread nawe ushadate na wangap??? usmnyooshee kdole mwenzio kumbe nawewe una msururu km msafara wa rais
 
wewe unaishi kama mafundisho ya dini yako yanavyotaka?

Pia ajiulize alitaka Wema ajikane kwamba yeye ni mtoto wa kiislam halafu aseme yeye ni dini gani???haoni kama angeikana imani yake angepata dhambi juu ya dhambi!binadam unaeishi duniani pigania kwanza nafsi yako je u-safii!usi- judge nafsi ya mtu wote dunian hakuna alokamilika jitengenezee njia yako mwenyewe ulieleta huu uzi.
 
waarabu waliwafanya dini gani ya kulazimishana na kuangalia matendo ya watu badala ya kujiangalia wewe unaangalia watu dini zitawapeleka vibaya
 
Habari wana JF wenzangu hopeful mpo poa!
Jana usiku nlikuwa natazama kipindi cha THE MBONI SHOW katika kituo cha runinga namba 1kwa vijana Tanzania EATV chini utangazaji wa mwanadada MBONI MASIMBA ambapo katika kipindi huwa ana walika wegeni tofauti tofauti kuzungumza mada mbalimbali za kijamii,kiutamaduni,kimapenzi nk.

Kwa show ya jana alikuwa na bongo moves star Wema Isack Abraham Sepetu wakijadili mada ya Uwazi katika Mapenzi ambapo mwanadada Wema bila kupepesa macho wala kutafuna maneno alitiririka kinagaubauga kuhusu maisha yake ya kimahusiano ya mapenzi,ambapo aliwataja wanaume wote ambao kwa nyakati tofauti amedate nao.

Wanaume wao ni pamoja na Marehemu Stephen Kanumba,Jumbe,TID,Mr Blue,Chalz Baba na hivi karibuni Dimond Platinum"sukari ya warembo"Kwanza niseme nlikuwa sifahamu kama Wema ni Binti wa kiislam!ila ni katika show hiyo ya jana nlifahamu kutokana na Wema mwenyewe kujiita mtoto wa kiislam pale alipokuwa anajitetea au kujibu maswali aliyokuwa akibanwa na aidha wanaalikwa kwenye show au host wa kipindi Mboni Masimba.

Lengo la thread hii siyo kuutazama na kujaji uislamu wa Wema ila kilichonisikitisha ni jinsi Wema alikuwa anajificha katika kivuli cha mwamvuli wa dini ya kiislam kwa mambo mbalimbali aliyokuwa akiulizwa!Ni ukweli usiopingika kuwa matendo anayofanya Wema ni kinyume kabisa na mafundisho ya dini ya kiislamu au jinsi binti wa kiislamu anatakiwa aishi,mojawapo ikiwa ni hilo la kukiri kufanya zinaa na wanaume zaidi ya watano kabla ya ndoa tena hadharani.

Ni aibu kubwa Wema Kujivunia uislamu wake wakati matendo yake yapo kinyume kabisa na mafundisho ya dini hiyo!

Wito wangu kwa dada Wema na mastar wengine ambao wana majina ya kiislam waache haka katibia cha kujiita mtoto wa kiislam wakati dhahiri shahiri metendo,tabia na maadili yao haviendani na mafundisho ya dini ya kiislamu kwani wanaidhalilisha uislam na waislamu ni vyema wakakaa kimya tu wasifiche uchafu wao kwa kujiita watoto wakiislamu!Uislam kama dini ni mfumo mzima wa maisha wenye maadili sheria na taratibu zake ambazo Wema anatakiwa kuzifuata kabla ya kujinadi kuwa yeye ni mtoto wa kiislam!

Mwisho napenda kumsihi dada yangu Wema kumrejea Muumba Wake kama ilivyoamrishwa ktk kitabu chao kitakatifu cha Quran!
Uchiwakemwacheni mean I kun a speedometer kilaa anaepita aikja mwingina inasoma 0
 
Back
Top Bottom