Wema Sepetu: Mwanaume pekee ambaye najutia kutozaa nae ni Kanumba, ila wengine sijutii hata kidogo

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mwigizaji na mshindi wa zamani wa Miss Tanzania, Wema Sepetu, ameweka wazi hisia zake za ndani kuhusu safari yake ya mahusiano, akieleza kuwa marehemu Steven Kanumba ndiye mwanaume pekee anayejutia kutopata naye mtoto.

Wema amebainisha kuwa kipindi alipokuwa kwenye uhusiano na Kanumba hakuwa na changamoto yoyote ya kiafya ya kupata ujauzito, bali maamuzi ya ujana na utoto wake ndiyo yaliyomfanya atende mambo yasiyoelezeka yaliyopelekea msanii huyo nguli wa filamu kumchukia sana kabla ya umauti wake.

Akizungumzia wanaume wengine aliyowahi kuwa nao baada ya Kanumba, Wema ameeleza kuwa hana majuto yoyote ya kuachana nao au kutopata nao watoto, kwani hakuna cha thamani wala cha msingi walichoweza kuongeza kwenye maisha yake.

Hata hivyo, amemtaja mwanamuziki Whozu kama mwanaume wa tofauti sana na wa pekee kwake. Wema amekiri kuwa angeumia mno kama asingebahatika kupata naye mtoto, akimsifu Whozu kama mwanaume wa kweli aliyeonyesha msaada na thamani kubwa kwake, tofauti na mtazamo wa jamii inayowachukulia wanaume wengine kuwa bora machoni mwao.
1790148631503.png
 
View attachment 3676214
Sepenga tupumzishe ,tupo na YBWYB -Mamba 24 - Hali ni MBAYA.
 
Back
Top Bottom