Wema Sepetu nakupenda sana na huu ndio ushauri wangu

Nimeufurahia ujumbe wake kwa ccm tu. Hamna shukrani. Ngoja niwaambie dunia mapema kuwa ccm, hawanaga shukrani, hawaangalii mchango wako kwao baada ya kuingia ndani. Nadhani hili ndilo alilotaka sote tujue
 
Hahaha Paganism mpito miaka 60? Mtafika lini huko mwendako? Mpaka Yesu arudi?
 
Angekuwa hana effect yule mama Suluhu Hassan asingezunguka naye kwenye kampeni nzima akimtumia Wema Sepetu kama main striker wake, pamoja na madudu ya Wema Sepetu but usiundermine influence yake
Biashara anayo fanya ni ya misimu! Kama ua linavyo chanua na kusinyaa!
 
Naanza kuamini kuwa mlimbwende Wema alidanganya umri kwa wenzake akina Lowassa ujana wamekula CCM halafu uzee wao wameenda kumalizia CDM, namuona Wema akienda kumalizia uzee wake CDM.
"Eti ameshindwa kumtoa Zari kwa Mond ataweza kumtoa Msukuma magogoni..."
 
Hahahaha
 
Babu aliniambia, " Mjukuu wan gu hata siku moja usikate mti wakati wa kiangazi ukiamini kuwa mti huo umekufa( hautachipua tena), subiri mvua zinyeshe usipotoa majani basi jua hakika umekufa." Hii ni wakati aliponishauri kuwa kuna hatari kubwa ya kuchukua maamuzi ukiwa na joto hasira!! Kuna status ya jamaa yangu mmoja huwa inanifundisha kitu, yeye ameandika ," Jifunze kunyamaza". Naheshimu maamuzi yako dada Wema, ila naombea uwe hujayafanya ukiwa na joto hasira.
 
Kwa hiyo kama umemwaga damu (sijui damu ya nini) basi watu wengine hawatakiwi kuingia? Acha ubinafsi wewe
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wema Wacha afanye analoona sahihi hajui serikali ya huyu Msukuma hainaga ushemeji. Alitaka wamdekeshe na akati hata alipokuwa Mwanza na waigizaji wenzake chumbani kwake watu walikuta nini? Kama anatumia bangi au madawa yoyote aache tu hiyo ndiyo njia pekee. Na kuhusu yeye kwenda Chadema, namshauri aende kwa Kujua kuwa Chadema ndiyo chama kimbilio la Wanyonge nasio kupelekwa na Msongo wa mawazo au kufikiri kuwa akienda atamkomoa Makonda. Makonda ni msomi ukitaka kumkomoa nenda shule kwanza na uje na mawazo yenye tija zaidi kuliko yeye.
 
Ameondoka Lowassa Sahizi hatujui hata yuko wapi mzee wa Mafuriko! Kaondoka Sumaye sahizi hatuji hata kama yupo Tanzania Au wapi na Mashamba Kanyang'anywa.....Kaondoka Kingunge naye hatuji alipo potelea .......sembuse Wema Sepetu? Sio kitu cha kukaa kujadiri.....Atadaiwa hadi hadi kodi ya kutembea huyo na lipstick zake zitaaambiwa hazina Kiwango na TBS ngoja tusubiri
 
Yaani Mm nachoka na hichi kizazi cha sasa HV huyu wema ana impact gani ktk maisha yenu ,yaani hao wasanii sijui upuuzi gani ,hebu fanyeni.kazi.nyie ndo mnazidisha kuwafanya wafanye upuuzi tu
 
Wema Sepetu Wema Sepetu.

nyota inayozizima,tatizo liko wapi?

1.kukosa washauri wazuri kuanzia katika ngazi ya familia.
2.Kukosa marafiki wa ukweli (friendship is earned not given)
3.kujihusisha na magenge/marafiki wasio na maana (Crowd psychology)
4.mahusiano ya kimapenzi yasio na tija i.e TID

nakusikitikia sana Wema nakusikitikia sana una mtaji mkubwa wa watu lakini umeshindwa kuutumia
 
Please Wema, Please Wema narudia tena, naomba unisikilize katika dakika hizi za mwisho usiende Chadema. Tafadhali, usiende Chadema. Nakijua sana hicho chama unaenda kupotea kabisa... Katika kipindi hichi bado una hasira za Makonda usithubutu kutoka CCM.... Unamarafiki wengi CCM hivyo ni rahisi kusurvive kuliko huko..

Usifanye maamuzi saizi una hasira. Nakupenda sana sana, naomba usiende CDM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…